Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Rais anawafahamu sana hawa ni suala la muda tu, ukifika majipu yatatumbuliwa tu.
 
Wanasuburi Magu aitishe mkutano wa kuwasamehe kwani nchi.hii waafungwa wezi wa kuku tu
 
Yan ukisoma hii list kuna maswali mengi sana ya kujiuliza!
 
Watoto WA Mama Mdogo dili chafu ndo zao, toka Ngada, Ujambazi n.k.....wapo Wao then kwa kulalamika hao?
 
bhakresa katufanya kitu mbaya sana,muungano ufe tu arudi kwao.
 
Mali zao zikamatwe na kupigwa mnada kufidia deni.
 
Nilimsikia vizuri sana mhe raisi; hakulalamikia wizi (remember alikua bado waziri na it sound yalikua mazungumzo na washikaji zake wa kitaa). Alichokisema ni kwamba; kwanini Barrick/Acacia wasijenge hicho kiwanda cha kuyeyusha Ag, Fe na Cu hapa hapa nchini? Tunashindwaje kutengeneza tanuri lenye centigrade 1500 tu.
 
Upo sahihi kabisa, kuna wadau wa bandari kimsingi bila kuwaangalia kwa umakini italeta shida sana
 
Mkuuu kama watanzania wote wanaona mbali kama ww nchii hii ingefika mbali lkn wengi ni watu wa mihemuko ya matukio, bila kujua whgs behind hayo makafara ya kuwatoa head wa tra, bandari na katibu uchukuzi.
 

Uhauri wangu kwa Mhe. Rais TMAA ivunjwe kabisa na shughuli zake zifanywe na Geological Surveyu of Tanzania maana wanakila nyenzo za kufanya shughuli hizo , nasikia mwanzo ilikuwa shughuli hizo zifanywe na GST likapigwa zengwe
 
Kwa nini mheshimiwa Rais asimpe Kikwete ukamanda wa watumbua majipu nchini maana tunajua wengi anawajua kwa majina na hata kwa sura.

Rais akimuona JK anatumbua kwa kulegeza mkono au akiyaacha kwa makusudi majipu yaliyoiva anabananishwa hapo hapo.
 
Aiiseee... Twiga,Tembo ,Magogo na Kobe wanatoroshwa...
Madini ni Jipu
 

Songoka,

Habari Mkuu? Hili suala la mchanga kutoroshwa kwenda nje ya nchi inatakiwa uwe na uelewa wa hali halisi ilivyo naona na wewe pia wengine wanachangiaa kuwa kwa nini Tanzania inashindwa kuwa na tanuri la centigrade 1,500. Hapa kinachotokea ni watu kukosa uelewa kuhusu huu mchanga unaoongelewa hapa. Kwanza ili nchi iweze kujenga huo mtambo wa ku-smelt huo wanaouita mchanga wa dhahabu inatakiwa iwe inauwezo wa kupata kiasi fulani cha mchanga huo ili uweze kujiendesha kibiashara. Ili mtambo uweze kujiendesha kwa faida unahitaji zaidi ya tani 150,000 za mchanga kwa mwaka , na Tanzania inazalisha chini ya tani 50,000 kwa mwaka. Watu hawajui kuwa ni migodi miwili tu ndio inazalisha huo mchanga ambao ni Bulyanhulu na Buzwagi, Hii inamaanisha kiasi cha mchanga wa dhahabu unazalishwa na migodi hiyo haiwezi ikatosha kiasi kinachotakiwa ili faida ipatikane. Ni sawa sawa mtu kwa kuwa unahitaji unga wa sembe uamue kununua mashine ya kusaga na kuiweka nyumbani kwa ajili ya kusaga unga kwa ajili ya chakula. Ni kweli utapata chakula lakini utapata hasara kwa kuwa utakuwa na mashine kubwa lakini unakiasi kidogo cha kusaga. Pia duniani nchi zinazoongoza kuzalisha mchanga huo ambao kwa kitaalamu unaitwa copper concentrate hupeleka mchanga huo katika nchi za China na Japan kwa hiyo sio Tanzania tu inapeleka copper concentrate huko hata nchi za Canada, Australia, Chile n.k

Vilevile, gharama za kujenga mtambo wa chini kabisa wa ku-smelt copper concentrate ni USD milioni 800 sawa na Shilingi trilioni 1.7. Mtambo huo hauwezi kujiendesha kwa faida kama utakuwa unachenjua tani 50,000 kwa mwaka wakati uwezo wake ni tani zaidi ya 150,000. Pia mitambo hii inahitaji umeme mwingi sana ndio maana inajengwa katika nchi zinazotumia umeme kutokana na nyuklia. Tanzania bado haijaweza kuwa na umeme mwingi kiasi hicho.

Hapa tatizo sio kwanini mchanga huo unasafirishwa kwenda nje ya nchi, cha muhimu ni kuhakikisha kuwa kilichomo ndani ya hayo makontena yanalipiwa malipo yote yanayostahili na hiyo ndio kazi inayofanywa na TMAA. Kabla makontena hayajaondoka tayari Serikali inakuwa tayari imeshalipwa mapato yake.
 
Uhauri wangu kwa Mhe. Rais TMAA ivunjwe kabisa na shughuli zake zifanywe na Geological Surveyu of Tanzania maana wanakila nyenzo za kufanya shughuli hizo , nasikia mwanzo ilikuwa shughuli hizo zifanywe na GST likapigwa zengwe

Vile vile ili kupunguza gharma tuondoe SDuplication ya Wakala maana kuna wakala zinafanya kazi zinazofanana mfano GST , TMAA na STAMICO itasaidia kupunguza gharama za serikali.
 
unachoeleza kinaweza kuwa sawa, lakini mimi sikuungi mkono!! bado utaratibu mzima uko kifichoni mno au ni lugha za kuwaambia watz hawawezi hata kuwekeza kwenye vitalu vya gesi maana ni ghaaali sana,
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…