Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Tatizo la Muhongo sio mwanasiasa, ila wakati wake alipiga kazi ya hatari, tena mie nitaenda mbali zaidi na kusema kama inawezekana na Masele arudi kuwa katibu mkuu wizara ya nishati.

Aliokoa vitalu vyetu vya gesi kutoka kwa madalali uchwara, anafaa...
 
Shikamooooo
 
Huo ushauri ukampe Mbowe akiunda baraza kivuli!!!
 
Hivi nyie mnaojaribu "ku mshauri " Mh Rais Magufuli ni nani Kati yenu nyie na Mh Magufuli anawafahamu vizuri hawa wabunge wa CCM ? Yeye kafanya nao Kazi kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali na Baraza la Mawaziri, katika kamati Mbalimbali za Bunge hivyo ana wajua vilivyo. Ninyi wengine mna chu kulia mambo ya kwenye mtandao kama vigezo vya uongozi bora. Mh Magufuli anaifahamu Serikali anayotaka kuunda ili imsaidie kuleta maendeleo aliyoajidi... Mwacheni ataunda Serikali makini. Siyo kila Adui yako lazima awe Adui wa wenzako....
 

umesahau shirika la reli ILA umeenda vizuri sana
 
Wazo zuri!!!,sema hawa watawala wetu huwa wanapangiwa nini cha kufanya ndo tatizo hapo mkuu.
 
Mtoa mada kama umekatika kichwa vile wewe unachuki binafisi na watu so ndo utashangaa na roho yako pindi lukuvi atakapo kuwa waziri mkuu
 
Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?

Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.
 
Mh. Rais, Dr. John Pombe Magufuli ningependa kuleta mawazo yangu hapa Jamii forum kama njia ya kukufikia wewe. Mh. Rais ni ukweli kwamba jiji la Dar es Salaam litaendelea kua kitovu cha ukuaji wa uchumi wetu na taifa kwa ujumla na ni ukweli usiopingika kwamba kama tunataka kukuza uchumi lazima tuangalie upya uwekezaji wa physical and economic infrastructure kwenye other major cities yenye potential kubwa ya kukuza uchumi wa taifa letu. Majiji kama Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma yanaitaji kuangaliwa upya ili yachangie kwa kasi ukuaji wa uchumi wa Taifa letu.

Kuna Athari za wazi kuacha kukuza hii miji ya kikanda, kwa kiasi kikubwa unemployment rate ni kubwa sana kwenye hii michi na fulsa za kiuchumi ni chache ukilinganisha na Dar es Salaam, Hii inapelekea vijana wengi wasomi na wasio wasomi kulundikana na kuendelea kua na mawazo yakwenda sehemu moja tu ya nchi kutafuta fulsa za kiuchumi.


Nimeshawishika baada ya kusoma speech ya Deputy Prime Minister Nick Clegghttps://www.gov.uk/government/speeches/deputy-prime-ministers-speech-on-economic-decentralisation-at-mansion-house na kuangalia mazingira ya taifa letu. Hatuwezi kukuza uchumi na kua na Taifa liliondelea na la mfano kama tunaendelea kuwekeza physical and economic infrastructure sehemu moja tu ya nchi, Dar es Salaam. Tunaitaji ?economic decentralization? ili kuchochea ukuwaji wa uchumi.


Mungu Ibariki Tanzania

Mungu Mbariki Raisi wetu Mpya.
 
Magari ya waliokuwa mawaziri yarudishwe yakiwa katika ubora wake, likirudishwa gari bovu waziri husika akatwe mafao yake litengenezwe!

Utashangaa hakuna gari lenye zaidi ya miaka miwili lakini wanataka mapya!
 
Kingine labda cha kuongezea ni asiwe kama vasco da gama! Ktk matrip
 
Sema ni nani anafaa ili kuendana na kasi ya HAPA KAZI TU
 
ndani ya ccm si rahisi kumpata kiongozi mzuri ndio maana mabadiliko maana yake ilikuwa kuitoa ccm madarakani lakini kwa hapa tulipofikia tutaumia tu,kwa miaka mingine mitano
Khaa!! Kweli bana labda aongee na Edo awe PM, Mbowe (Fedha), Sumaye (Spika) nafasi nyingine wajazwe kina Lissu, Sugu, Lema nk
😎
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…