Maoni: Tatizo la Kujifanya Usalama wa Taifa na Kuongeza Lawlessness

Maoni: Tatizo la Kujifanya Usalama wa Taifa na Kuongeza Lawlessness

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
7,427
Reaction score
10,905
Tanzania imechukua hatua kubwa katika kuboresha miundombinu yake kwa kukamilisha ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR).

Huu ni wakati muafaka wa kuimarisha mifumo ya usafirishaji na kuhifadhi mizigo kwa kujenga Bandari Kavu (Dry Ports) katika mikoa ya Morogoro na Dodoma.

Faida za Bandari Kavu Morogoro na Dodoma:
  1. Kupunguza Msongamano wa Malori
    Bandari Kavu Morogoro na Dodoma zitapokea mizigo kutoka Bandari ya Dar es Salaam kupitia SGR, na hivyo kupunguza idadi kubwa ya malori yanayoelekea jijini Dar es Salaam. Hii itapunguza msongamano wa magari, hasa katika barabara ya Morogoro-Dar, ambayo kwa sasa ina msongamano mkubwa sana na kufanya safari kuwa nyepesi kwa magari mengine ya abiria na biashara....(mathalani kwa sasa ukitaka kufika Morogoro kutokea Dar kwa barabara kwa sasa ukiwa na gari dogo itakuchukua hadi masaa matano au sita mahala ambapo unapaswa kufika kwa masaa yasiyozidi matatu...ukifika tu pale Kibaha Maili moja foleni kali sana)

  2. Kuboresha Ufanisi wa Usafirishaji
    Bandari ya Kwala iliyopo Pwani inaweza kutumika kuhifadhi mizigo kama magari ya IT (In-Transit), wakati mizigo mingine itaendelea kusafirishwa hadi Morogoro au Dodoma kwa usafirishaji wa ndani na nje ya nchi hasa mzigo bulky na wa kontena. Hii itapunguza muda wa usafirishaji na kuongeza ufanisi wa biashara na kuwawezesha wateja wetu wa Congo,Rwanda, Burundi,Zambia,Malawi,Zimbabwe nk kufikia mizigo yao kwa haraka na kupunguza urasimu na kuokoa muda kwa kuwa huko mikoa ya Morogoro, Dodoma na Pwani (Kwala) land mass ni ya kutosha inawezesha mizigo kutolewa kwa haraka.
  3. Kukuza Uchumi wa Kanda za Ndani
    Bandari Kavu zitatengeneza fursa za ajira, biashara, na uwekezaji kwa mikoa ya Morogoro na Dodoma. Pia, zitasaidia kurahisisha biashara kwa nchi jirani zinazotumia Bandari ya Dar es Salaam kama Uganda, Rwanda, na Burundi.
  4. Kulinda Miundombinu ya Barabara
    Kupunguza idadi ya malori yanayotumia barabara kuu kutasaidia kuongeza muda wa maisha wa barabara zetu kwa kupunguza uzito wa magari makubwa yanayopita mara kwa mara.
  5. Kupunguza Uchafuzi wa Mazingira
    Usafirishaji wa mizigo kwa kutumia SGR badala ya malori utaongeza matumizi ya usafiri wa reli usiochafua mazingira, na hivyo kuchangia juhudi za kuhifadhi mazingira.
Mapendekezo:
  1. Serikali na sekta binafsi zishirikiane kuhakikisha ujenzi wa Bandari Kavu Morogoro na Dodoma unafanyika kwa haraka.
  2. Bandari ya Kwala iimarishwe ili kuhifadhi mizigo ya IT na magari ya kusafirisha ila mzigo mwingine tofauti na magari ya Transit uende Morogoro na Dodoma.
  3. Kuanzishwa kwa sera madhubuti ya usimamizi wa mizigo inayosafirishwa kupitia SGR na Bandari Kavu ili kuondoa changamoto zozote za kiutendaji.
  4. Maoni haya yaongezwe kwenye #Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ukiwamo upanuzi wa TAZARA kuwa SGR mapema iwezekanavyo ili kuhudumia Southern Corridor.
  5. Kwa kuzingatia maendeleo haya, Tanzania itaimarisha nafasi yake kama kitovu cha biashara na usafirishaji wa kikanda, huku ikiendelea kukuza uchumi wa ndani na kuboresha maisha ya wananchi. Au mnaona wananzengo.
  6. dry-port (1).jpg
 
Mods tafadhali Rekebisheni Headline ya hiyo Sledi isomeke: Wazo la Ujenzi wa Bandari Kavu Morogoro na Dodoma litapunguza foleni ya Malori Morogoro road
 
Bora hata umejirekebisha mwenyewe kwenye heading maana nilikuwa sielewi
 
Back
Top Bottom