Hali ya Kisiasa
1. Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili
2. Katiba mpya ya JMT ? pengine si ajenda ya chama chako kwa sasa lakini linahitaji dhamira yako ? chonde chonde litendee haki taifa hili
Mfumo na Uendeshaji wa Serikali
3. Uza mashangingi ya Serikali na ubakize machache tu kwa shughuli muhimu. Watumishi wa Serikali wakopeshwe magari na wapewe mafuta ili kuokoa fedha nyingi mno zinazopotea kiholela.
4. Rejesha nyumba za Serikali kwani wananchi wengi hatuna imani kuhusu dhamira, mantiki na umuhimu wa kuziuza nyumba za Serikali
5. Punguza sana idadi ya Wizara na Mawaziri ili kupunguza gharama
6. Boresha kipato cha Watumishi serikalini ili kuwaongezea morali
7. Toa fursa katika vipindi tofauti mikoani ukutane na wananchi wenye matatizo uwasikilize ana kwa ana, mmoja mmoja (uwe rais wa wananchi)
8. Misamaha ya kodi ni donda ndugu linalohujumu Taifa mapato, dhibiti hili kwa nguvu zako zote.
9. Panua wigo wa vyanzo vya mapato ya Serikali ? hili ni muhimu sana
10. Dhibiti safari za nje zisizo za lazima kwa Viongozi waandamizi wa Serikali
Rushwa na Ufisadi
11. Mahakama ya Rushwa na Ufisadi ianzishwe kama ulivyoahidi
12. TAKUKURU ipewe mamlaka ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila kibali cha DPP
Afya, Maji na Mazingira
13. Karabati hospitali za umma (Taifa, Mikoa, Wilaya) ziko katika hali mbaya (Zahanati kwa kila kijiji inawezekana!)
14. Imarisha Hospitali ya Muhimbili ikidhi viwango vya kimataifa ili kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi
15. Panua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili ijumuishe wananchi wote (Rwanda wameweza hili) watakaochangia kiwango nafuu
16. Miji na Majiji ni machafu mno (taka ngumu na maji taka), imeshindikana kubadili hali na inaelekea hakuna suluhisho, inabidi tuzoe uchafu ? tunaomba wahusika wageuke taka
17. Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto iboreshwe kwa nguvu zote
18. Serikal igharimie magonjwa hatarishi ikiwemo saratani na UKIMWI
19. Matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku (Rwanda, Zanzibar imewezekana)
20. Anzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yote
Elimu
21. Wanafuzi wengi wa elimu ya juu hawakupata mikopo kwa mwaka2015/2016? litatue hili kwani ni aibu
22. Elimu ya bure hadi kidato cha nne iwe kweli na yenye ubora
23. Shule ziimarishwe kwa kupatiwa madarasa, maabara, vitabu, walimu na lishe muafaka
24. ?One Computer, One Pupil? ? tujenge taifa la kisasa na linaloendana na mabadiliko ya nyakati kimaendeleo
25. Anzisha Kamisheni ya Taifa ya Ushauri kuhusu elimu
Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda
26. Fufua kilimo cha mazao asilia (mkonge, kahawa)
27. Anzisha Mfuko wa Taifa wa Kilimona Mifugo utakaotoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
28. Imarisha na jenga miradi ya umwagiliaji na majosho ya mifugo
29. Imarisha vyama vya ushirika na viwezeshe kujitafutia masoko
30. Futa kodi zote kandamizi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
31. Anzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi
32. Weka kodi nafuu na shindani kuhamasisha wawekezaji
Miundombinu na Uchukuzi
33. Punguza gharama za vifaa vya ujenzi ili wananchi wengi wamudu kujenga nyumba bora
34. Fufua Shirika la Ndege la Taifa (ATC)
35. Imarisha miundombinu ili kuondosha misongamano katika majiji na miji mikubwa (Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha)