Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Shikamoo Magufuli,

Mhe sina shaka na utendaji wako ; kwani ni urithi kutoka kwa Baba yako. Naongea hili nikitambua Baba'ko alikuwa Mwenyekiti wa shule Rubabangwe alikuwa na msimamo kwenye mambo ya Msingi.

Nakumbuka Marehemu Baba yangu Mwalimu Borakupata akiwa Mwalimu Mkuu alimfukuza Kazi ya ualimu na utumishi wa umma kwa Kosa la kuacha shule kipindi kirefu akichana mbao polini, alimpa onyo lakini mzee wangu akusikiliza na ilikuja tume na kumfukuza kazi na kupewa adhabu ya kulipa mshahara wa miezi 3, kwa kosa la utoro.

Ingawa Baba ako alitaka kukuachisha shule kwa kumuonga Mzee wangu Mbuzi kutokana na tabia na usikivu wako ; uwe unachunga mbuzi na ngombe mzee wangu alikataa rushwa ya Mbuzi na kumpa onyo kali.

Kuhusu suala la Nyumba za nyasi ni rahisi kuziondoa Chato, Mganza , Buziku na Tanzania nzima kwa miaka 2. Inawezekana kama ukiendeleza msimamo wako na kufanya maamuzi magumu na bora kama urithi kutoka kwa Marehemu Babako.

Machine za mabati zipo na zinatengenezeka na zinaajiri watu wengi , na kutokana na kuwa na viwanda vingi vya Cement ni wakati wa kuleta mashine hizo ambazo bei yake ni ndogo sana.

 
Hivi inashindikana nini kwenda kwenye point moja kwa moja bila utangulizi mreeefu wa kujisifia...!? Au ndiyo jadi ya watu wa Chato.. Loh..
Ushauri mzuri lakini.
 
Kwa nini wasibomolewe tu? NEMC wazibomoe tu, maana hakuna namna
 
Hivi bado bei za vifaa vya ujenzi hazijashuka? Mi nasubiri zishuke ndo nianze ujenzi
 
Kwa magufuli hakuna kitu kitakachoshindikana kila goti litapigwa tu.
 
Hivi inashindikana nini kwenda kwenye point moja kwa moja bila utangulizi mreeefu wa kujisifia...!? Au ndiyo jadi ya watu wa Chato.. Loh..
Ushauri mzuri lakini.
sorry nilionyesha historia ya msimamo wake;
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni viongozi wa serikali kuwa mawakala wa magabacholi, fikra za kitumwa kwamba wananchi wao hawawezi na mengine yanayofanana na hayo.
Kama mheshimiwa Rais akipambana na hayo, maendeleo kwa ujumla yatapatikana tu!
 



Kabla hamjaanza kuota ndoto zenu,mwambieni awasitiri wanaCCM kindakindaki wa Dodoma wanaohatarisha maisha ya ndege kwa kuwalia chakula chao-viwavi jeshi.Wanaloweza kulisimamia CCM tena kwa ghalama yoyote ni Rushwa ya uchaguzi tu,wakati wa kampeni wanauwezo wa kuwasafirisha watu kwa maelfu,kuwahonga T-shirts,chumvi,kofia na kanga.wanaweza kuwanunua wasanii kwa 50,000,000/ kila mmoja.

Hiyo shule yenyewe unayoitolea mfano,watoto hawana kucha vidoleni kutokana na kujikwaa kwenye mawe yaliyotapakaa eneo lote la shule.
 
Kwa nini wasibomolewe tu? NEMC wazibomoe tu, maana hakuna namna
Mkuu japo umeongea kama masikhara lakini inawezekana tu wakaitolea amri kuwa hadi ifikapo mwaka fulani pasiwe na nyumba za nyasi na ikiwepo itabomolewa,afadhali iwe chini udongo lakini juu umepiga bati.
 
Si kila anayekuchekea anakutakia mema,wengine wanafanya kila wawezalo ili kukuharibia ili mwisho wa siku uonekane umeshindwa.

Mgogoro wa Zanzibar,maandamano ya wale vijana waliobeba mabango (placards) yenye kubeba ujumbe wa kibaguzi (racist remarks) na hii bomoa bomoa holela sidhani kama yanatokea kwa bahati mbaya.

Kuwa makini na haya mambo rais wetu, najua unawapenda Watz na umedhamiria kuwafanyia mambo mazuri sana.Kila la kheri!
 
Last edited by a moderator:
HHuu mtanziko wa kisiasa Zanzibar unamharibiavilivyo Mh JPM... Na asipokuwa makini kwenye utatuzi wake na yeye atapotea.o
 
Hilo bomu amefungiwa kwa makusudi na wasiomtakia mema,wapo pembeni kimya wanatabasamu tu, asipobeba ujasiri wa kufanya maamuzi yatakayoenda kinyume na msimamo wa chake basi urais wake waweza kuingia dosari mapema kabisa,he has to take a leaf from Jaji Warioba and his constitution review issue, or else....
HHuu mtanziko wa kisiasa Zanzibar unamharibiavilivyo Mh JPM... Na asipokuwa makini kwenye utatuzi wake na yeye atapotea.o
 
siku akianza kuvurunda umsifie hivyo hivyo
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…