SERIKALI HAINA DINI
Post sent using JamiiForums mobile app
MUDA UTAONGEA...Watu walioenda shule kuiacha siasa kwa wasioenda shule ndio imekuwa tatizo,wenye elimu watakwambia mimi na siasa tofauti ndio maana mabashite wanatuongoza kwasababu wao wameingia kwenye siasa na kuwa viongozi.na mtu yoyote hawezi kujitenga na siasa kwasababu siasa ndio inatupangia maisha iwe unataka au hutaki siasa itaathiri maisha yako kwa namna moja au nyingine.
Makosa!Yehovah Mungu Baba aliye yote na juu
Kwa akili za kawaida tu ni kwamba huyu jamaa hana dini bali anatumia mwavuli wa dini.
Pili upinzani wa sasahivi siuelewi kabisa, I think Jamaa wa chato ni mchawi balaa, I mean katuroga wote. Maaskofu wamenywea, Mashehe wameshazibwa midomo, wafanyakazi na vyama vyao chali, Upinzani ndo tayari kabisa. Yamebaki matamko, leo tamko hili kesho lile. Mara fulani kawekwa ndani, Mara fulani anahojiwa.
Tunapoelekea MAGU atateua mpaka wenyeviti wa vyama siasa na wafanyakazi na hakuna atakayefungua domo.
Hahahaaaaaaa!! Kwakweli kwangu mimi madhaifu niliyo yaona kwake ni hayo tuu na naona akiyarekenisha hayo tuuuu !! Mimi nitapambana vikali na watakao msema vibayaHayo 6 huwezi yapata toka kwa JPM!Unatafuta mvua jangwani ndugu!
Kuna mambo yupo sahihi na ukweli bila unafiki nakubaliana naue kabisa lakin kuna mengi ana enda kinyume nyume akirekebisha atakuwa rais bora kwangu 100%
1. Akubali kukosolewa na kukosoleka
2. Aamini kuwa yeye ni kiongozi na sio mtawala
3. Awe na lugha na matendo yanayo waunganisha watanzania bila kujali vyama,imani na makabila yao.
4.apuunguze chuki za wazi hasa kwa makundi anayo dhani hayamuungi mkono na aondoe upendo wa wazi kwa makundi anayo dhani yanamuunga mkono
5. Awe na roho ya kujali makundi yote na kuona kila kundi lina umuhimu kwa taifa mf. Wahanga,watumishi,wakulima,wafugaji,watoto,vijana , wanawake,walemavu, wazee na makundi mengine yooote
6.asimuone kiongozi fulani ni muhimu kuliko wengine ,woote wawe sawa mbele zake wakikosea waonywe wote na wakiweza wasifiwe wote kwa usawa.
Hayo 6 tu kwangu mimi ndio yanayo nifanya niwe nae kwa 50%
Nasisitiza kwangu mimi sijamsemea yeyote ila unaruhusiwa kuniunga mkono na kunipinga pinga pia
Mkuu nipe ruhusa niliongeze hili kwenye uzi ni muhimu sana sana asante kunikumbusha hasa hilo (i)Mimi langu namba 7 (lenye vipengele viwili) kuongezea hayo uliyosema ni kama ifuatavyo:
(i) Aendeleze mchakato wa katiba ya Warioba na kutupilia mbali ile iliyoitwa "pendekezwa" baada ya kuchakachuliwa na chama chake cha CCM.
(ii) Muendelezo wa katiba ya Warioba uhakikishe kipengele cha tume huru ya uchaguzi hakichakachuliwi na pia Wabunge wapewe haki ya kuendelea na ubunge wao hata kama watafukuzwa vyama vyao. Kwa maana nyingine, wabunge wawe huru, ili hatimaye tuwe na bunge lenye meno na sio hili kibogoyo la sasa lililojaa wagonga meza waoga. Hapo Magu atakuwa wangu 90% (kuna mengine sijasema ndio maana natoa 90%).
Mkuu nipe ruhusa niliongeze hili kwenye uzi ni muhimu sana sana asante kunikumbusha hasa hilo (i)