Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Leo ni siku nyingine tena Rais Samia Suluhu aka Mama amepata wasaa wa kuhutubia wateuzi na taifa kwa ujumla.

Hotuba yake imesheheni matumaini mapya, lugha laini na rahisi kueleweka na kila mtu.

Mama ameonyesha kuifahamu nchi na matatizo yake kwa ujumla.
Amegusia karibu nyanja zote za kijamii, kiuchumi nakadhalika.
Huko kote ameonyesha kuwa naye anahitaji kuona mabadiliko hasa katika huduma bora.

Jambo lingine muhimu zaidi amwonyesha kuwa pamoja na kufukua cv za wateule wake pia hufuatilia sana maoni ya wananchi kupitia mitandao ya kijamii, hii ni habari njema kabisa kuwa wengine tusiokuwa na access naye moja kwa moja tutakutana mitandaoni.

Jambo lingine muhimu ni kuqgiza vyombo vya habari vilivyofungwa vifunguliwe ili asionekane anakandamiza uhuru wa habari...hongera nyingi.

*******

Nimetumia kauli hii (kuwa ni mtamu) nikimaanisha kuwa Mama amevuta hisia za wengi kumaikiliza, lugha yake na lugha ya mwili/body language vinafufua matumaini mapya kwa wengi wafanyabiaahara, wakulima na wafanyakazi.

Tangu aapishwe kuwa rais wa JMT anga la Tanzania limekuwa jepesi mno, kuna tumaini jipya, mwelekeo mpya na amani ya moyo.

Mambo haya machache yamwnifanya nimuone kuwa huyu mama ni Mtamu.

ANGALIZO KWA MAMA
1. Utaimbiwa kila nyimbo tamu/praise and worship na kila kada hadi nyumba za ibada

2. Utaitwa mteule wa Mungu

3. Tutajikomba sana

Nakuomba usilewe sifa zetu.
Sisi hawahawa tunaokusifu ipo siku tutakupeleka msalabani kukusulubu uchi na viboko juu.
Kukwepa hili jitahidi kuyaishi haya unayoyahubiri itakusaidia usisulubiwe sana.

Mungu akutie nguvu
 
Ndg wana JF 'GT's' salamu kwenu!
Nimekuwa mfatiliaji mzuri sana wa namna Rais wa awamu ya sita Mhe. Samia Suluhu Hassan anavyotupeleka Watanzania.

Hakika hotuba zake zimejaa matumaini makubwa ya kuipeleka Tanzania kwenye uchumi wa kati ngazi ya juu! Kila sekta ameizungumzia kwa namna kubwa ya jicho la tatu.

Nilichogundua wale wakosoaji wa hayati JPM RIP wamekosa cha kuandika wamebaki wanambwelambwela!! Nadhani posho kutoka upande wa pili imekata.

Nimegundua udhaifu wa Hayati Rais Magufuli kwao ulikuwa ni mtaji mkubwa, na sasa uwezo wa Mhe. Samia Suluhu Hassan kwao ni hasara kubwa!! Watuacheeeee!! Mhe. Hayati JPM amejenga misingi na mama anapandisha kuta huku akirekebisha mapungufu ya Msingi! Mungu ibariki Tanzania.

Tuendelee kumuunga mkono hakika yajayo yanafurahisha!!
 
Kama kichwa habari kinavyojieleza ....kwa kweli kwa sasa naweza sema Mama Samia ni mama lao...au mama la mama...katuonyesha mawingu hakuna shaka mvua itanyesha....ongera kwa mwanzo mzuri...
 
Hakika anajua kuongea kwa weledi anatumia ukali pale panapohitajika na anafata sheria. Pengine tunyamaze kwanza tumpe kwanza muda but dalili zinaonekana Tanzania inaenda kuwa yenye furaha tena. Yaani hii sasa ndo tunaiita Win Win situation ya vitendo yani nchi itaingiza mapato na wananchi pia uchumi wao hautashuka.
 
Mungu kafanya vizuri sana kutuondolea mwendazake.

Wakatoliki tulikuwa na Novena ya kimya kimya Mungu akajibu maombi, na tunaomba ashikishwe adabu huko aliko.
 
Mimi huwa unanikera sehemu moja tu! Kuleta mada zako katika mfumo wa vijembe na taarab nyingi!

By the way, ni mapema sana kutushawishi. Aturudishie kwanza Bungeni ule Mchakato wetu wa Katiba Mpya ili tuwe pamoja.
 
Pia mama ni hivi hapo makao makuu Lumumba, kuna vijana wanaitwa buku7 mama, wapo kiumbea umbea hawana shughuri yoyote zaidi ya propaganda, tena mama nimesahau wanajifanya usalama wa taifa, eti mama si bora wakalime. Mama kama mama.
 
Ni mapema sana. Ngoja tumpe muda ili tuijue rangi yake halisi. Hata mtangulizi wake alipoingia madarakani, alitupa matumaini lukuki! Ila mwisho wa siku akaishia tu kutunyoosha.

Sisi Watumishi wa umma kamwe hatuto msahau.
 
Pia mama ni hivi hapo makao makuu Lumumba, kuna vijana wanaitwa buku7 mama, wapo kiumbea umbea hawana shughuri yoyote zaidi ya propaganda, tena mama nimesahau wanajifanya usalama wa taifa, eti mama si bora wakalime. Mama kama mama.
Hahaha umekandamizia mule mule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…