Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hivi we jamaa kama dawa zako zimeisha si useme tu tukununulie...
 
Watanzania wengi tunataka Magufuli afanikiwe. Lakini kuwa Raisi sio kazi ndogo kwasababu kuna watu wanakushauri kwa manufaa binafsi ya kichama, kuan watu wanataka kupata nguvu kupitia migongo yako, na kuna viongozi ambao wanafikiria wanajua kila kitu. Tatizo kubwa sana la Magufuli na uongozi wa sasa inaonekana hawana plan. Hawana plan ni kwasababu wanajaribu kuendesha nchi kwa jinsi wanavyofikiria wakati huo na kibaya zaidi ukifanya hivyo mara nyingi nchi itakushinda kwasababu kuna kelele nyingi sana.

Hivyo kuna wanaosema hatushauri sasa mimi najua Magufuli anatakiwa kuanzia wapi na matatizo yako ni yapi. Na ni nini kitafanya maendeleo ya nchi yaanze kuonekana na furaha kwa nchi. Kwasasa hakuna anayefurahia chochote Tanzania. Nitaandika vitu hatua moja moja kuwasaidia


1. Ajiri team ya pricewaterhousecooper ikishirikiana na Mhasibu mkuu wa nchi kufanya yafuatayo

a. Kuchunguza utendaji wa idara zote za serikali na utendaji wake

b. Kutoa report ya kuongeza ufanisi kwenye kila idara hasa kwenye kuweka technologia, kupunguza wafanyakazi wasio wa lazima, kuunganisha idara zinazofanya kazi moja n.k…

c. Kuweka hatuna za kuchukua za utekelezaji wa hiyo plan bila kujali faida za kisiasa

Hii step ya kwanza itasaidia kujua tuko wapi, idara ambazo si za lazima na kutakuwa na plan ya utekelezaji.Utaratibu wa sasa wa viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi hautasaidia maana wengine hawana ujuzi lakini vilevile wengine hasa viongozi kuwa na budget kubwa ni faidia kwao hivyo hawawezi wenyewe kupunguza matumizi ya ofisi zao maan itakuwa ni kujipunguzia power zao kitu ambacho ni kigumu. Hii inatakiwa kufanya na sharia lisilo na siasa wala agenda nyingine ya siri.

2. Achane ya vyombo vya habari. Waache watu waongee lolote , chochote kile na serikali iwekeze kwenye kukuza uchumi tu. Uchumi ukikuwa watu wanafurahia hautahitaji polisi wala uhasama. Na kikubwa hii vita huwezi kushinda

3. Ruhusu vyama vya siasa kuwa free na kufanya mikutano. Uhasama wa sasa hausaidii nchi na vievile ujue kwamba skendo kubwa za rushwa zimeletwa na upinzani. Ukiwa na wale wanaokuita mzee kila wakati huta kaa ujue ukweli . Lakini kikubwa corruption itaongezeka badala ya kupungua. Watakaonufaika sio TZ wala wewe ni viongozi binafsi wa CCM. Be careful kwenye hili utaka nchi ifanikiwe au CCM… ni vitu tofauti hivyo.

4. Fanya mpango wa uangalizi upya wa kodi. Kodi zetu sio zote nzuri na nyingi ziko juu sana na kupunguza uwekezaji. Kodi ziwe zina stimulate maendeleo

5. Fanya kufungua biashara iwe rahisi. Tuachane na milolongo ya kufungua biashara hakuna sababu maana wafanyabiashara ni walipa kodi.

6. Bank: Serikali isikope kutoka bank za ndani hii itapunguza riba za bank

7. Kila Mtanzania awe na kitambulisho na vitumike kila mahali hii itasadia sehemu nyingi sana. Vilevile kuwe na address za nyumba wanazoishi kwenye vitambulisho.

8. Ajiri watu wenye uzoefu sio wasomi wasio na uzoefu mfano hakuna wafanyabiashara kwenye baraza lako na wengi wa Dr, Prof hawajui chochote kuhusu utendaji wa kazi. Research za kishue hazisaidii sana kwenye utendaji.

9. Unda team maalumu za mapendekezo ya mabadiliko ya mifumo kama Afya, Elimu, Land, Kilimo….. mifumo ya sasa imepitwa na wakati sana. Unda team ambayo tena… ina watu wenye uzoefu wa hizo sehemu sio wasomi wasio na uzoefu na ziweke utendaji na plan zote.

10. Sikiliza ushauri sio kutoka kwa wana siasa pekee bali wapinzani, wafanyabiashara, wanafunzi, NGO’s na wengine wengi

11. Achana na vyombo vya sheria . acha view huru sasa tunaona mahaka ya rushwa inachagua makossa, kuna video za rushwa lakini hakuna washitakiwa! Polisi kwenye siasa achana na haya itaweka future mbaya ni si ya lazima.


Kikubwa Magufuli angalia sana sera zako. Ili Tanzania iende mbele haihitaji wewe kuwa na nguvu zaidi bali wewe kuwa na nguvu pungufu. Maana kesho na kesho kutwa akija mwingine na ana power zote uliyofanya yote anaweza kufuta kwa mwaka mmoja tu. Hivyo kama unapenda TZ ni lazima upende demokrasia kwa manufaa ya nchi nzima sio binafsi maana hata wewe una muda tu utaondoka
 
Good Thinking Running a Government it is Not Like Family Matters others say a Country is Not a Company 'Hao Ma Dr/Prof Wengi wana jitoa Ufahamu" They Would Like to Treat Every body Like Their Student 'Hatuko Shule Tuna hitaji Maendeleo'We need Welfare Type of Economy 'Uchumi unao ongeza kipato kwa kila Mwananchi na Siyo Maendeleo ya vitu' peke yake
 
Hiki Chama Cha Mapinduzi ni Chama kwanza Taifa baadaye,haauwapigie zeze hawatakusikiliza
 
Natamani mkuu auone huu ushauri moja kwa moja. Mtumie kwenye twitter yake mkuu
 
habari wa wakubwa huku leo niliamua kuulizia kuhusu bima za afya nilichokutana nacho kweli hizi Bima kama za Matajiri nimepita hapa AAR dah bima kwa mwaka 1.6 M hao NHIF ndio ghali sasa hizi Bima mbona mwananchi wa kawaida hatuzimudu Serekali ina ibidi iingalie upya Raisi wa Nyonge angalia hili
 
Wakuu nimekaa nikitafakari kauli ya Mh Rais juzi kwa katibu wa itikadi na uenezi wa CCM Ndugu H. Polepole..
kama Mtanzania ambae ninaamini katiba inaniruhusu kutoa maoni yangu mradi sivunji sheria.
naomba kusema kauli ile imenijeruhi mno..! Naamini kuna wengine pia waliojeruhiwa..!
Ninazo sabbu kadhaa za kusema haya.

1: Endapo Mh, Rais kaamua kusafisha Nchi hii miaka kumi kwa waovu kusubiri aondoke kisha waendelee na uovu wao.! Sio mingi ni kiasi tu cha wao kujipanga wakiwa na matumaini tele ya kumuandaa mrithi wanaejua ataendana na matakwa yao.

2: Katika ukanda huu wa Afrika mashariki na kati Tanzania pekee ndio Nchi iliyokuwa inachekwa na kuwa kituko. Tuna kila aina ya raslimali ambazo zingeweza kuifanya Tanzania kuwa Nchi bora lakini tulikosa kiongozi mwenye uchungu na uzalendo halisi.wa kusimamia maamuzi yake.!!

Kama alivyo wahi sema baba wa Taifa ili Nchi iendelee inahitaji. WATU, ARDHI, SIASA SAFI, NA UONGOZI BORA..
ninaamini hivyo vingine halikuwa tatizo isipokuwa tulikosa uongozi bora japo tulikuwa na viongozi..!

Wakati ambapo tunaanza kuona Nuru ya uongozi bora..... Daaah[emoji21]

Yapo mengi lakinj mwisho niseme
Nchi hii ina kundi la watu ambao wapo ili waone mabaya tu kwa Taifa hili nq hawa ni wengi sana.
nirudie kusema tuna watu ambao kila kukicha huwa hawaoni jema lolote kwenye macho yao zaidi ya matumbo yao na hiki ni kizazi kilichotamalaki toka kwenye timu zetu za mpira wa miguu mpaka sehemu nyingine za michezo na siasa.
hebu Angalia yanayoendelea Simba na Yanga. Ni klabu kongwe Afrika mashariki kinachondelea kwenye hizo klabu ni uozo mtupu.
Angali TFF na Taifa stars.!
Alikuja Maximo akaonesha uelekeo walipoona tunafanikiwa wakatengeneza fitna kwenye vyombo vya habari mpaka akafukuzwa waulize leo hao waliotengeneza fitna Taifa stars ya Maximo iko wapi.
hawana majibu..!![emoji22][emoji22]

Mh, Rais nakumbuka uliwahi sema pale bandarini
"kuwa Rais Nchi hii ni Mateso makubwa"!!
kauli ile bado inazunguka kwenye akili yangu kila nikiona kejeli za kwenye mitandao juu ya utendaji wako kauli hiyo inajirudia tena na tena.najiuliza nani mwenye moyo wa chuma awezaye beba kejeli hizo? Akavumilia..?

Mh, Rais naomba nitabiri haya japo si mtabiri yamkini ukiondoka baada ya msimu wako kuisha tutarudi kulekule tulikotoka.. tumeonja dalili za mafanikio.
tumeona kule walikokuwa Rwanda. Na walipo sasa kwa uongozi wa Mh paul kagame.
tumeona walikokuwa Uganda na walipo sasa kwa uongozi wa Museveni..
wananch wa Nchi hizo sio wajinga wanafahamu thamani ya viongozi wao.!

Mh, Rais tuache tutoe yaliyo moyoni Mwetu.!
Tusije tukakufuru na kumkosea Muumba wetu..!

Ndimi Mtanzania Mzalendo.
getrusa.
 
Wakuondolewa ni CCM kama ulivyoianika mwenyewe maana ndio iloyotufikisha hapa tulipo. Rais anahitajika kuijenga taasisi ya urais ili iwe imara zaidi kwa kuwa urais sio mtu. Kwa mfano akifariki leo ina maana matumaini yako yote yataisha?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…