Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kisheria ukinunua mali ya wizi hata kama umepewa risiti halali waweza fungwa.vivyo hivyo hilo ghorofa,hata kama lina hati iliotolewa na manispaa lakini kwa kuwa ni kosa kujenga juu ya bomba,basi ni haki yake kuvunjiwa
Ni sheria gani unayoisema? Hapo hakuna mali ya wizi na hata kama mtu akinunua mali ya wizi toka kwa mamlaka zinazotambuliwa kisheria, hawezi kuhusishwa kumiliki mali ya wizi. Kwa mfano wewe unakwenda kwenye duka linalouza Redio ukanunua Redio na risiti ukapewa, halafu ije igundulike kumbe Redio uliyonunua ni miongoni mwa redio zilizoibiwa Bandarini, huwezi kushitakiwa kwa kumiliki mali ya wizi,hapo sheria itakulinda!!

Halafu suala hilo linahusu mambo ya Ardhi na umiliki wake na mambo ya mipango miji. Kwanza huwezi kujenga Jengo kama hilo bila ya kuwa na Hati ya Umiliki wa Ardhi,ambayo hutolewa na Kamishina wa Ardhi baada ya kupitia Ngazi mbali mbali ikiwa na pamoja na mtaa kilipo kiwanja. Hao wote hawakujua hapo linapita bomba la Mafuta, kwani kwenye Ramani zao hakuoneshi kwamba hapo kuna bomba la TAZAM linapita?

Wewe unajua waliojenga juu ya Bomba hilo kwa kutokujua au kwa makusudi wapo wengi sana hasa kwenye mikoa ya Dar es salaam, Pwani, Morogoro na Mbeya?
 
Hapa common sense itumike. Apigiwe hesabu za kupitisha bomba sehemu nyengine. Hilo jengo linatia sura ya mji na kuweka mazingira mazuri.

Dah kwa hiyo Sheria zisifuatwe tena? Je si atatokea mwingine ajenge barabarani au kwenye njia juu ya umeme na busara itumike kupindisha barabara au njia kuu ya umeme,?
 
wenyewe wanasema ni kiwanja chenye hati. lakini bila shaka ni eneo la bomba la tazara ila ikamegwa na kuchongwa kiwanja. ukweli ushajulikana ndio maana wameambiwa wavunje.
 
Acheni uzushi hii ni hoteli ya tiagi masamaki hebu mwacheni.huyo one one

Mkuu kiroho safi tu..

Ndiomaana nimesema nasikia.... mean sijathibitisha...(Understand now?) Uwe na Amani na huyo Oneone huna haja ya kupaniki, Kama jengo si lake kinakupakachua kitu gani? Calm down kama uko kihalali utakuwa hivyo siku zote... hata kama akatokea mwendawazimu akadai wewe ni haramu.. ebooooooh

BACK TANGANYIKA
 
Hivi itakuwaje kama wakipitisha hiyo sehemu nyingine ambayo nayo ina nyumba za watanzania wengine ambao wapo nje kabisa ya eneo la bomba........?......nimewaza tu kidogo.........
Pembeni ya hiyo Hotel kuna Morogoro Muslim University sasa kwa ushauri huu wa eti busara itumike inabidi wavunje University!!!
 
Hiyo si ipo pale Morogoro round abaut?

Nasikia ni ya bwana mmoja hivi tajiri sana anaitwa one one... Daaah mbona majanga haya!!!

BACK TANGANYIKA


Mkuu hiyo Hotel Ni ya Bosi mmoja WA TRA,ila kamwandikisha jina la umiliki ndugu yake ambaye ndiyo Meneja WA Hotel kwa sasa!
 
No comment
1450505069444.jpg
 
Hıvı vyuo viliharibika baada ya kuanza kusajili wanafunzi wa shahada ya kwanza.Vilitakiwa kubaki na hadhi ya kuandaa technicians.Hawa ndo mafundi halisi na hata ufundishwaji wao ulikuwa wa vitendo zaidi.DIT,Mbeya Tec,NIT kwisha habari yake.IFM,CBE,AIA,ISW,TIA nao kwishine.Wazalishaji na watendaji walitoka taasısı hz lakn kwa sasa zimejaa vijana etı wanasomea digrii wangali ufaulu wao nı wa dıv 3-4.Haupaswi kusomea digree straight ukiwa na ufaulu wa dıv.3 au 4.
 
Awali nimpongeze Rais JP Magufuli kwa jitihada anazoonesha hadi sasa katika uongozi wake. Lakini ni wazi kuwa uozo unaosafishwa sasa usingekuwepo kama usingelelewa. Hivyo kwa maoni yangu Rais mstaafu JM Kikwete amehusika kwa namna moja ama nyingine kuulea. Ndiyo maana nasema Rais Magufuli ukitaka kufanikiwa rais mstaafu JMK akamatwe ili asaidie polisi. Kwa ama kuyalea yote haya ama kuhusika. Ni maoni yangu tu.
 
Jaman mbona cjaelewa inamaana bomba lipo chin mita ngap mpaka ghorofa linajengwa juu wakat ujenz wa ghorofa msing lazma uwe chin zaid naomben mnieleweshe kam kuna anaelewa kuhusu hlo bomba
 
Mkuu hiyo Hotel Ni ya Bosi mmoja WA TRA,ila kamwandikisha jina la umiliki ndugu yake ambaye ndiyo Meneja WA Hotel kwa sasa!

Poa mkuu

Nimekupata kwa uzuri kabisaaa, Si unaelewa tena tetesi za mitaani..

BACK TANGANYIKA
 
Mkuu Tanzania hii au nyingine ya kufikirika, maana kwa hii tunayoishi ndani yake hilo wazo lako haliwezi hata kufikiriwa, ukiacha kutamkwa tu maeneo husika.
 
Alichimbwa mkwara juzi pale lumumba akatangaza baraza lisilokamilika ndo ataweza kumshika born h?re h?re jk .ndoto za mchana jk ndo anweza kuamua h?ta sasa jamaa akamatwe na yy achukue urais
 
Dah kwa hiyo Sheria zisifuatwe tena? Je si atatokea mwingine ajenge barabarani au kwenye njia juu ya umeme na busara itumike kupindisha barabara au njia kuu ya umeme,?
.

Katika kila kesi KISHERIA, hiyo unayotaka kuzungumzia kuna kitu kinaitwa "mitigating circumstance". Jaji akitaka kupitisha hukumu mahakamani huwauliza mawakili, "Is there any mitigating circumnstace in this case? Akiwa na maana ikiwa kuna jambo linalofanya hii kesi ipunguwe nguvu.

Huyu muwekezaji itakuwa kapata vibali vyote kutoka serikalini, kama ni kufata sheria basi zichunguzwe hizi nyaraka zake kwanza halafu serikali iwajibike kwa upande wake. Suala la kuvunja jengo linalogharimu mabilioni kama hili si la kulichukulia masihara. Uwe na uhakika 101% na unachokifanya na iwe vichochoro vyote vya sheria vimefatwa.
 
Jamani tusiendelee kupotosha,kilichojengwa juu ya bomba la TAZAMA ni jengo la generator na sehemu ya uzio na ndivyo vinavyotakiwa kuvunjwa.

Kama ni hivyo basi kuna upotoshaji mkubwa sana siku hizi. Hata mimi akili ya kawaida iligoma kabisa kuwa jengo la ghorofa zote hizo liwe juu ya bomba. Kwa waliosoma Foundation Design atakubaliana na mimi kuwa Depth/kima tu cha msingi si chini ya Mita 2-3, sasa isingewezekana kabisa. Matamko mengi yanakuzwa sana na vyombo vya habari na ili kupata cheap popularity, na kwa ukweli awam hii matamko ya kwenye vyombo vya habari tena papo kwa papo bila kupata data sahihi yametamalaki. Kabla ya kufoka ni bora kujiridhisha kwanza!
Nafananisha na enzi za Naibu mmoja Waziri enzi za Kikwete alikua TAMISEMI, panapostahili kuongea kawaida anafoka, panapotakiwa kufoka bado anafoka, sasa inakua ni full Lugha Gongana.

Busara itumike zaidi wakati tuko kwenye TRANSITION kuelekea TANZANIA ya WATANZANIA WELEDE NA WAADILIFU. Tukienda kwa papara zaidi tutajikuta tumeacha majeraha makubwa kumbe pengine tungeweza KU PHASE OUT MFUMO UOZO taratibu taratibu!
 
Operation TANESCO inayoendelea imekuwa chachu sana kwa baadhi ya watu na shirika limekusanya hela sanaa.

Zoezi hili napendekeza liwe na kwa DAWASCO watu wengi wamecheza michezo yao kuwaibia.

Zoezi hili muweke na TAKUKURU na Polisi wafanyakazi wenyewe wanafanya miradi yao ya kuongeza kipato, wanalipwa hela ndefu tu wanakuja kuwafungia mita mpya.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom