MAONI: Serikali iboreshe mfumo wa ukataji tiketi SGR

DustBin

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2021
Posts
609
Reaction score
604
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Najikita moja kwa moja kwenye mada husika. Naiomba serikali iboreshe mfumo wa ukataji tiketi kwenye tren yetu ya mwendokasi SGR. Nalisema hili kwa sababu nimeshuhudia zaidi ya mara moja mfumo unaonesha tiketi zimeisha (nafasi zimejaa) lakini ukisema vizuri na wahudumu unapata nafasi. Hii nahisi inaweza kuleta mwanya wa wahudumu wasio wazalendo kupiga (kwa lugha isiyo ramsi). Nachelea watu wakanunua risiti za mkononi kwa gharama (bei) ya juu zaidi ya kawaida, hivyo ikawanufaisha wachache wasiopenda maendeleo ya nchi yetu.


Natoa maono haya kama mwananchi mpenda maendeleo, ambaye ninanufaika kwa kiasi kikubwa na uwepo wa SGR. Kwa hili naipongeza serikali na pia Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan.
#kaziiendelee
 

Attachments

  • 1733660212443.jpg
    253 KB · Views: 2
Nyongeza baadhi ya vijana walioko eneo la ukaguzi mizigo hasa Dodoma (umri kati ya 19-26) hawana maadili mazuri wana lugha zisizo na staha na vitisho kwa abiria eti ni wawakilishi wa usalama wa taifa. Wananyang'anya asali kutoka kwa abiria ambazo zimepita kwenye mashine ya utambuzi (scanner) eti hairuhusiwi!!!. Kwanini wafanyabiashara wa asali na zabibu wameruhusiwa kupanga biashara zao nje ya geti la kuingilia ambapo kuna walinzi wa JKT Suma wananunua na kuingia getini wakiwa wanawaona bila kuwakataza?
 
Kuna ubabaishaji mkubwa sana
 
Nina imani litafanyiwa kazi
 
TRC walikuwepo huku walitolee hili ufafanuzi tafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…