Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hili suala ni la kimfumo na linaanzia chini from the roots.
Mfano hai: Reli imekufa kabisaaa hii ilikuwa inachangia sana ktk usafiri wa wanafunzi kutoka sehemu moja kwenda nyingine kwa urahisi zaidi kitu ambacho kilileta combination ya watanzania wote tukawa ndugu moja.
TRC ilikuwa ina mabasi yake yaliyokuwa yanasaidia usafiri wa wanafunzi kuwa rahisi hapa nchini.
Mfumo wa elimu urudishwe kama zamani.
Mwanafunzi anatoka Zanzibar anapangiwa Kilimanjaro, wa Kilimanjaro anapangiwa Mbeya, wa Mbeya anapelekwa Dar, wa dar anaenda Kigoma.
Elimu iboreshwe na elimu iwe ni suala linalosimamiwa na serikali kwa 100%. Shule za binafsi zipungue kama siyo kuisha.
Jeshi baada ya form six lirudishwe mchanganyo wa kambi ni uleule kama mashuleni.
Hivyohovyo vyuoni.
Mpaka tunakuja kufika makazini mchanyiko unakuwa ni hivhohivyo kwa sababu taarifa za muombaji kazi zitakuwa zinajieleza kutoka kwenye CV yake.
Hii itasaidia kuondoa ukabila na udini kwa kiasi kikubwa sana na italeta mshikamano wa watz kwa ujumla.
Leo hii mtoto kazaliwa dosoma kakulia dodoma kasoma Dodoma kuanzia primary-chuo kazi hapohapo dodoma ofisini kapigiwa pande na ndugu yake hapohapo Dodoma sasa kwanini wasiongee kilugha hapo ofisini.
Hili tatizo limetoka chini kabisa
Mtoa mada kwa unyenyekevu mkubwa naomba kuchangia kama ifuatavyo:-
Wakati makabila na watu wa kanda fulani fulani mkicheza vigodoro, baikoko, mchiriku na mnanda. Na wakati wengine mkiwatembeza watoto wenu msituni kutwa nzima kama wanyama ili wachunge mifugo wachaga, wahaya na wanyakyusa waliwekeza nguvu kupeleka watoto wao shule.
Wakati dini fulani fulani zikiweka nguvu kupeleka watoto kwenye mafunzo ya kidini na kuyaita mafunzo hayo kama "vyuo", dini nyingine ziliweka mkazo kwenye elimu dunia.
Sasa watu wa makabila na dini zilizoweka msukumo kwenye elimu kwa watoto wao wamejaa kila ofisi. Na ni utaratibu wa kawaida tu kumsaidia mwenzio unayemjua kuingia ofisi uliyopo. Na wote wanaosaidiwa wana sifa.
Cha msingi hapa ni kumuomba JPM aongeze wigo wa ajira ili na ninyi ambao mna asili ya kuchunga ng'ombe, kucheza vigodoro, mnanda na baikoko mpate ajira.
Ushauri wako ni mzuri lkn matunda yake ni zaidi ya miaja 20 ijayo. Kwa Sasa hivi maofisini nini kifanyike?
Umeongea ukweli mtupu.
Jipu la kuajiri kwa kigezo cha dini na kabila Lipo sana kwenye baadhi ya taasisi za serikali,ukienda TRA 80% ni kutoka kule na ukienda NSSF 90% ni dini Ile.
Well said mkuu...huu wmbo akaimbe mwenyewe apa anazunguka sana mbuyu ila analenga makabila ya kaskazin I. E wachaga...wameru na wapare...jamaa asilolijua ni kua kwenye taasisi nyingi za elimu wamejaa wanafunzi wa kanda ya kaskazin cz watu wa kaskazin wamewekeza kwenye elimu na ukiangalia ata performance wanaongoza sasa unaanzaje kuwanyima kazi??kna Kimei...Nassari...Msuya etc
serikali bado haijatoa vibali vya kuajiri intern wote walio maliza bado wapo mtaani au private usipotosheKuna mdogo wangu ni Dentist mzuri sana alisomea Cuba amemaliza internship Muhimbili miezi michache iliyopita but hadi leo hii hana ajira. Baadhi ya madaktari Muhimbili walimshauri awe lecturer pale na akakubali but hadi leo hana ajira. Nashindwa kuelewa tunaelekea wapi - haya mambo ya udini na ukanda ndio yanayochangia kudumaa kwa utendaji wa serikali na huduma za jamii
Wana JF,
Habaru zenu
Nianze kwa kumpongeza Rais Magufuli kwa uzalendo alionao!
Tumo katika zama za kutumbua majipu. Tumemulika sana upande Wa uchumi au mapato ya serikali. Utumbuaji Wa majipu TRA, TPA, PCCB nk.... ni jambo linalotupa faraja.
Japo tumeangalia uchumi, lakini kuna jipu LA AJIRA KATIKA OFISI ZA UMMA. Naamini ni kubwa kuliko yote.
Watanzania tuna haki ya kupata ajira serikalini kwa misingi ya uadilifu. Zisiangaliwe dini, kabila, koo, eneo tunakotoka na jinsia. Cha kuangaliwa uwe uwezo Wa MTU kufanya kazi husika.
Kwa masikitiko makubwa, ajira serikalini zinazingatia dini, kabila na kanda katika wizara na mashirika mengi. Ukuu wa idara unazingatia dini, kabila na kanda. Huu mdudu umeanza kututafuna na utatupeleka pabaya sana.
Tutajikuta tuna dini fulani au kabila fulani ndiyo limeendelea kiuchumi sana kuliko dini au makabila mengine.
Kuna baadhi ya mashirika kama TRA, TPA, NSSF, baadhi ya mabenki nk...., yamelalamikiwa kuwa na ukabila na udini.
Tumefika mahali tumeanza kusema, kwa mfano, kupata kazi maliasili lazima uwe kabila fulani. Kupata kazi Tra lazima uwe kabila fulani, kupata kazi nssf lazima uwe dini fulani.....
Hii nchi ni yetu sote. Tuna haki ya kupata ajira kwa usawa bila upendeleo.
Namuomba Muh. Rais aunde tume ya kuchunguza jambo hili. Kwa mfano, Je TRA kuna zaidi ya nusu ya wafanyakazi kabila moja au dini moja! Kama ni hivyo kwa nini? Tuendelee na uchunguzi katika mashirika na wizara zote. Penye mapungufu ajira ziitishwe upya na uwiano uzingatiwe.
Bila kufanya hivi, watu wataendelea kuvutana na baadhi ya kabila, dini na kanda zitaendelea kuwa za wasindikizaji. Watoto wao hata wakisoma haitokua rahisi kupenya katika ajira serikalini. Barua za kazi lazima zitaendelea kuwekwa kapuni.
TANBIHI
Tuache mtindo Wa kukwepa kuzungumzia udini na ukabila. Tunazidi kulifanya jipu hili liwe kubwa zaidi na sugu. Kadri linavyozidi ukubwa watu wanazidi kuumia. Rais Magufuli tafadhali Pasua jipu hili.
Ni kweli kabisa kama unatafuta kaZ nssf na we si wa dini ya huyo kionhoz wao huwez kupewa kaz. Hili linalalamikiwa sana. Na ni hatarinsana. Rais tunaomba umulike.san nssf kwa udin.
Kama kuna MTU alishawahi kukukosa ajira akaambiwa Na hiyo mwajiri sababu ya kukosa ni kuwa Ukabila Fulani au Dini Fulani akathibitishe. Mnakosa sifa za kuajiriwa mnasingizia Dini Na Ukabila.Kwa hiyo ukiwa Ukabila Fulani na sifa unazo usipewe kazi pale? Mtakufa kwa wivu na umbeya.George Bush Baba yake GBush Na Jeb Bush, ni familia moja Na wote wana sifa za kutawala USA. Sijapata kusikia mmarrkani alisema hii America si ya Bush's wanaangalia UWEZO Wa MTU. Huku bongo Ukabila Na Dini. Kwani si watanzania hao Na wanafanya kazi Tanzania! Acheni Vijiba vya roho mtakufa. Kubwa zima unamshauri Rais Utumbo.Well said mkuu...huu wmbo akaimbe mwenyewe apa anazunguka sana mbuyu ila analenga makabila ya kaskazin I. E wachaga...wameru na wapare...jamaa asilolijua ni kua kwenye taasisi nyingi za elimu wamejaa wanafunzi wa kanda ya kaskazin cz watu wa kaskazin wamewekeza kwenye elimu na ukiangalia ata performance wanaongoza sasa unaanzaje kuwanyima kazi??kna Kimei...Nassari...Msuya etc
Hili ni nafikiri ni jipu ambalo limekomaa sana, kama ukifuatilia ofisi nyingi ajira zimekua zikitolewa kwa upendeleo ama ukabila, udini, undugu kama hivyo si sababu basi rushwa inachukua nafasi yake.
Nafikiri kutumbua jipu hili kunahitaji mkakati na dhamira ya dhati ya mtumbuaji na watumbuliwaji.
Ndio maana waliosoma wanatafuta kazi ila wenye vyeti feki wanapata kazi kiulaini.
Taifa la kutafutana uchawi kila siku
shida ya Tanzania ni kuwa hatuna 'strong corporate world'
sisi serikali ndie muajiri mkuu
ndo maana tunagombania ajira za serikalini....
kuwa mwalimu wa chuo au secondary TZ ni better kuliko kufanya kazi bank au kampuni binafsi
Kama kuna MTU alishawahi kukukosa ajira akaambiwa Na hiyo mwajiri sababu ya kukosa ni kuwa Ukabila Fulani au Dini Fulani akathibitishe. Mnakosa sifa za kuajiriwa mnasingizia Dini Na Ukabila.Kwa hiyo ukiwa Ukabila Fulani na sifa unazo usipewe kazi pale? Mtakufa kwa wivu na umbeya.George Bush Baba yake GBush Na Jeb Bush, ni familia moja Na wote wana sifa za kutawala USA. Sijapata kusikia mmarrkani alisema hii America si ya Bush's wanaangalia UWEZO Wa MTU. Huku bongo Ukabila Na Dini. Kwani si watanzania hao Na wanafanya kazi Tanzania! Acheni Vijiba vya roho mtakufa. Kubwa zima unamshauri Rais Utumbo.