Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Utakasaji wa zile noti za 500 fake
Samaki wa Magu--
Barabara chini ya kiwango
 
Naona moto utawaka muda si mrefu katika sekta hii ilyojaa makandokando. Wakati wake umeshapita na sasa JPM anajipanga kupitisha fagio katika eneo hili, tumuombee rais wetu.
 
Yaani tabia yenu ya kuamini kwamba hamkosei na watu wa kwenu hawastahili kukosolewa ndio inatutoa imani. Pia mtu akiwaunga mkono ata kama ni muovu vipi ninyi kwenu sawa inatufanya tusiwaamini kabisa. Mimi nimekuambia watu hapo CRDB wanaajiriwa kwa misingi ya ukaskazini hali ya kuwa boss ni Kimei full stop siitaji kukulazimisha wala hauwezi kunishughulisha kwa lugha zako za hovyo.
 
Mh. Rais tunaomba uiangalie na dawasco magomeni, maaan kuna nenda rudi za hatar, huduma hazitolewi, ikifika saa tano, hamna mtu ukiuliza, unaambiwa wameenda site. Wanasema mfike asubuh mkiwah kufika wanavikao mpaka sa nne, wakitoka hapo chai, na wanatokomea huko huko!!!!
 
TRL Tanzania Railways Limited na mikataba gandamizi! Wafanyakazi trl kilio kila kukicha awasikilize kilio chao.
 
Nadiriki kusema wapi mwenyezi Mungu ulipokuwa umemficha Magufuli hadi tukafika sehemu ya kukata tamaa watanzania.Pengine ulisubiri asome matatizo yetu,Pengine ulisubiri akomae,watanzania nijuzeni huyu Mussa alifichwa wapi hadi tukatumikishwa na kunyonywa ktk ardhi yetu.
 
Habari wana JF!
Moyo wangu umefurahishwa sana na mwanzo mzuri, hotuba nzuri, mwendendo safi, kasi ya ajabu na kazi kweli kweli iliyo na kifani bila woga kwa rais wetu JPM. Najua haya ni matunda ya uzalendo wapatao walimu wanaopitia katika kazi hizi za uwalimu. Kama kweli mh. Ni mzalendo asilimia 100% akiendeleza wembe huu huu,apate washauri wazuri basi Tanzania tutauaga umaskini na amini kwa afrika mashariki na kati uchumi wetu utakua maradufu. Wigo la ajira litapanuka. Sera ya viwanda na utekelezaji wake ukifuata misingi bora tutafika mbali sana. Suala la kubana matumizi ndani ya mashirika ya umma likienda sambamba na kupunguzwa kwa wafanyakazi ndan ya halmashauri zetu ambao hawana kazi zozote wapo tu au waliwekwa kwa kujuana juana tu,lengo ni kuziba nafasi tu za watu walosomea katika vitengo hivyo. Nahisi yataleta manufaa kwa taifa letu. Matazamio haya unadhani tanzania baada ya miaka 10 itakuwa ni nchi yenye mafanikio sana kwa asilimia ngap?
 
Rekebisha kwanza jina, ni Magufuli na siyo Magifuli, pia mpe hishima yake, jina lianze na Dr. au uweke PhD baada ya jina, huyo aliisotea shule hiyo title siyo sawa ma zile za kugawiwa
 
Rekebisha kwanza jina, ni Magufuli na siyo Magifuli, pia mpe hishima yake, jina lianze na Dr. au uweke PhD baada ya jina, huyo aliisotea shule hiyo title siyo sawa ma zile za kugawiwa



Vibaka wa lumumumba ndio wanashtuka usingizini.


swissme
 
Miradi ya watoto wa vigogo wakubwa ndani ya chama wanaokwepa kulipa kodi (kama wapo)
 
Hao ndo hataree kwa kwenda mbele. Pembe za ndovu,twiga,kobe....
 
jipu la vyama vya siasa latumbuliwa.

2020 rudhuku za vyama kupungua asilimia 70, na rudhuku hizo za campaign marufuku kununua kofia, kila mtu achonge yake
 
Siku chache zilizopita tulichanga kiasi cha shilingi laki 4 kwa ajili ya kununua zawadi ya kumuaga mfanyakazi mwenzetu aliyekuwa amestaafu kisheria...
sijawahi kuona kadhia hii.

Tulikubaliana kununua Shati kadhaa nadhifu na vitenge pamoja na Microwave ya kupashia moto chakula,katika hali ya kushangaza baadae niligundua kwamba shati zilinunuliwa "serembua" na "microwave" haikua mpya maana ilionekana na vi"waliwali" ndani.....hii inamaana mnunuzi "alitupiga" na alitupiga hadi "lunch" yetu.

Watanzania tuna ugonjwa wa "upigaji" sio kwa viongozi wa ngazi ya juu tu bali hii imeshuka hadi uku chini.Tumeharibika!!

Maisha hayaendi bila rushwa na wizi wa waziwazi kama huo apo juu...

Sasa kwa vile mheshimiwa rais ameamua kutumbua majipu naamini kuna majipu ambayo hataweza kuyatumbua maana yatakuwa yamejificha sana.Wito wangu kwenu kila mtu atafute jipu na aanze kulitumbua.Iwe na mfanyakazi wako wa ndani, iwe ni mkeo, iwe na mesenger wako naamini kila mmoja ana mnyonge wake.

Ni kampeni maalum ya utumbuaji majipu, naanza na beki tatu wangu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…