Ningekuwa Rais Magufuli, Ninge.......
Kwanza kabisa, ningehakikisha wafanyakazi wote wanaoacha kazi wenyewe (resignation), na wanaofukuzwa kazi, wanapewa fedha zao au FAO LA KUJITOA toka mifuko ya jamii bila ukiritimba na mizengwe yoyote. Hii ingesaidia sana kujiimarisha kisiasa, kwa sababu waathirika wa hizi fedha zilizozuiwa na hii mifuko ya jamii bila maelezo yanayoingia kwenye bongo, wengi ni vijana. Kadhalika uchumi ungepaa sana kwa sababu vijana wengi wangefanya kilimo na biashara, tofauti na sasa ambapo kijana akifukuzwa kazi, hana pa kuanzia kutokana na kutokuwa na kianzio (capital) kwa ajili ya biashara na kilimo.
Pili, ningemteua Tundu Antiphas Lissu awe Waziri wa sheria, au attorney general. Hii ingesaidia sana katika masuala yote ya kisheria, nina hakika serikali ingeshinda kesi zake kirahisi inazoshitaki au kushitakiwa.
Tatu, ningeruhusu mikutano ya kisiasa kwa sababu naamini siasa ni kazi na ndiyo maana vyuoni kuna kozi za kisiasa.
Nne, ningehakikisha kila Mtanzania anapata bima ya afya, kwa sababu maendeleo ya taifa lolote duniani, iwe kielimu, kuchumi, na hata kiteknolojia yanategemea afya imara ya watu wake.