Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Yeye hausiki na kashfa ya crdb kuajiri wachaga tuu??? Naomba jibu
 
Hii ni dhana kongwe ya kimtazamo iliyojengeka kifalsafa. Ni uwezo wa mwanadamu katika taswira moja kuwaona viumbe wawili wenye kufanana. Hivyo, inahusu uwezo kuliona jambo hilo hilo katika sura tofauti. Ndio, kuna kuona kikiwa na kuona kama. Kuliangalia jambo kwa mtazamo tofauti.


Mwanafalsafa Thomas Kuhn yeye anazungumzia dhana ya ' Paradigm Shift'. Ni ile hali ya uwepo wa mapinduzi ya kifikra na ya kisayansi yenye kupelekea mabadiliko ya kimsingi katika jambo lile lile tulilokuwa na mazoea nalo.

Captain Thomas Sankara, kiongozi mwanapinduzi aliyeuawa wa Burkina Faso, katika wakati wake, alizungumzia umuhimu wa kuwa na ujasiri wa kuyapa mgongo mazoea ya kale.Sankara aliacha hiba njema ya kuenziwa ndani ya nchi yake, Afrika na duniani.

Mwanamapinduzi huyu alikuja kuawa kwa kupigwa risasi na wapinga mapinduzi na maendeleo ya Burkina Faso.

Sankara alipata kukaririwa akisema: ?Ningependa kuacha nyuma yangu, imani ya kuwa, kama tunaimarisha kiwango fulani cha uangalifu na oganaizesheni, basi, tunastahili ushindi.

Kamwe huwezi kuleta mabadiliko ya kimsingi bila ya kuwa na kiwango fulani cha uwendawazimu. Hali hii inatokana na kutoshinikizwa na taratibu zilizozoeleka, kuwa na ujasiri wa kuzipa mgongo kanuni za kizamani, ujasiri wa kuanzisha mustakabali. Ni wendawazimu wa jana waliotuwezesha kuyafanya tuyafanyao leo. Ninataka kuwa mmoja wa wendawazimu hao.? (Hayati, Kapteni Thomas Sankara)


Yumkini tunachokishuhudia kwenye nchi yetu ni Magufuli's paradigm shift'. Hali ya kuwa na mabadiliko ya msingi. Kuna wanaoshangaa John Magufuli kuchelewa kutangaza Baraza lake, yawezekana Magufuli anaonyesha kwa mawaziri wake wajao, kuwa nchi inaweza kwenda bila uwepo wa mawaziri miungu watu. Wakifanya mchezo wanatimuliwa.

Na hii ya Magufuli paradigm shift inaweza kuibadili nchi kwa haraka, maana kila mmoja atalazimika kubadilika.

Maggid

 
Na wale Wafanyabiashara waliochangia kampeni za CCM nao?uchaguzi ushaisha sasa kilichobaki ni kuunganisha nguvu kuijenga nchi yetu.Dr Kimei kumuunga mkono Lowassa hakumuondolei sifa ya kuhudumu kama Waziri,kama anakidhi vigezo na achaguliwe tu.Hata Marekani Obama alimchagua Hillary Clinton kama Secretary of States licha ya kwamba alikuwa hasimu wake mkubwa wa kisiasa. Pia aliwachagua Republicans watatu ktk cabinet yake,unfortunately we Africans have turned politics into hostility. I wish you could learn about the diversity accommodation and the role it plays in bolstering the organisation's activities in this modern day world we living in.

Kimei usitoke crdb hapo baki katika kuzidi kuijenga maana ninaona hiyo ya kumshawishi raisi hakupe kitengo ni mtego kuna mtu ananyemelea nafasi yako
Usishabikie vyeo vya kisiasa havina tija.
 
Hafai kabisa huyo Kimei. Yeye ndiye aliyekuwa anaratibu mkakati wa wafanyabiashara na taasisi za fedha kumhujumu Magufuli wakati wa kampeni. Kimei ni mkabila sana. Kimei aliona kuwa Lowasa ndiye Rais na akafanya kila jitihada kumhujumu Magufuli. Ilifikia hatua alichangisha kwa nguvu wafanyakazi wa CRDB fedha kwa ajili ya kampeni za Lowasa. Huyu mtu hafai kabisa na wala hastahili hata kufikiriwa

Hafai kwny chama chako bali anafaa kwa maendeleo ya nchi! Ifike mda tuache kushabikia mno vyama vyetu bali tuungane tujenge nchi yetu! Lizaboni change the u think about politics!
 
Last edited by a moderator:
hakuna mwenye jeuri ya kumuondoa zaidi wa wazungu waliomuamini wakamkabidhi benk yao,au kwa akili yako unadhani kimei ni mteule wa rais, la hasha hakubebwa yule bali wazungu walimuona anatenda vizuri wakampa na maeipaisha ile benk hadi wazungu wameona wamuache apige mzigo

kumbe crdb ni ya wazungu?
 
Hafai kabisa huyo Kimei. Yeye ndiye aliyekuwa anaratibu mkakati wa wafanyabiashara na taasisi za fedha kumhujumu Magufuli wakati wa kampeni. Kimei ni mkabila sana. Kimei aliona kuwa Lowasa ndiye Rais na akafanya kila jitihada kumhujumu Magufuli. Ilifikia hatua alichangisha kwa nguvu wafanyakazi wa CRDB fedha kwa ajili ya kampeni za Lowasa. Huyu mtu hafai kabisa na wala hastahili hata kufikiriwa
lete ushahidi
 
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema hatuwezi kuwa na rais ambaye hatujui kesho akiamka atasema nini au ameambiwa na mke wake afanye nini. Kwa kuzingatia hayo niliandika humu hatuhitaji rais kiranja bali waziri mkuu wa aina ya kiranja tunaweza kumvumilia

Sasa ni tofauti, rais anaonekana kiranja na waziri mkuu anaonekana rais. Najiuliza kama rais ndiye angeenda bandarini wakati wa kumtimua mkurugenzi wa TRA nini kingetokea, nadhani hata meza zingepinduliwa pale. Pasingetosha!..

Tunahitaji kuona action plan, tunahitaji kuona mipango endelevu, tunahitaji kujua kilimo kitakuwaje miaka 20 ijayo, elimu, afya, michezo nk. Hizi zimamoto amwachie waziri mkuu.

Umetumbuliwa jipu.
 
Tuwe makini usiku around nyumba zetu,kwa hali jinsi ilivyo unaweza ukaamka ukakuta wamekuwekea kontena nje......hii hali sio shwari.
 
hakuna mwenye jeuri ya kumuondoa zaidi wa wazungu waliomuamini wakamkabidhi benk yao,au kwa akili yako unadhani kimei ni mteule wa rais, la hasha hakubebwa yule bali wazungu walimuona anatenda vizuri wakampa na maeipaisha ile benk hadi wazungu wameona wamuache apige mzigo

CRDB ilishauzwa kwa wazungu?

Halafu una taarifa kwamba Karl Peters alikuwa mzungu pia?
 
Huyu c ni yule aliekua anakalili mpaka urefu wa barabara,ngoja atafatilia adi centi100
 


Dr. Kimei ni CEO wa a giant bank hapa nchini, anavuta super salary ya 100 milion plus!, wakati Dr. Magufuli ni mjamaa na mbana matumizi, jee ataweza kumlipa Dr. Kimei?!. Yaani umtoe mtu kwenye neema, umtupe kwenye dhiki?!.

Pasco

Naamini humaanishi hapo kwenye red, hakuna CEO wa benki hapa Tanzania anayepata salary ya TZS 100.00 million. Labda ulimaanisha salary yake pamoja na pesa anyaopata tokana na ma-deal mengine!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom