Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Furaha yangu sio ushindi wa CCM ... Ni ushindi wa Mgalatia .... Katika vipindi vinne ya taasisi ya uraisi watz tumeshuhudia Wavaa njiwa na wapiga soga mkiharibu nchi yetu, safari hii kaingia tena mwenye UCHUNGU na Tanganyika...... Mtaisoma namba.
Umechelewa jamvini, karamu imeshaliwa.
Magufuli ameshaanza kazi na kishaanza na mengi sana kuliko unavyotarajia.
Hongera sana.
Huko hunipeleki kwa sasa. Nnaiheshimu sheria ya mtandao ya kutoeneza chuki za kidini kama ufanyavyo.
Hatum-judge mtu kwa dini yake tunam-judge mtu kwa vitendo vyake.
Umechelewa jamvini, karamu imeshaliwa.
Magufuli ameshaanza kazi na kishaanza na mengi sana kuliko unavyotarajia.
Jirekodi video. Kisha anza kuisambaza whatsapp. Itamfikia tu.
Andika tu hapa kile ambacho unataka kusema kwa Rais. It is simple as that.
Rais ndio huyo tena ameshaapishwa, waliomtaka na wasiomtaka ila wote hawa ndio rais wao wa awamu ya tano.
Je, wewe raia ungependa rais aanze na jambo lipi kulitendea kazi au kulisimamia ambalo unaona ni la muhimu na kwa sababu zipi?
- Usikubali kofia mbili; wewe ni Raisi, uenyekiti wa CCM muachie mwingine ili chama kibaki chama na serikali ibaki serikali.
- Washauri Wabunge wa CCM, watangulize maslahi ya taifa mbele ya maslahi ya chama.
- Washauri Wabunge wa CCM kama itawezekana wamchague Spika wa Bunge asiyeegemea upande wowote.
- Pokea ushauri kutoka kwa vyama vya siasa lakini uwe huru kufanya maamuzi kulingana na matakwa ya Katiba ukizingatia maslahi ya wananchi.
- Usiruhusu Ikulu kutumika kwa maslahi ya CCM, vikao vya chama vifanyike nje ya Ikulu.
- Washauri CCM waachie mali za wananchi kwa kuzirudisha mikononi mwa wananchi kupitia serikali.
- Agiza vyombo vya dola vitoe haki sawa kwa wananchi bila upendeleo.
- Futa sheria zote kandamizi zinazozuia uhuru wa kutafuta, kupokea na kutoa habari. Vyombo vyote vya habari viwe huru.
- Hakikisha mikataba yote tunayoingia inawekwa wazi ili vijadiliwe na kupitishwa na Bunge.
- Vikumbushe vyombo vya dola kwamba jukumu lao la kwanza ni kuwalinda Watanzania na mali zao na si kupambana nao.
Amalize swala la Zanzibar mana bado ajawa rais kamili bila Zanzibar