Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hapo ndio patamu sasa, kama atakataa yote hayo elewa kuwa huyo rais siyo mtu wa kawaida, there's something wrong about him/her
 
Kama aliwekwa pale alipo kwa kura za wananchi na anatumia budget inayo tokana na kodi za wanachi basi ni halali kukosolewa pale anapo kosea lakin kama alijiweka mwenyewe na anatumia budget yake mwenyewe na pesa yake ya mfukoni kwakweli si busara na nidhambi kubwa sanan kumkosoa.
 
Jamani magufuli ana kosa gani mbona kila mtu anamsingizia magufuli kila kitu... magufuli mbona yupo fit jamani ila wananchi tunamuangusha, atumpi moyo. Rais yupo sawa jamani tumpe mkono tuachane na mambo ya siasa, siasa mda wake bado... tufanye kazi jamani tuache siasa. Siasa zitatupeleka pabaya
 
Itakuwa bado unajifunza kuanzisha threads, hongera umeweza japo hukujua unaandika nini! Tafakari tena ulichaandika!
 
JPM anawapeleka watanganyika pale dunia ilipo na inavyotaka lakini watanganyika wamekuwa wabishi aidha kwa kuto kujua siasa za dunia zimebadilka au kwa kuto kuamini kama huko wanakopelekwa ndio njia sahihi tunapistaili kwenda dunia ya sasa ni saisa ya utengano tumetoka kwenye ujamaa ,tukaenda kwenye ubepari sasa tupo kwenye utengeno kila nchi inajifungia milango ameanza US kesho utasikia Ulaya then dunia nzima hakuna tena anko joe wa kutoa misaada tena ni kufanya kazi na kujitegemea ndicho kitatuokoa na ndo kitu watanganyika amtaki
 
aisee
 
Itakuwa bado unajifunza kuanzisha threads, hongera umeweza japo hukujua unaandika nini! Tafakari tena ulichaandika!
Rudi shule kwanza ukajifunze kusoma na kuandika, naona unapalamia tu kuandika af ujui
 
Jf ni shule tosha, tatizo labda hujashiriki vya kutosha ktk mijadala!
Karibu, ni imani yangu utazoea tu!
 
Rudi shule kwanza ukajifunze kusoma na kuandika, naona unapalamia tu kuandika af ujui
Jf ni shule tosha, tatizo labda hujashiriki vya kutosha ktk mijadala!
Karibu, ni imani yangu utazoea tu!
 
Mheshimiwa Rais mimi binafsi na wengine walio wengi tumetambua juhudi zako za kupambana kupunguza gape kati ya walionacho na ambao hawana.
Nimeona jinsi unavyopambana na kujenga infrastructure nk.

Mbali na hayo yote nchi inakabiliwa na ukosefu wa ajira, hili limekuwa tatizo sugu sana, vijana wa kitanzania wanatapatapa hawajui wafanye nini maana private sector hawaajiri kwasababu ya hali mbaya ya biashara zao na Serikali nayo imesitisha ajira kwa mda usiojulikana.

Ombi langu kwako ni hili mheshimiwa:

Tusaidie kujenga irrigation scheme za kutosha hapa nchini ili sisi vijana tuweze kujiajiri kupitia kilimo ni dhahiri kwamba kukiwa na irrigation schemes za kutosha hakuna kijana anaejitambua atakaebaki kucheza pool badala ya kwenda kulima. Lkn tukisema tusubiri ajira za kupigwa na kiyoyozi tutasubiri sana. Nchi yetu imejaariwa ardhi kubwa na vyanzo vingi vya maji lkn imekosa watu makini wa kuvitumia ipasavyo vitu hivyo. Tunamshukuru Mungu tumepata Rais anaesikiliza vilio vya wanyonge. Mheshimiwa Rais JPM hiki nikilio chetu sisi vijana kwako. Hakika ukitujengea hizo irrigation schemes hatutakuangusha.

Njaa, umaskini na uzululaji tutakuwa tumevitokomeza kabisa endapo tutakuwa na kilimo cha umwagiliaji ktk maeneo mengi.

Kama ndani ya mda mfupi umeweza kununua ndege, kujenga hostel udsm, nyumba za askari, uwanja wa ndege chato nk. Najua na hili hutashindwa.

Sijui kama unapitia post za humu jf, lkn natumai kuna mtu wa karibu yako anaweza uona huu ujumbe na kukufikishia.

Ni hayo tu mheshimiwa.
Zaidi ya yote nakutakia afya njema na kazi njema pia
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…