Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Good Thinking Running a Government it is Not Like Family Matters others say a Country is Not a Company 'Hao Ma Dr/Prof Wengi wana jitoa Ufahamu" They Would Like to Treat Every body Like Their Student 'Hatuko Shule Tuna hitaji Maendeleo'We need Welfare Type of Economy 'Uchumi unao ongeza kipato kwa kila Mwananchi na Siyo Maendeleo ya vitu' peke yakeWatanzania wengi tunataka Magufuli afanikiwe. Lakini kuwa Raisi sio kazi ndogo kwasababu kuna watu wanakushauri kwa manufaa binafsi ya kichama, kuan watu wanataka kupata nguvu kupitia migongo yako, na kuna viongozi ambao wanafikiria wanajua kila kitu. Tatizo kubwa sana la Magufuli na uongozi wa sasa inaonekana hawana plan. Hawana plan ni kwasababu wanajaribu kuendesha nchi kwa jinsi wanavyofikiria wakati huo na kibaya zaidi ukifanya hivyo mara nyingi nchi itakushinda kwasababu kuna kelele nyingi sana.
Hivyo kuna wanaosema hatushauri sasa mimi najua Magufuli anatakiwa kuanzia wapi na matatizo yako ni yapi. Na ni nini kitafanya maendeleo ya nchi yaanze kuonekana na furaha kwa nchi. Kwasasa hakuna anayefurahia chochote Tanzania. Nitaandika vitu hatua moja moja kuwasaidia
1. Ajiri team ya pricewaterhousecooper ikishirikiana na Mhasibu mkuu wa nchi kufanya yafuatayo
a. Kuchunguza utendaji wa idara zote za serikali na utendaji wake
b. Kutoa report ya kuongeza ufanisi kwenye kila idara hasa kwenye kuweka technologia, kupunguza wafanyakazi wasio wa lazima, kuunganisha idara zinazofanya kazi moja n.k…
c. Kuweka hatuna za kuchukua za utekelezaji wa hiyo plan bila kujali faida za kisiasa
Hii step ya kwanza itasaidia kujua tuko wapi, idara ambazo si za lazima na kutakuwa na plan ya utekelezaji.Utaratibu wa sasa wa viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi hautasaidia maana wengine hawana ujuzi lakini vilevile wengine hasa viongozi kuwa na budget kubwa ni faidia kwao hivyo hawawezi wenyewe kupunguza matumizi ya ofisi zao maan itakuwa ni kujipunguzia power zao kitu ambacho ni kigumu. Hii inatakiwa kufanya na sharia lisilo na siasa wala agenda nyingine ya siri.
2. Achane ya vyombo vya habari. Waache watu waongee lolote , chochote kile na serikali iwekeze kwenye kukuza uchumi tu. Uchumi ukikuwa watu wanafurahia hautahitaji polisi wala uhasama. Na kikubwa hii vita huwezi kushinda
3. Ruhusu vyama vya siasa kuwa free na kufanya mikutano. Uhasama wa sasa hausaidii nchi na vievile ujue kwamba skendo kubwa za rushwa zimeletwa na upinzani. Ukiwa na wale wanaokuita mzee kila wakati huta kaa ujue ukweli . Lakini kikubwa corruption itaongezeka badala ya kupungua. Watakaonufaika sio TZ wala wewe ni viongozi binafsi wa CCM. Be careful kwenye hili utaka nchi ifanikiwe au CCM… ni vitu tofauti hivyo.
4. Fanya mpango wa uangalizi upya wa kodi. Kodi zetu sio zote nzuri na nyingi ziko juu sana na kupunguza uwekezaji. Kodi ziwe zina stimulate maendeleo
5. Fanya kufungua biashara iwe rahisi. Tuachane na milolongo ya kufungua biashara hakuna sababu maana wafanyabiashara ni walipa kodi.
6. Bank: Serikali isikope kutoka bank za ndani hii itapunguza riba za bank
7. Kila Mtanzania awe na kitambulisho na vitumike kila mahali hii itasadia sehemu nyingi sana. Vilevile kuwe na address za nyumba wanazoishi kwenye vitambulisho.
8. Ajiri watu wenye uzoefu sio wasomi wasio na uzoefu mfano hakuna wafanyabiashara kwenye baraza lako na wengi wa Dr, Prof hawajui chochote kuhusu utendaji wa kazi. Research za kishue hazisaidii sana kwenye utendaji.
9. Unda team maalumu za mapendekezo ya mabadiliko ya mifumo kama Afya, Elimu, Land, Kilimo….. mifumo ya sasa imepitwa na wakati sana. Unda team ambayo tena… ina watu wenye uzoefu wa hizo sehemu sio wasomi wasio na uzoefu na ziweke utendaji na plan zote.
10. Sikiliza ushauri sio kutoka kwa wana siasa pekee bali wapinzani, wafanyabiashara, wanafunzi, NGO’s na wengine wengi
11. Achana na vyombo vya sheria . acha view huru sasa tunaona mahaka ya rushwa inachagua makossa, kuna video za rushwa lakini hakuna washitakiwa! Polisi kwenye siasa achana na haya itaweka future mbaya ni si ya lazima.
Kikubwa Magufuli angalia sana sera zako. Ili Tanzania iende mbele haihitaji wewe kuwa na nguvu zaidi bali wewe kuwa na nguvu pungufu. Maana kesho na kesho kutwa akija mwingine na ana power zote uliyofanya yote anaweza kufuta kwa mwaka mmoja tu. Hivyo kama unapenda TZ ni lazima upende demokrasia kwa manufaa ya nchi nzima sio binafsi maana hata wewe una muda tu utaondoka
Yanaingia huku yanatokea hapa..ha ha! eti price cooper water house hata anawajua? hata delloitte yenyewe sidhani..!Mnashauri mburulaaaa!!
Akiutuma atakamatwa kwa uchochezi.Natamani mkuu auone huu ushauri moja kwa moja. Mtumie kwenye twitter yake mkuu
Nisaidie siko kwenye twitter kwa sasaNatamani mkuu auone huu ushauri moja kwa moja. Mtumie kwenye twitter yake mkuu