Awali ya yote niungane na wote wanaomuombea kamanda Lissu Mungu ampe afya na apone haraka na kurudi kwenye uwanja wa mapambano. Kwa mara ya kwanza, mara nilipopata taarifa hizi, nilikuwa na wanangu wawili, niliwataka tumwombee Lissu, na mwanangu mmoja aliongoza sala hiyo. Sijawahi kufanya kitu kama hicho kwa kweli, ila kwa Tundu Lissu, niliona kuna haja ya kufanya hivyo, na hata Zaidi.
Sasa tuje kwenye mada. Rais wetu, JP Magufuli, pamoja na nia nzuri aliyo nayo ya kuondoa maovu katika nchi hii na kuiwezesha kufaidi rasilimali zake, kuna huu utaratibu wa kutumia nguvu nyingi, kuwabana wengine wasifanye siasa abaki peke yake, kuendesha utawala ambao yeye mwenyewe aliwahi kukiri kwamba anapenda "kutumia rungu". aliyasema haya alipokuwa akiongea mbele ya Rais wa Zambia, ambaye ana jina la "Lungu". alimwomba wabadilishane jina, ampe jina lake la "Pombe" kwa sababu yeye Magufuli hapendi na hatumii Pombe, lakini achukue jina la "Lungu" kwa sababu yeye Magufuli anapenda "kutumia rungu".
Huu utaratibu wa kuongoza nchi namna hii, unafanya upinzani uchukue hatua za kiharakati Zaidi, na ndio maana akina Tundu Lissu wamejitokeza sana. uwanja wa siasa umefungwa, na kwa hiyo kumbi za mahakama na vituo vya Polisi ndio vimegeuzwa kuwa viwanja vya siasa. siyo kwa kupenda, lakini kwa sababu "Nature Abhorrs vacuum". Siyo lazima nchi iwe katika hali ya taharuki namna hii. kwa kuwa "antagonize" wapinzani, yamejengwa mazingira ambapo sasa hivi siasa za vyama vingi ni uadui, badala ya kuwa ni utani, na kusaidiana kujenga nchi. inafikia hatua mpaka tukio kama hili la kupigwa risasi Tundu Lissu, inakuwa vigumu kuamini kwamba serikali haihusiki, kutokana na aina ya mahusiano yaliyopo baina ya upinzani na serikali na CCM yake.
Hata katika maisha ya kawaida, kama mtu anashambuliwa na risasi namna hii, watuhumiwa wa kwanza Polisi inaoanza nao ni wale ambao ni "maadui" za huyu mhanga. wote waliowahi kutoa kauli za vitisho kwake, wanakuwa watuhumiwa. hiyo ni kadiri ya utaratibu wa kawaida kabisa wa kipolisi. na inaleta ukakasi kusikia vyombo vya dola, viongozi wa serikali, pamoja na Rais mwenyewe, spika Ndugai na wengine kama hao, wakitoa kauli za "pole" na kulaani tukio. wanaonekana kama wanafanya kejeli tu. kauli kama hizi zinatakiwa ziungwe mkono na aina ya mahusiano ya kila siku yaliyopo kati ya serikali na upinzani. ndio maana napendekeza kwa dhati kabisa, Rais Magufuli ajitafakari. CCM ijitafakari. namna nyingine itabidi serikali ifanye jitihada kubwa kumlinda Tundu Lissu, maana akipata tatizo lolote, itakuwa vigumu sana kwa serikali kukwepa lawama