Juhudi zifanywe uchumi umilikiwe na wazawa aka Watanzania weusi kwa 90% kuliko ilivyo sasa ambapo kwa kiasi kikubwa uchumi uko mikononi kwa wahindi, waarabu aka Waasia ambao hujiita watanzania kwa manufaa binafsi lakini ukweli sio watanzania moyoni, Hili lifanyike kwa kuweka mikakati imara kwa siri itakayonufaisha weusi aka watanzania wenyewe hasa vijana. Mikakati hiyo ijikite kwenye kutoa elimu ya uwekezaji, kutoa mikopo nafuu ya vitendea kazi, kupromote uchimbaji mdogomdogo na Serikali kuwa mnunuzi mkuu na agency wengine wenye ofisi na leseni maalum ya ununuzi wa madini.
Serikali iwekeze kwenye machimbo ya chuma na makaa ya mawe, uwekezaji huu ukifanyika na watu wetu wakiwa tayari wamepata elimu ya innovations/handcrafting na skills katika uwanja huo basi tutakimbia kwa haraka sana. Namna gani chuma kitatumika nitaelezea hapo chini.
Juhudi zifanyike idadi ya watu iliyopo itumike vizuri kiasi cha kila mtanzania kuwa productive, Wizara ya viwanda, wizara ya fedha, wizara inayodeal na vijana kuweka nguvu kiasi cha watanzania vijana wenye nguvu watumike sana kwenye uzarishaji hasa wa mazao na kuyaongezea thamani na kazi ya serikali kuhakikisha inatumia nguvu kubwa kuleta masoko na ikiwezekana inunue ndege kubwa tatu za mizigo na nyingine ndogo ndogo kama kumi, reli ya zamani itumike vizuri kwa kuongezewa ufanisi ili bidhaa ziweze kufika sokoni kwa urahisi. Wakulima waelimishwe juu ya kilimo cha kisasa cha biashara chenye tija baadala ya kulima kienyeji kama walivyozoea.
Serikali itilie mkazo kwenye elimu ya ufundi zaidi tuachane na elimu ya vyeti ikiwezekana tupeleke vijana wadogo wengi sana China na Japan wakajifunze handcrafting na skills na wakija hapa tuwatumie kwa kuwapa mikopo nafuu ya vitendea kazi, wao wakidesign na kuproduce wale waliosoma marketing na vitu vingine watatafuta masoko worldwide kwa kupata percent kwenye kila sales ya bidhaa, tukiproduce ndani vya kutosha bidhaa bora kwa gharama ndogo ya uzarishaji basi hata bei ya bidhaa zetu itakuwa ndogo kiasi cha kuvutia watu wengi kuja kufanya biashara ndani. Tanzia ni sehemu ambayo gharama za uzarishaji zinaweza kuwa ndogo sana kama CHUMA kitachimbwa, MAKAA yatachimbwa na GAS itakuwa well utilized, maana tayari kuna workfoce nyingi sana ipo mtaani inazurura ambayo inaweza kuwa very cheap (hii workforce inatumika humu na wahindi, waarabu na wachina tena kwa mateso na unyanyapaa mkubwa kwa malipo kiduchu sana, wazungu kwa kiasi fulani hunufaika sana na hii workforce kwenye uchimbaji madini na biashara nyingine angalau kidogo hawa wana utu wa kujali ubinadamu). Elimu kitolewa kwa vijana hizi garage nyingi tunazoziona mitaani nyingi zitageuka kuwa maeneo ya kuzarisha product mbalimbali na miji yetu mikubwa mingi nyumba zake zitageuka viwanda vidogovidogo, Elimu hii ya "Handcrafting na Innovations" italeta mapinduzi makubwa sana kwa watu wetu kiasi cha kusaidia sana maelfu kwa mamia ya vijana (wengi wetu ni mashahidi jinsi wachina/wahindi wanavyosumbua kwenye mitandao wakiuza bidhaa za aina mbalimbali, hii ni faidi ya teknolojia walionayo).
Dunia bado inahitaji vitu vingi sana kurahisisha mambo mengi sana kiasi cha kufanya dunia iwe bado ni soko la kila aina ya bidhaa, hali hii itategemea na bidhaa yako kwa maana ya ubunifu wako juu ya bidhaa husika hili huja baada ya kufanya market survey nzuri ( Ajira nyingine kwa watu kufanya market survey na kuuza idea).
Hayo yoote yakifanyika kwa kuanzia, ndani ya Taifa letu kutakuwa na mzunguko mkubwa wa kibiashara ambao utaleta urahisi wa makusanyo ya kodi na ongezeko kuwa la makusanyo ya kodi, Exportationa itakuwa kubwa sana na dunia itapambana kuhakikisha ina import vitu vingi vyenye maana ndani ya Tanzania hali hii italeta in and out nyingi sana Tanzania na Mambo mengi tunayohangaika nayo leo yatakaa sawa automatically, hali hii itafanya makampuni makubwa kama Caterpillar, Nike, Cocacola, Mercedes, VW, Toyota, nk kuja kufungua plant zao hapa ili kufaidi low production cost and good policy kwenye nchi yetu na hapo ndipo ajira nzuri zitakuwa zimekuja kwa watu wetu, huu utalii tunaohangaika nao utajiset wenyewe, Estate developer watafanya kazi hapo, utawaona Uber wanavyokimbia Tanzania, utaona kila rangi nzuri..