Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Ningemshauri asikilize mahubiri ya Mwakasege kutoka katika kitabu cha Mithali 28:16.
 
Mkuu,kwamba yeye hapangiwi cha kufanya hukumkusikia,au unatafuta tu maneno ya kichochezi?,kwamba yeye no dereva wa roli asiye sikiliza kelele za aburia nalo hujalisikia!!.

Mambo ya kutupwa mabwepande au ununio siyataki.
Katumwa achokoze watu watqpike, halafu watekwe
 
KWA MHESHIMIWA RAISI

Mheshimiwa Rais pole kwa kazi, lakini naomba nichukue wakati wangu kuandika au kukueleza hiki ambacho sina uhakika kama kitakufikia au hakitakufikia. Lakini kwa imani na mapenzi ya taifa langu nitaandika pasipo kujali kama ujumbe huu utafika au haufiki ila naamini wapo watanzania watakaosoma.

Mheshimiwa umeingia madarakani ukiwa na vision ya mapinduzi ya viwanda, sawa ni nzuri sana ila tuangalie njia ya kupita. Vision ambayo nilikuwa natafuta ama nina ndoto ya kumsikia raisi atokee na kuisimamia.

Lakini katika kutimiza ndoto hii kuna namna ambayo naona tunaweza kuchemka nikirudi mbali na kupekua document mbalimbali, tunaona wazi kuwa nchi zote duniani ambazo zilifanya mapinduzi ya viwanda zilianza na kilimo.Bila kufanya mapinduzi ya kilimo Baba itakuwa ni ndoto ya mchana.

Angalia China, Marekani, Uingereza, Ubelgiji na kwingineko, walianza na mapinduzi ya kilimo. Nikitazama katika taifa la Tanzania kwanza naona ardhi ipo ya kutosha ila hakuna jitihada za dhati. Kwani tungeweza kwenda mbali kuliko ambavyo tumejaribu.

Kwanza ili viwanda viwepo ni lazima malighafi iwepo ya kutosha kisha kupata malighafi ya kutosha kwasababu viwanda vingi hutegemea mali ghafi basi sekta ya viwanda ingeweza kufanikiwa na endapo mali ghafi inatoka nchini basi hata uwezekano wa kuuza bdhaa zinazotokana na viwanda kwa bei rahisi ni rahisi mno,kwani malighafi hazifuuatwi kwa gharama kubwa.

Mheshimiwa raisi sababu nyingine ya kuweza kufanikiwa kiviwanda kupitia kilimo ni kwamba Uingereza, China na Marekani walipata faida kubwa kupitia kilimo baada ya kupata mazao mengi hivyo kuuza na kupelekea kupata mtaji ulioweza kuwafanya waanzishe viwanda na kuongeza uwekezaji katika kilimo. Mheshimiwa Magufuli hapa nchini tuna maeneo mengi makubwa lakini wananchi wanashindwa kuyatumia wakitegemea mvua na maeneo mengine mvua ni za kuungaunga.

Mheshimiwa raisi ukitaka kufanya nchi iendelee kiviwanda ni lazima tuhakikishe kwanza tunalima mwaka mzima na kilimo kinaleta tija ili kupata malighafi na kukuza uchumi ikiwemo hali za wananchi kwani wengi hutegemea kilimo.

Eneo la mikoa ya kati kama Dodoma, Singida na ya mikoa ya magharibi watu wanatakiwa kupata maji mwaka mzima kwani hawana mvua za kutosha lakini eneo hili lina rutuba ya kutosha. Mikoa mingine iliyobaki yapo maeneo yanayopata mvua za wasiwasi kama Tanga na mikoa mingine michache. Ukija mikoa ya nyanda za juu kusini hawa wamebarikiwa kupata mvua na siku mvua ikigoma mikoa hii nchi nzima itakumbwa na njaa. Mikoa kama Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe na Rukwa na hata Morogoro inalima mazao kwa wingi ila hutegemea mvua.

Lakini kama kutakuwa na mpango wa kupeleka maji taka kwa ajili ya kilimo vijijini basi nina uhakika maeneo mengi wananchi wangekuwa wanalima mwaka mzima na wangekuwa kiuchumi kwani maeneo haya watu hawalimi kama inavyotakiwa.

Ukitaka taifa watu wapige kazi basi waboreshee miundombinu. Kama hakuna mapinduzi ya kilimo,mapinduzi ya viwanda ni ndoto. Mataifa mengi yaliyoendelea kiviwanda yalianza kuboresha kilimo. Ukiweka miundombinu katika kilimo watu watapata soko hadi nje ya nchi na mwishowe watapata pesa za kuanzisha kuongeza uchumi kwa taifa.
Yako mengi ila leo naishia hapa.

NISAIDIE KUSHARE
 
Mradi wa maji toka l victoria yatasaidia irrigation. Hata maji toka ardhi ni ni muhimu.pawepo na maeneo maalum kwa kuanzi
 
uko sawa. ila tukumbuke hili alilisema sana ktk uchaguzi. Ukiangalia maeneo mazuri ya kilimo yalishikiliwa na watangulizi wake wenye tamaa. kinachofanyika sasa ni kuyagawa upya. Kisha tuone tunaendaje. pamba itiliwe mkazo mno. viwanda vya ngozi si shida tene Ppf wapo. ila kule kwenye ufugaji wa kienyeji mm nashauri wagawiwe vitaru ikiwezekana visima vichimbwe wawe wanamwagilia nyasi na ngombe waepuke mwendo mrefu wa malisho kwani unaleta mmomonyoko. kando kando ya mito visima vichimbwe kitaalamu na tusiruhusu aji yanayo tiririka toka mtoni kutumika ktkt umwagiliaji. REA wakazane kupeleka umeme kila mahali na wasubiri tu kuitwa na neno NATAKA UMEME hapa.
 
Industrial Revolution is nothing without Agrarian revolution. Discuss

Agrarian Revolution is the backbone of Industrial revolution. Discuss with vivid examples from Tanzania.

MKUU NADHANI HOJA YAKO IMEFIKA NA ITAFANYIWA KAZI
 
Kama kichwa cha somo kinavyojipambanua hapo juu, kumekuwa na malalamishi,maoni,ushauri, Hoja,na mitazamo mbalimbali kuhusu uongozi wa mheshimiwa rais wa jamhuri yetu tukufu ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dr John Pombe Joseph Magufuli. Kwa nia njema ya kuleta maendeleo na kuangazia mambo yenye tija kwa watanzania walio wengi bila ya kujali hadhi zao! Makabila yao! Rangi zao na hata itikadi zao.....je ukipata nafasi ya kukutana na mheshimiwa rais utamwambia nini?

Kwa kuanza na Mimi mwenyewe nikikutana na mheshimiwa rais nitamshauri aanze kwanza na utekelezaji na utoaji wa Huduma za kijamii kama miundo mbinu ya mawasiliano, shule, Huduma za afya na elimu halafu ndio aje kwenye viwanda kwa sababu bila ya Huduma hizi kuwa sawa hatuwezi kuanzisha na hata kuendesha kiwanda! Pia nitamshauri asiimbe sana kwenye majukwaa kuhusu viwanda kwa sababu mataifa makubwa ukiyahubiria viwanda huwa hayapendelei sana....kwa hiyo kama inawezekana neno serikali ya viwanda lisitumike kabisa!
Note; huu ni mtazamo wangu na wewe unaweza kusema chochote cha kumshauri Mkulu kwa nia njema ya kujenga taifa la Tanzania.
 
Mie nitamwambia uchaguzi alioushinda, wanananchi hawakuwa wakipiga kura kuchagua mtu mwenye akili kuliko Watanzania wengine wote, ulikuwa wa Watanzania wenye akili timamu kuchagua raisi wao wa kuwaongoza, sio kuwaendesha kama mizigo kwenye lori lake.

Kisha nitamwambia kama una masikio nisikie, na kuaga.
 
Kama kichwa cha somo kinavyojipambanua hapo juu, kumekuwa na malalamishi,maoni,ushauri, Hoja,na mitazamo mbalimbali kuhusu uongozi wa mheshimiwa rais wa jamhuri yetu tukufu ya muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dr John Pombe Joseph Magufuli. Kwa nia njema ya kuleta maendeleo na kuangazia mambo yenye tija kwa watanzania walio wengi bila ya kujali hadhi zao! Makabila yao! Rangi zao na hata itikadi zao.....je ukipata nafasi ya kukutana na mheshimiwa rais utamwambia nini?

Kwa kuanza na Mimi mwenyewe nikikutana na mheshimiwa rais nitamshauri aanze kwanza na utekelezaji na utoaji wa Huduma za kijamii kama miundo mbinu ya mawasiliano, shule, Huduma za afya na elimu halafu ndio aje kwenye viwanda kwa sababu bila ya Huduma hizi kuwa sawa hatuwezi kuanzisha na hata kuendesha kiwanda! Pia nitamshauri asiimbe sana kwenye majukwaa kuhusu viwanda kwa sababu mataifa makubwa ukiyahubiria viwanda huwa hayapendelei sana....kwa hiyo kama inawezekana neno serikali ya viwanda lisitumike kabisa!
Note; huu ni mtazamo wangu na wewe unaweza kusema chochote cha kumshauri Mkulu kwa nia njema ya kujenga taifa la Tanzania.

Hataki ushauri mie nitamwambia aue wapinzani wote wanaompinga ili abaki peke yake na wale anaowapenda
 
Hii mada ni aina flani ya uchochezi kati ya JF na dola!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom