Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Ni sheria gani unayoisema? Hapo hakuna mali ya wizi na hata kama mtu akinunua mali ya wizi toka kwa mamlaka zinazotambuliwa kisheria, hawezi kuhusishwa kumiliki mali ya wizi. Kwa mfano wewe unakwenda kwenye duka linalouza Redio ukanunua Redio na risiti ukapewa, halafu ije igundulike kumbe Redio uliyonunua ni miongoni mwa redio zilizoibiwa Bandarini, huwezi kushitakiwa kwa kumiliki mali ya wizi,hapo sheria itakulinda!!Kisheria ukinunua mali ya wizi hata kama umepewa risiti halali waweza fungwa.vivyo hivyo hilo ghorofa,hata kama lina hati iliotolewa na manispaa lakini kwa kuwa ni kosa kujenga juu ya bomba,basi ni haki yake kuvunjiwa
Halafu suala hilo linahusu mambo ya Ardhi na umiliki wake na mambo ya mipango miji. Kwanza huwezi kujenga Jengo kama hilo bila ya kuwa na Hati ya Umiliki wa Ardhi,ambayo hutolewa na Kamishina wa Ardhi baada ya kupitia Ngazi mbali mbali ikiwa na pamoja na mtaa kilipo kiwanja. Hao wote hawakujua hapo linapita bomba la Mafuta, kwani kwenye Ramani zao hakuoneshi kwamba hapo kuna bomba la TAZAM linapita?
Wewe unajua waliojenga juu ya Bomba hilo kwa kutokujua au kwa makusudi wapo wengi sana hasa kwenye mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Mbeya?