Maoni, Ushauri, Mapendekezo na Pongezi kwa Rais Samia Suluhu Hassan

Akifanya mwanaume sawa....
Leo anafanya mwanamke tena kwa udogo tu... kelele zinaanza.
 
Mimi huwa unanikera sehemu moja tu! Kuleta mada zako katika mfumo wa vijembe na taarab nyingi!

By the way, ni mapema sana kutushawishi. Aturudishie kwanza Bungeni ule Mchakato wetu wa Katiba Mpya ili tuwe pamoja.
Mkuu umeshasoma katiba inayotumika ya 1977 na ukaielewa na ile pendekezwa(rasimu ya katiba au proposed constitution) na ukaona iliyopo inashida gani au na we una muunga mkono Anti pasipo kujua.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kila rais na zama zake...tusifananishe.................
 
Huwezi toa hutuba umenuna tuu muda wote utawachosha wanaokusikiliza,kwani sio kweli maumbile yake ni kike je macho yake hayajalegea utani uko wapi!
Kasi ya usaliti kwa marehemu Jiwe imekuwa kubwa hata wewe ? Unakosoa utawala wa malaika mkuu .
 
Tafadhali kuwa na heshima yule ni Rais wa Tanzania.

Ingekuwa mama yako ungefurahia kuambiwa hivyo?

Uhuru wa kusema usizidi mipaka na kukiuka heshima na tamaduni zetu.
Nipeleke polisi basi kama nimevunja Sheria
 
Mzee magufuli kuna siku alisema kuhusu upara wake akiwa jukwaani kwamba upara wake sijui umefanyaje nimesahau.

Sasa leo mama anasema macho yake yamelegea kuna ubaya gani mkuu ?

Macho ni yake na ni kweli yako hivyo kama ambavyo magufuli mzee wetu upara ulikuwa na wake na ni kweli upo hivyo.

Sasa ambona hatukuwahi kuwasikia mkipiga kelele kuhsu mzee magufuli kuzungumzia upara wake badala yake unakuja leo unamsema mama wa watu ambae kachukua Nchi kwa rehema za Mungu.

Kwa nini usiambiwe una roho mbaya dhidi ya raisi wetu mama SAMIA. ?
 
Jamaa alipopewa kuku tuu “ ntakupa mama yangu hata umlee kidogo”
Sheitwan muflisi.
 
Nakuhakikishia Safari yako itakuwa ni nyepesi sana endapo utayafanya haya Mambo MANNE (4), MH: MADAM kwa haraka ikiwezekana ndani ya kipindi cha mwezi mmoja na NYOTA yako itazidi kung'ara

(1) MPE AMRI DPP AFUTE KESI YA MASHEKH WA UAMSHO ILIYODUMU ZAIDI YA MIAKA MINANE BILA USHAHIDI KUKAMILIKA (NOLE PROSEQU)

(2) PANDISHA MISHAHARA KWA WATUMISHI WA UMMA WALAU KWA 100% YA MISHAHARA YA SASA! ITASAIDIA SANA MZUNGUKO WA FEDHA MITAANI NA KUFUTA MACHUNGU YA MIAKA TAKRIBAN MINANE

(3) LIPA FIDIA KWA WALIOBOMOLEWA NYUMBA ZAO KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA UBUNGO KIMARA

(4) TANGAZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA WANAFUNZI WOTE WENYE SIFA IWE NI LAZIMA KUPATA MIKOPO HIYO NA WAKATI HUO HUO REJESHA KIWANGO CHA RIBA YA MAREJESHO YA MKOPO KAMA ILIVYOKUWA AWALI ASILIMIA 8

KWA HAYO TU TAYARI MADAM UMESHAJINYOOSHEA NJIA FOR 2025 PRESIDENCY KAZI NI LAINI SANA NI SAWA NA KUMSUKUMA MLEVI
 
Ila mama awe makini sana na madini yetu pamoja na kuleta chanjo ya corona nchini..ki ukweli hatuhitaji chanjo Kabisa..
 
(4) TANGAZA MIKOPO YA ELIMU YA JUU KWA WANAFUNZI WOTE WENYE SIFA IWE NI LAZIMA KUPATA MIKOPO HIYO
Mkopo sio lazima pia sheria za mkopo zinataka ukopeshe mtu uliye na uhakika atarejesha

Ndio maana selikali.ilikuwa ikikopesha kwa fani hasa za sayansi za udaktari ,engineering na ujenzi sababu hao wana uhakika wa kujiajiri au kuajirika

lakini unampa mtu mkopo wa digrii ya business administration au history unategemea nini? mkopo hautalipika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…