Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.

naunga mkono hoja
 
Kama kuna jamaa aliniambia ni Mburundi?

Watu wengine ni 0 brain kweli! Inamaana kila mtu anayetoka Kigoma sio raia wa Tanzania?!!!

Mbona hamsemi hata wale wa jimbo X waliomchagua mbunge X aliyeshindwa hata kuapa bungeni kwa maandishi ya Kiswahili?!!
 
Jibu alilitoa Waziri wa Elimu Mh. Shukuru Kawambwa. Soma hapa kisha rudi tujadili...


kwa nini agawanye kwa tatu badala ya mbili matokeo ya islamic knowlegde?..akadai ni tatizo la kiufundi japo ilitokea kwa somo hilo tu,mengine ni sarakasi za kisiasa tu
 

Pondaism is a bad disease than cholera. Magufuli tangaza siku ya usafi.
 
KAMA UKO SERIOUS.MH RAIS.BASI hII KANDA.MAALUM DAR YA.KINAKOVA INAITAJI.MABADILIKO HARAKA SANA ..AIJALISHI UNAJUANA.NANANI.KWA SPEED UNAYOTAKA WATAKUANGUSHA TU KAMWE HUTOWEZA ENDA.NAO

NAKUTAKIA.MAFANIKIO MEMA NA KAMA UAMINI ENDELEA KUWAACHA HAPO UTAKUMBUKA SIKU YA LEO
 
Yaani wewe una F ya math na Biology unasema umefelishwa somo la dini..!?
ndalichako mswahili ametoka sasa rudi uchape kazi
 
Shida yako wewe huleti hivyo vipande vyenye mashiko, unaishia kusema mambo bila ushahidi.

Na mambo uyasemayo ni ya uongo, na kwa kuwa ni ya uongo huwezi kuleta ushahidi. Mimi nimekuletea ushahidi ambao unaweza kuupata toka tovuti ya NECTA

http://www.necta.go.tz/opendata/data/csee/CSEE2013_RANKING_40_AND_MORE.pdf

Wewe hauna ushahidi wowote umebaki na chuki ambayo haina msingi wowote. Pole sana

Dr. Ndalichako mwenyewe hata huo uwaziri hauhitaji, hapa wanazungumza watu wanaomfahamu vema.
 
kwa nini agawanye kwa tatu badala ya mbili matokeo ya islamic knowlegde?..akadai ni tatizo la kiufundi japo ilitokea kwa somo hilo tu,mengine ni sarakasi za kisiasa tu

Swali lako analijibu Waziri mwenyewe. Soma tamko hili la Waziri wa Elimu Mh. Shukuru Kawambwa, na yeye sijui alikuwa anadhulumu Waislamu???!!!.



Ukishasoma, kama umeelewa vizuri, rudi hapa tuendelee kujadili.
 
Yaani wewe una F ya math na Biology unasema umefelishwa somo la dini..!?
ndalichako mswahili ametoka sasa rudi uchape kazi

Ahaaaaa "Mshwahili" keshapumzika yakhee! Ila kaharibu elimu yetu na hiyo "BRN". This is an area JPM has to work hard on it by involving big brains like Dr.Ndalichako.
 
Swali lako analijibu Waziri mwenyewe. Soma tamko hili la Waziri wa Elimu Mh. Shukuru Kawambwa, na yeye sijui alikuwa anadhulumu Waislamu???!!!.



Ukishasoma, kama umeelewa vizuri, rudi hapa tuendelee kujadili.

kisha kwa nini waligawanya kwa mbili baada ya malalamiko?..siwezi kusoma blablah hzo
 
Hatutaki wabaguzi wa kiimani serkalini! Huyu mama alitolewa kwa sababu za kubagua wanafunzi wa kiislam kwenye usahihishaji mitihani ya taifa. Hatutaki,taifa limejaa wasomi wengi wenye weledi hatutaki wabaguzi.

Chuki tu ndiyo inayokusukuma kutoa maoni yenye nia ya kuchochea ubaguzi wa kidini. Hakuna ushahidi wowote wa tuhuma zako dhidi ya Dr. Joyce Ndalichako.
 
kisha kwa nini waligawanya kwa mbili baada ya malalamiko?..siwezi kusoma blablah hzo
Mbona hayo yote kaeleza Kawambwa vizuri sana? Maelezo ya Ustaadh Kawambwa unayaita Blabla?

Kwa hiyo Kawambwa muongo?

Wewe mtu ambaye hutaki kurejea vyanzo vya habari vinavyoaminika, na kisha unakuja hapa na chuki zako ambazo hazina msingi wa ukweli hustahili jina la great thinker.

By the way, inaonekana kuna watu wana picha kuwa Dr. Ndalichako alikuwa akifanya kila kazi ya NECTA, kutunga mitihani, kusahihisha, kuingiza kwenye computer, kuingiza formula kwenye computer, na kukagua majina ya watu ili awabague.

Ni mpumbavu tu ndie anaweza kuamini hivyo. Wanafunzi wanaofanya mtihani ni zaidi ya 500,000 kwa mwaka. Tena wa shule ya Msingi, Sekondari na vyuo vya elimu. Haiwezekani mtu mmoja afanye yote. Ndivyo Kawambwa anavyoeleza. Watu wa kitengo cha IT ndio wanaoingiza kwenye computer, na ndio wana formula. Na Kawambwa ameelezea vizuri kilichotokea. Sasa wewe unayekataa ukweli kwa chuki zako, utakufa na gubu lako..

Kwa taarifa yako Wakuu wa Shule za Kiislamu waliiandika barua Wizara ya Elimu kushukuru jinsi tatizo lilivyoshughulikiwa

Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.-Tamko la Kawambwa
 
Ama kweli vichwa vingine vibovu sana. Yaani unamtaja mbibi aliyesjindwa just a part of wizara kisha umtwishe wizara!? By the way rais anajenga umoja wa kitaifa hawezi kumteuwa mzembe aliyesababisha migongano baina ya watanzania kwa misingi ya kupendelea. Yaani nimemshangaa sana huyu mleta mada
 

Mkiambiwa kichwani hamna mnalalamika. Jamaa kachangia kwa figures wewe unaropoka tu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…