Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Tatizo la Muhongo sio mwanasiasa, ila wakati wake alipiga kazi ya hatari, tena mie nitaenda mbali zaidi na kusema kama inawezekana na Masele arudi kuwa katibu mkuu wizara ya nishati.

Aliokoa vitalu vyetu vya gesi kutoka kwa madalali uchwara, anafaa...
 
Hali ya Kisiasa

1. Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili

2. Katiba mpya ya JMT ? pengine si ajenda ya chama chako kwa sasa lakini linahitaji dhamira yako ? chonde chonde litendee haki taifa hili



Mfumo na Uendeshaji wa Serikali

3. Uza mashangingi ya Serikali na ubakize machache tu kwa shughuli muhimu. Watumishi wa Serikali wakopeshwe magari na wapewe mafuta ili kuokoa fedha nyingi mno zinazopotea kiholela.

4. Rejesha nyumba za Serikali kwani wananchi wengi hatuna imani kuhusu dhamira, mantiki na umuhimu wa kuziuza nyumba za Serikali

5. Punguza sana idadi ya Wizara na Mawaziri ili kupunguza gharama

6. Boresha kipato cha Watumishi serikalini ili kuwaongezea morali

7. Toa fursa katika vipindi tofauti mikoani ukutane na wananchi wenye matatizo uwasikilize ana kwa ana, mmoja mmoja (uwe rais wa wananchi)

8. Misamaha ya kodi ni donda ndugu linalohujumu Taifa mapato, dhibiti hili kwa nguvu zako zote.

9. Panua wigo wa vyanzo vya mapato ya Serikali ? hili ni muhimu sana

10. Dhibiti safari za nje zisizo za lazima kwa Viongozi waandamizi wa Serikali


Rushwa na Ufisadi

11. Mahakama ya Rushwa na Ufisadi ianzishwe kama ulivyoahidi
12. TAKUKURU ipewe mamlaka ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila kibali cha DPP

Afya, Maji na Mazingira

13. Karabati hospitali za umma (Taifa, Mikoa, Wilaya) ziko katika hali mbaya (Zahanati kwa kila kijiji inawezekana!)
14. Imarisha Hospitali ya Muhimbili ikidhi viwango vya kimataifa ili kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi
15. Panua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili ijumuishe wananchi wote (Rwanda wameweza hili) watakaochangia kiwango nafuu
16. Miji na Majiji ni machafu mno (taka ngumu na maji taka), imeshindikana kubadili hali na inaelekea hakuna suluhisho, inabidi tuzoe uchafu ? tunaomba wahusika wageuke taka
17. Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto iboreshwe kwa nguvu zote
18. Serikal igharimie magonjwa hatarishi ikiwemo saratani na UKIMWI
19. Matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku (Rwanda, Zanzibar imewezekana)
20. Anzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yote

Elimu

21. Wanafuzi wengi wa elimu ya juu hawakupata mikopo kwa mwaka2015/2016? litatue hili kwani ni aibu
22. Elimu ya bure hadi kidato cha nne iwe kweli na yenye ubora
23. Shule ziimarishwe kwa kupatiwa madarasa, maabara, vitabu, walimu na lishe muafaka

24. ?One Computer, One Pupil? ? tujenge taifa la kisasa na linaloendana na mabadiliko ya nyakati kimaendeleo

25. Anzisha Kamisheni ya Taifa ya Ushauri kuhusu elimu

Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda

26. Fufua kilimo cha mazao asilia (mkonge, kahawa)
27. Anzisha Mfuko wa Taifa wa Kilimona Mifugo utakaotoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
28. Imarisha na jenga miradi ya umwagiliaji na majosho ya mifugo
29. Imarisha vyama vya ushirika na viwezeshe kujitafutia masoko
30. Futa kodi zote kandamizi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi
31. Anzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi
32. Weka kodi nafuu na shindani kuhamasisha wawekezaji


Miundombinu na Uchukuzi

33. Punguza gharama za vifaa vya ujenzi ili wananchi wengi wamudu kujenga nyumba bora
34. Fufua Shirika la Ndege la Taifa (ATC)
35. Imarisha miundombinu ili kuondosha misongamano katika majiji na miji mikubwa (Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha)
Shikamooooo
 
Hivi nyie mnaojaribu "ku mshauri " Mh Rais Magufuli ni nani Kati yenu nyie na Mh Magufuli anawafahamu vizuri hawa wabunge wa CCM ? Yeye kafanya nao Kazi kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali na Baraza la Mawaziri, katika kamati Mbalimbali za Bunge hivyo ana wajua vilivyo. Ninyi wengine mna chu kulia mambo ya kwenye mtandao kama vigezo vya uongozi bora. Mh Magufuli anaifahamu Serikali anayotaka kuunda ili imsaidie kuleta maendeleo aliyoajidi... Mwacheni ataunda Serikali makini. Siyo kila Adui yako lazima awe Adui wa wenzako....
 
[FONT=&quot] Hali ya Kisiasa [/FONT]

[FONT=&quot]1. [/FONT][FONT=&quot]Mgogoro wa Zanzibar ni jukumu lako kwa sasa halikwepeki. Tafuta wasuluhishi wawili (kutoka Bara na Visiwani) wakusaidie kulishughulikia hili[/FONT]

[FONT=&quot]2. [/FONT][FONT=&quot]Katiba mpya ya JMT ? pengine si ajenda ya chama chako kwa sasa lakini linahitaji dhamira yako ? chonde chonde litendee haki taifa hili [/FONT]

[FONT=&quot] [/FONT]

[FONT=&quot]Mfumo na Uendeshaji wa Serikali[/FONT]

[FONT=&quot]3. [/FONT][FONT=&quot]Uza mashangingi ya Serikali na ubakize machache tu kwa shughuli muhimu. Watumishi wa Serikali wakopeshwe magari na wapewe mafuta ili kuokoa fedha nyingi mno zinazopotea kiholela.[/FONT]

[FONT=&quot]4. [/FONT][FONT=&quot]Rejesha nyumba za Serikali kwani wananchi wengi hatuna imani kuhusu dhamira, mantiki na umuhimu wa kuziuza nyumba za Serikali[/FONT]

[FONT=&quot]5. [/FONT][FONT=&quot]Punguza sana idadi ya Wizara na Mawaziri ili kupunguza gharama[/FONT]

[FONT=&quot]6. [/FONT][FONT=&quot]Boresha kipato cha Watumishi serikalini ili kuwaongezea morali[/FONT]

[FONT=&quot]7. [/FONT][FONT=&quot]Toa fursa katika vipindi tofauti mikoani ukutane na wananchi wenye matatizo uwasikilize ana kwa ana, mmoja mmoja (uwe rais wa wananchi) [/FONT]

[FONT=&quot]8. [/FONT][FONT=&quot]Misamaha ya kodi ni donda ndugu linalohujumu Taifa mapato, dhibiti hili kwa nguvu zako zote.[/FONT]

[FONT=&quot]9. [/FONT][FONT=&quot]Panua wigo wa vyanzo vya mapato ya Serikali ? hili ni muhimu sana[/FONT]

[FONT=&quot]10. [/FONT][FONT=&quot]Dhibiti safari za nje zisizo za lazima kwa Viongozi waandamizi wa Serikali[/FONT]

[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]Rushwa na Ufisadi[/FONT]

[FONT=&quot]11. [/FONT][FONT=&quot]Mahakama ya Rushwa na Ufisadi ianzishwe kama ulivyoahidi[/FONT]
[FONT=&quot]12. [/FONT][FONT=&quot]TAKUKURU ipewe mamlaka ya kuwafikisha watuhumiwa mahakamani bila kibali cha DPP[/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]Afya, Maji na Mazingira[/FONT]

[FONT=&quot]13. [/FONT][FONT=&quot]Karabati hospitali za umma (Taifa, Mikoa, Wilaya) ziko katika hali mbaya (Zahanati kwa kila kijiji inawezekana!)[/FONT]
[FONT=&quot]14. [/FONT][FONT=&quot]Imarisha Hospitali ya Muhimbili ikidhi viwango vya kimataifa ili kupunguza gharama za matibabu nje ya nchi[/FONT]
[FONT=&quot]15. [/FONT][FONT=&quot]Panua wigo wa Mfuko wa Bima ya Afya ili ijumuishe wananchi wote (Rwanda wameweza hili) watakaochangia kiwango nafuu[/FONT]
[FONT=&quot]16. [/FONT][FONT=&quot]Miji na Majiji ni machafu mno (taka ngumu na maji taka), imeshindikana kubadili hali na inaelekea hakuna suluhisho, inabidi tuzoe uchafu ? tunaomba wahusika wageuke taka[/FONT]
[FONT=&quot]17. [/FONT][FONT=&quot]Huduma ya Afya ya Mama na Mtoto iboreshwe kwa nguvu zote[/FONT]
[FONT=&quot]18. [/FONT][FONT=&quot]Serikal igharimie magonjwa hatarishi ikiwemo saratani na UKIMWI[/FONT]
[FONT=&quot]19. [/FONT][FONT=&quot]Matumizi ya mifuko ya plastiki yapigwe marufuku (Rwanda, Zanzibar imewezekana)[/FONT]
[FONT=&quot]20. [/FONT][FONT=&quot]Anzisha Mfuko wa Maji Vijijini ili kuongeza kasi ya upatikanaji wa maji katika maeneo yote[/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]Elimu[/FONT]

[FONT=&quot]21. [/FONT][FONT=&quot]Wanafuzi wengi wa elimu ya juu hawakupata mikopo kwa mwaka2015/2016? litatue hili kwani ni aibu[/FONT]
[FONT=&quot]22. [/FONT][FONT=&quot]Elimu ya bure hadi kidato cha nne iwe kweli na yenye ubora[/FONT]
[FONT=&quot]23. [/FONT][FONT=&quot]Shule ziimarishwe kwa kupatiwa madarasa, maabara, vitabu, walimu na lishe muafaka[/FONT]

[FONT=&quot]24. [/FONT][FONT=&quot]?One Computer, One Pupil? ? tujenge taifa la kisasa na linaloendana na mabadiliko ya nyakati kimaendeleo[/FONT]

[FONT=&quot]25. [/FONT][FONT=&quot]Anzisha Kamisheni ya Taifa ya Ushauri kuhusu elimu [/FONT]
[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Viwanda[/FONT]

[FONT=&quot]26. [/FONT][FONT=&quot]Fufua kilimo cha mazao asilia (mkonge, kahawa)[/FONT]
[FONT=&quot]27. [/FONT][FONT=&quot]Anzisha Mfuko wa Taifa wa Kilimona Mifugo utakaotoa mikopo kwa wakulima, wafugaji na wavuvi[/FONT]
[FONT=&quot]28. [/FONT][FONT=&quot]Imarisha na jenga miradi ya umwagiliaji na majosho ya mifugo[/FONT]
[FONT=&quot]29. [/FONT][FONT=&quot]Imarisha vyama vya ushirika na viwezeshe kujitafutia masoko[/FONT]
[FONT=&quot]30. [/FONT][FONT=&quot]Futa kodi zote kandamizi kwa wakulima, wafugaji na wavuvi[/FONT]
[FONT=&quot]31. [/FONT][FONT=&quot]Anzisha viwanda vya kusindika mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi[/FONT]
[FONT=&quot]32. [/FONT][FONT=&quot]Weka kodi nafuu na shindani kuhamasisha wawekezaji[/FONT]

[FONT=&quot] [/FONT]
[FONT=&quot]Miundombinu na Uchukuzi[/FONT]

[FONT=&quot]33. [/FONT][FONT=&quot]Punguza gharama za vifaa vya ujenzi ili wananchi wengi wamudu kujenga nyumba bora[/FONT]
[FONT=&quot]34. [/FONT][FONT=&quot]Fufua Shirika la Ndege la Taifa (ATC)[/FONT]
[FONT=&quot]35. [/FONT][FONT=&quot]Imarisha miundombinu ili kuondosha misongamano katika majiji na miji mikubwa (Dar, Mwanza, Mbeya, Arusha)[/FONT]

umesahau shirika la reli ILA umeenda vizuri sana
 
Wazo zuri!!!,sema hawa watawala wetu huwa wanapangiwa nini cha kufanya ndo tatizo hapo mkuu.
 
Mtoa mada kama umekatika kichwa vile wewe unachuki binafisi na watu so ndo utashangaa na roho yako pindi lukuvi atakapo kuwa waziri mkuu
 
Ili kuipa hadhi na kuitangaza lugha yetu ya taifa, nashauri rais wetu mpya atumie Kiswahili katika shughuli zote rasmi za kitaifa na kimataifa. Cha msingi ni kuwa na wakalimani mahiri katika shughuli za kimataifa. Hii itainua hadhi na heshima ya nchi yetu badala ya kuendelea kuthamini lugha za kigeni. Tumekuwa watumwa mno wa lugha ya kiingereza mpaka kufikia hatua kudhani kuwa mtu anayeongea kiingereza vizuri ndiye aliye elimika wakati si kweli. Elimu ni uwezo siyo kuongea kiingereza. Hiki kiingereza cha "izi, wozi, wea, kongrugesheni, ameizingi, wati?, yu no, no problemu hakitusaidii kitu. Na kwa ujinga wetu tunafundishana kwa lugha tusiyoijua vizuri matokeo yake watoto wanafeli halafu tunawaona wajinga kumbe sera zetu ndio mbovu. Wachina, wakorea, wajerumani, wareno, wafaransa mbona wanatumia lugha zao na wanapiga hatua kubwa sana katika uchumi na sayansi. Sisi na kiingereza chetu cha kuombea maji tumefika wapi zaidi ya kutudhalilisha?

Maoni yangu haya hayana maana kuwa sitambui uwezo mkubwa wa kiingereza alio nao dr. Nataka aendeleze pale mwenzake alipoachia mwenzake, kwani alianza kwa kuhutubia kwa kiswahili kwenye mkutano wa AU lakini baadaye akaacha. Mimi nashauri Dr. sasa ajikite pamoja na mambo mengi kuitangaza lugha ya kiswahili kimataifa kwa yeye mwenyewe kuitumia badala ya kiingereza. Huwa naona viongozi wa nchi nyingine kama za kiarabu pamoja na kuwa wanajua kiingereza lakini utakuta wanazaunguza kiarabu na kisha wasiojua kutafsiriwa. Wakalimani sasa hivi tunao wengi, ni vizuri wakatumika vizuri kuikuza lugha yetu ya taifa. Ukweli ni kuwa unapotumia lugha mama au lugha ya taifa una kuwa na uhuru na uwezo mkubwa sana wa kujieleza na kuelezea kuliko unapotumia lugha za kigeni. Kwa watanzania wengi lugha yetu ya mama ni kiswahili.
 
Mh. Rais, Dr. John Pombe Magufuli ningependa kuleta mawazo yangu hapa Jamii forum kama njia ya kukufikia wewe. Mh. Rais ni ukweli kwamba jiji la Dar es Salaam litaendelea kua kitovu cha ukuaji wa uchumi wetu na taifa kwa ujumla na ni ukweli usiopingika kwamba kama tunataka kukuza uchumi lazima tuangalie upya uwekezaji wa physical and economic infrastructure kwenye other major cities yenye potential kubwa ya kukuza uchumi wa taifa letu. Majiji kama Mwanza, Arusha, Mbeya na Dodoma yanaitaji kuangaliwa upya ili yachangie kwa kasi ukuaji wa uchumi wa Taifa letu.

Kuna Athari za wazi kuacha kukuza hii miji ya kikanda, kwa kiasi kikubwa unemployment rate ni kubwa sana kwenye hii michi na fulsa za kiuchumi ni chache ukilinganisha na Dar es Salaam, Hii inapelekea vijana wengi wasomi na wasio wasomi kulundikana na kuendelea kua na mawazo yakwenda sehemu moja tu ya nchi kutafuta fulsa za kiuchumi.


Nimeshawishika baada ya kusoma speech ya Deputy Prime Minister Nick Clegghttps://www.gov.uk/government/speeches/deputy-prime-ministers-speech-on-economic-decentralisation-at-mansion-house na kuangalia mazingira ya taifa letu. Hatuwezi kukuza uchumi na kua na Taifa liliondelea na la mfano kama tunaendelea kuwekeza physical and economic infrastructure sehemu moja tu ya nchi, Dar es Salaam. Tunaitaji ?economic decentralization? ili kuchochea ukuwaji wa uchumi.


Mungu Ibariki Tanzania

Mungu Mbariki Raisi wetu Mpya.
 
Magari ya waliokuwa mawaziri yarudishwe yakiwa katika ubora wake, likirudishwa gari bovu waziri husika akatwe mafao yake litengenezwe!

Utashangaa hakuna gari lenye zaidi ya miaka miwili lakini wanataka mapya!
 
Kingine labda cha kuongezea ni asiwe kama vasco da gama! Ktk matrip
 
Pamoja na kwamba sina imani na chama chako, ila naomba unishawishi wewe binafsi katika serikali yako.
Kama ulivyojinaji kuwa serikali yako, yani Tanzania ya Magufuli itakuwa KAZI TU, basi naomba udhihirishe hivyo katika baraza lako la mawaziri.

Kabla hata sijataka kujua waziri mkuu ambaye ataendana na sura ya kauli mbiu yako, lakini nataka usituletee watu hawa ambao walikuwa mzigo kwa taifa na waliolifikisha nchi hapa ilipo chini ya aliyekutangulia pamoja na waziri mkuu wake.

1. Sopteter Muhongo.
Huyu pamoja na kwamba tunaambiwa hakuhusika moja kwa moja kwenye kashfa xa escrow lakini alikuwa kinara wa utetezi katika sakata hili. Pia ni miongoni mwa waziri wenye elimu kubwa lkn hakuwa na mkakati bunifu wa kutatua tatizo la umeme nchini zaidi ya kuiacha tanesco kwenye deni kubwa. Pia ni miongoni mwa viongozi ambao hawathamini wawekezaji wa ndani, anaamini nchi itajengwa na wazungu au wachina.

2. Lazaro Nyalandu.
Huyu ni miongoni mwa mawaziri ambao tumeshuhudia tembo wakiuliwa kwa wingi, na twiga wetu wakisafirishwa kwenda nje, hafai katika serikali yako, kwani atafanya kazi ya mazoeaa ya serikali ya awamu ya 4.

3. Mwigulu Nchemba.
Pamoja na kwamba hakukaa kwenye wizara ya fedha kwa mda mrefu, lkn ni miongoni mwa vijana ambao hawana adabu katika taifa hili. Ni mmoja wa wanasiasa wachanga ambao hajali matamshi yake mbele ya umma, haangalii baada ya hapa athari zake zitanipeleka wapi, sio mstaarabu.

4. Willium Lukuvi.
Huyu kwa mwendo wa kasi inayohitajika nchini hatufai, utendaji wake hauto tofautiana na wa awamu ya 4, hana jipya ndani ya serikali yako.

5. Shukuru Kawambwa
Huyu ni moja ya mawaziri walioshusha thamani ya elimu yetu. Sio mbunifu. Fedha za fidia za rada mpaka leo hatujui matumizi yake yalienda wapi, hatufai kabisaa.

6.Hawa Ghasia.
Huyu mama bado uchama umemkaa kichwani kuliko maslai ya taifa. Hayupo active katika utendaji wake.

7. Jumanne Maghembe.
Huyu ni moja ya mawaziri ambao ndio chanzo cha huduma mbovu za elimu na maji. Elimu yake ni kubwa lkn haina msaada kwetu.

8.Harrison Mwakyembe.
Huyu kinachompa sifa ni lile sakata la richmond ambalo tunamwona kama shujaa. Lakini kiukweli hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji. Sijaona mafanikio yake katika wizara alizozisimamia, ni mzigo ana asili ya mtandao ambao ni chanzo cha utendaji mbovu nchini. Ni mafya wa kisiasa

9. Magreth Sitta
Mama huyu tangu zama ni outdated, haendani na kasi ya dunia, yupo nyuma na mda, hafai katika serikali yako.

10. Sofia Simba
Hana tofauti na Mama sitta, tena huyu uchama na mtandao wa uongozi umemjaa kichwani, hafai katika serikali yako.

11. Andwer Chenge
Najua huyu unamfahamu vema

12. Anna Tibaijuka
Najua unamfahamu vizur

13. Willium Ngeleja
Najua wamfahamu vzr

NB.
1. Mheshimiwa Rais kuna vijana wengi ambao naamini katika utendaji wao lkn siamini kundi lake, na mmoja wao ni Januari Makamba. Huyu binafsi namwamini kiutendaji, ubunifu lakini kinachomsumbua ni kutaka madaraka makubwa, kundi lake lililo nyuma yake, Huyu badala ya kuchapa kazi atakuwa anawaza urais baada yako kustaafu. Kwa mtazamo wangu ungemweka kando kwa mda baada ya miaka miwili ndo uumpe majukumu.

2. Kwa kukusaidia mh Rais ni vema ukachagua mawaziri wachache ambao wengi wao hawakuwa mawaziri, sio viongozi katika chama, vijana, wenye elimu isiyo na shaka. Hawa ndio wataileta tanzania mpya ya HAPA KAZI TU.

Mh Rais ukikosea kwenye baraza la mawaziri basi jua umeuwa nchi, na hapo tutadhibitisha kuwa hakuna cha Magufuli 4 change itakuwa ccm ni ile ile.
Asantee.
Sema ni nani anafaa ili kuendana na kasi ya HAPA KAZI TU
 
ndani ya ccm si rahisi kumpata kiongozi mzuri ndio maana mabadiliko maana yake ilikuwa kuitoa ccm madarakani lakini kwa hapa tulipofikia tutaumia tu,kwa miaka mingine mitano
Khaa!! Kweli bana labda aongee na Edo awe PM, Mbowe (Fedha), Sumaye (Spika) nafasi nyingine wajazwe kina Lissu, Sugu, Lema nk
😎
 
Nimekumbuka kitu kuhusu Hawa Ghasia.

attachment.php
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom