Kama kichwa cha somo kinavyojipambanua hapo juu, kumekuwa na malalamishi,maoni,ushauri, Hoja,na mitazamo mbalimbali kuhusu uongozi wa mheshimiwa rais wa jamhuri yetu tukufu ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dr John Pombe Joseph Magufuli. Kwa nia njema ya kuleta maendeleo na kuangazia mambo yenye tija kwa watanzania walio wengi bila ya kujali hadhi zao! Makabila yao! Rangi zao na hata itikadi zao.....je ukipata nafasi ya kukutana na mheshimiwa rais utamwambia nini?
Kwa kuanza na Mimi mwenyewe nikikutana na mheshimiwa rais nitamshauri aanze kwanza na utekelezaji na utoaji wa Huduma za kijamii kama miundo mbinu ya mawasiliano, shule, Huduma za afya na elimu halafu ndio aje kwenye viwanda kwa sababu bila ya Huduma hizi kuwa sawa hatuwezi kuanzisha na hata kuendesha kiwanda! Pia nitamshauri asiimbe sana kwenye majukwaa kuhusu viwanda kwa sababu mataifa makubwa ukiyahubiria viwanda huwa hayapendelei sana....kwa hiyo kama inawezekana neno serikali ya viwanda lisitumike kabisa!
Note; huu ni mtazamo wangu na wewe unaweza kusema chochote cha kumshauri Mkulu kwa nia njema ya kujenga taifa la Tanzania.