1. Mh Rais, sitisha hili zoezi la bomoa bomoa kwa makazi na nyumba za wanadamu. Hakuna mtu anayependa kuishi kwa tabu na shida. Watu wamepoteza maisha tayari kwa kihoro, na mashinikizo ya damu; hasa wazee. Watanzania wasiku-reflect tena kuwa wewe ni muharibu wa makazi ya Watanzania.
2. Tengeneza mazingira ya kuwalipa wazee wetu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki, malipo yao. Kumbuka unapowahehimu wazee, unamgusa Mungu moja-kwa-moja.
3. Nyumba za ibada (za dini zote) zisibughudhiwe kwa namna yoyote ndani ya utawala wako, ndipo baraka zitakapoendelea kukujilia na kukupata. Barikiwa JPM.