Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mheshimiwa Rais, salaam!

Umeingia madarakani ukiwa na lengo la kuwatumikia Watanzania kwa kuona wanaishi maisha bora na salama.

Lengo hilo limetokana na fursa ya raslimali nyingi zilizopo hapa nchini hivyo wewe kuamini kwamba hakuna sababu ya Watanzania kulia na umaskini kwa kua raslimali hizi zikisimamiwa vizuri zinaweza kunufaisha kila raia wa nchi hii.

Naamini Kuna mpango kazi ambao umejiwekea (priorities) kufikia ndoto ya Tanzania unayoitarajia.

Tukirudi nyuma, tawala zilizopita kuanzia awamu ya kwanza mpaka ya nne Kuna mema zimefanya na Kuna mabaya pia yalifanyika.

Ndugu Rais, baadhi ya wadau wakiwemo na wanasiasa wanataka ufanyie kazi tuhuma mbali mbali za awamu zilizopita, za ubadhilifu wa Mali ya umma.

Kwangu mimi kazi hii ni ngumu sana na ni mtego wa kuhakikisha hufanikiwi katika malengo yako, Kwani muda mwingi utabaki kushughulikia kashfa zilizopita badala ya kuwaletea Watanzania maendeleo.

Huu ni utawala mpya wa awamu ya tano, unavipaumbele vyake.

Nashauli kama ni masuala ya ufisadi hakikisha hayafanyiki kwenye utawala wako kwa kuibana mianya yote ya ufisadi kama mkuu wa nchi, ikiwemo kuengua watumishi wasio waaminifu na kuweka wazalendo zaidi kwenye serikali yako, japo si jambo jepesi kutokana na utamaduni wa watumishi wetu, wa business as usual.

Jukumu la kulinda na kurejesha raslimali za nchi hii ni za Watanzania wote. Wanaharakati, mahakama kama muhimili upo, bunge lipo. ni kazi ya wananchi wenye ushahidi wa tuhuma hizo kuzipeleka maeneo husika kwa ajili ya hatua stahiki, na si kila jambo Magufuli fanya hivi, fanya vile.

Ikizingatiwa hayakufanyika chini ya utawala wako.utakachotakiwa ni kuwa transparent kwa kutoingilia mihimili iliyopo kwa mujibu wa katiba.

Nashauri bana kuanzia sasa, siku hazigandi.
 
Huu ushauri wako haufai! kosa ni kosa tu hata liwe la miaka 20 iliyopita, halafu usiseme Magufuli ndiyo anawashughulikia..it is the GOVERNMENT mhalifu wa jana na mhalifu wa leo hawana tofauti wote ni wahalifu, sheria ni ile ile na serikali waliyoikosea ni ile ile, hawajamkosea Magufuli!
 
Naona rais amesoma post yangu na kafanya comparative analysis

"Rais Magufuli amesema anafahamu vijana hawapendwi lakini amegundua ndio wachapakazi ambao watasaidia kulipeleka taifa ktk maendeleo anayoyatamani. “Nimegundua vijana wengi hawapendi rushwa, hivyo nitaongeza vijana kila nikiteua kwa kuwa niliowaweka naona matunda ya kazi zao,"....“Najua watu wanawachukia sana ila nitawaongeza. “Palipo na vijana nimeona mambo yanaenda na kuna mabadiliko. Wazee ndio tumelifikisha taifa hili hapa"

Kama unaamini kweli vijana watalibadilisha Taifa hili comment 'YES' na kama huna imani nao comment 'NO'
 
Kwa cheo chako ambacho ndio cheo kikubwa APA nchini , tegemea kupata misukosuko kama hii, na mingine itagusa moja kwa moja kwenye familia.
Kwa kumsaidia binti kisaikolojia na kumhakikishia future nzuri omba uongozib wa udom kusitisha masomo ya binti.
Fedha unayo bwana mpeleke uko ulaya au Malaysia binti apate elimu kwani APA bongo imeshakua taabu.
 

Na wale Vilaza aliowasema Wazazi wao watawapeleka wapi?
 
Mh. Rais pole kwa majukumu ya kila siku naomba nikushauri tu jambo moja

Mh.rais baada ya kuingia ikulu miezi kadhaa iliyopita umejitengenezea sifa kubwa kwa utendaji wako uliotukuka kwa ufuatilia na utumbuaji

Ukaongeza ukusanyaji wa kodi na mengine mengi tu mazuri yaliyowavutia wananchi wengi

Kuanzia nchini hadi nje ya nchi ulimwagiwa sifa

Mh. Rais watu wakawa wafuatiliaji wazuri wa luninga na vyombo vingine vya habari ili kujua nini leo raisi kafanya au kasema nini

Lakini mh. Raisi kadri siku zinavyokwenda hotuba zako zinaleta mtafaruku na changamoto mbalimbali nchini ukitofautiana na watendaji wako pamoja na serikali iliyopita sababu hotuba zako zinakuwa na maneno makali sana

Pia hotuba yako kwa mfano ile ya udsm ukipata fursa ya kuangalia upya hakika pointi zako zinajirudia rudia pia hakuna mtiririko mzuri maneno ni makali sana

Nadhani hata wazazi pamoja na vyuo vingine walijisikia vibaya sana

Sasa yaliyotokea baada ya hotuba yako ndio habari ya mjini kwa sasa watu wakasema kama mbwai na iwe mbwai

Mh.rais wewe ni mlezi wetu na wewe ni mwananchi namba moja unaewakilisha sample ya watanzania mil 45

Hii mh.rais inaweza kukushusha sana na pia inaweza kusababisha chuki baina ya wananchi au serikalini

Mh.rais jaribu kuandika hints zako wape wakuchapie alafu ipitie palipokosewa rekebisha

Mh.rais mimi sio mwandishi wa habari sijui kama nimepangilia pointi vizuri

Ni wako

Kilaza wa mwendokasi
 
Hahaaa eti kilaza wa mwendo kasi kusoma hata sio tatizo ni bure awe makini tu na kauli zake tatizo na yeye akiona makofi hasomi tena ile hotuba anaanza ku flow ya moyoni mwake. Makofi humpandisha midadi ukichangia na busara ya kuangalia mini cha kuongea na target ya hadhira
 
The graphics are pointing downwards in the secret but tremendous speed..the shortcomings are now seen clearly
 
Hahahaa yale makofi yanamdatisha anaanza kupandisha mzuka! Makofi yale awe makini maana mengine kumfanya amalize tu anakuwa off points ila kwa kuzuga wanapiga makofi ili apite kwenye hiyo pointi! Yeye haelewi anadhani wanamshangilia....basi anaanza kulipuka
 
Alazimishwe awe anasoma anakosea kutamka kwa usahihi majina, anakosea matamshi ya maneno mbalimbali , anakosea kutaja vyeo vya watu nk.

Alimuita Prof.Mgaya kuwa Mwenyekiti wa TCU badala ya katibu mtendaji wa TCU.
Hiyo TCU haina hata cheo cha mwenyekiti yeye akatamka Mara mbili kuwa prof. Mgaya ni mwenyekiti wa TCU.

Wasaidizi wa rais msaidieni mh.kwa kumwambia kuwa awe anasoma hotuba,anafanya makosa mengi sana anapohutubia bila kusoma.
 
hilo ndio tatizo hata mimi nililoliona...rais hataki kusoma hotuba aliyoandaliwa jukwaani matokeo yake anatoa kauli za kutatanisha bila kufikiri vizuri...
 
1. Maranyingi Nyerere pia alikuwa hasomi hotuba..kurudiarudia maanayake ni kutia msisitizo
2. Kutumia maneno makali ni sawa kabisa (pls msiturudishe kipindi cha "diplomasia").
3. Cha muhimu tu aache kutumia "self-contradicting statements" eg. Wanaovunja sheria za barabarani gari zao zikilala kituoni ziondolewe tyres (kitendo ambacho ni kinyume na sheria pia)..... unless kama hapo alikuwa anatania tu
 
tena awe anasoma neno kwa neno bila kuchomekea maneno yake mengine...hiii itasaidia sana kuondoa kauli za kukweza watu
 
Mheshimiwa Raid wetu mtukufu mm naona utendaji wako umeuelekeza zaidi baadhi ya mikoa kama dar es salam Na mikoa mingine mikubwa yenye majina na hata wizara pia kuna wizara nadhan huziangalii kabisa wakat ndo zilizojaa uchafu na ufisadi na uonevu wa kinyam na hakuna wa kututetea lkn naongelea mama kilango alikudanganya ukamtumtumtumbua vp na huyu mkuu wa mkoa wa lindi??miongoni mwa wilaya zake wilaya ya liwale hajatoa hata mfanyakazi hewa hata mmoja.????

Ni kweli??? Au anatetea ufisadi??? Hataendana na kasi yako kweli???tumbuaMheshimiwa Raid wetu mtukufu mm naona utendaji wako umeuelekeza zaidi baadhi ya mikoa kama dar es salam Na mikoa mingine mikubwa yenye majina na hata wizara pia kuna wizara nadhan huziangalii kabisa wakat ndo zilizojaa uchafu na ufisadi na uonevu wa kinyam na hakuna wa kututetea lkn naongelea mama kilango alikudanganya ukamtumtumtumbua vp na huyu mkuu wa mkoa wa lindi??miongoni mwa wilaya zake wilaya ya liwale hajatoa hata mfanyakazi hewa hata mmoja.????

Ni kweli??? Au anatetea ufisadi??? Hataendana na kasi yako kweli???tumbua.​
 

Attachments

  • IMG-20160601-WA0068.jpg
    49.6 KB · Views: 39
Shiremoor baba:$

Ningepeonda kuona unawareach watu wote wawe na complains au ushauri kwa kupitia mobile phone utapata yawider audience na kupata picha halisi ya walla hoi

Hata Jamie forums ni sehemu tu ya watu wote wa Tanzania,wengi bado Hawana computer facilities /Internet

January makamba alianzisha hii system sijjui ilifikia wapi?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…