Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mi naona wewe si mwanademokrasia. Maana ya demokrasia ni hiyo unayoiona. Watu wanahama kutoka huku kwenda kule muda watakao. Au kwako mkuu demokrasia ni Lema kutoka TLP na kujiunga na CDM tu lakini kina Waitara wakifanya the same ishakuwa kuua vyama vya siasa? Mi naona wewe ujitafakari upya. Hayo mambo ya hama hama unayoyaona Hiyo ndiyo Demokrasia.
Sidjhani kama uko vzr kichwani, anyway ndio upeo uliojaaliwa!
 
Mi naona wewe si mwanademokrasia. Maana ya demokrasia ni hiyo unayoiona. Watu wanahama kutoka huku kwenda kule muda watakao. Au kwako mkuu demokrasia ni Lema kutoka TLP na kujiunga na CDM tu lakini kina Waitara wakifanya the same ishakuwa kuua vyama vya siasa? Mi naona wewe ujitafakari upya. Hayo mambo ya hama hama unayoyaona Hiyo ndiyo Demokrasia.
Tanzania ni nchi ya Demokrasia ya Vyama vingi, kwa mujibu wa katiba yetu. Rais anafanya yafuatayo kukiuka Katiba hii:
1) Kuzuia vyama vya upinzani visifanye kazi zake. Vyama vya siasa, kwa mujibu hata wa sheria ya vyama vingi, vina majukumu ya kufanya mikutano, kufanya maandamano inapobidi, tena kuna utaratibu wa kufanya maandamano, ku-protest vitendo mbalimbali vya serikali, na mengineyo. Rais Magufuli kapiga marufuku hayo yote. Rais anadai kwamba kuviruhusu vyama vya upinzani vifanye kazi zake ni kumzuia yeye asilete "maendeleo". Nakumbuka Tume ya Haki za Binadamu (ya serikali), chini ya Jaji Amiri Manento, iliwahi kuikemea Polisi kwa kuwazuia CHADEMA kufanya mikutano yao, kwa kisingizio cha serikali kuongeza siku za watu kuhesabiwa katika sensa ya kitaifa, enzi zile yalipotokea mauaji ya Daudi, 2012. Jaji Manento alifafanua kwamba CHADEMA kama chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kina haki na wajibu kuendelea na kazi zake. kufanya sensa haina maana kwamba watu na Taasisi wasifanye kazi. kisingizio cha kuwataka CHADEMA kusimamisha shughuli zao ilikuwa kwa sababu ya kuwadhibiti tu basi.
2) Chaguzi za marudio chini ya awamu ya Tano ni UDIKITETA MTUPU. Chaguzi zote zimekuwa na matumizi ya nguvu hasa dhidi ya mawakala, wagombea, viongozi wa vyama vya upinzani.
3) Kumekuwa na ushahidi wa viongozi wa serikali kuwahonga viongozi wa upinzani, uliokusanywa na mh. Nassari, na akaiwasilisha TAKUKURU. lakini baada ya Rais kumpa promosheni mtuhumiwa, TAKUKURU waligwaya kuendelea na upelelezi wao

Katika mazingira haya hii hama hama ya wapinzani kwenda CCM, ni wazi ni mbinu zinatumika
 
Ningemshauri ampe ukuu wa wilaya na wema sepetu amejitoa sana kwa chama.
 
Ndugu wanabodi:
Kwa yanayoendelea nchini hususani hili janga la hamahama ya wapinzani halina afya kwa taifa, kwani inalenga kulipeleka taifa kwenye mfumo wa chama kimoja. Mfumo ambao husisitiza kudumisha fikra za mwenyekiti wa chama.

Mfumo wa zidumu fikra za mwenyekiti wa chama ni mfumo uliopitwa na wakati na haufai kwa maendeleo endelevu

Hivyo kama watanzania tunapenda maendeleo endelevuendelevu yapaswa tuipinge nia hiyo ovu ya kuua upinzani ili tubaki na chama kimoja kinachoshika hatamu.

Lakini bado tunatumaini kubwa la kuimarisha upinzani kwani bado tunayo silàha kubwa, silaha hiyo ni Mh, Tundu Lissu.

Huyu ni mpinzani asilia,historia yake inajitosheleza.Kipaji chake cha kuongea,kujenga hoja na taaluma yake inayoshabihiana na hulka yake ya kutetea haki za wanyonge vinamfanya kuwa nguzo kubwa ya upinzani kwa sasa.

Hivyo akirudi kutoka kwenye matibabu harafu shughuli za kisiasa zikaruhusiwa kwa mujibu wa katiba, ndani ya muda mfupi upinzani utaimarika mara dufu.
Nawasilisha.
 
Mh, Rais kwanza pole kwa majukumu mazito ya kulijenga Taifa hili kisha nikupongeze kwa mafanikio unayoyapata.

Mh, Dhumuni la ujumbe wangu kwako ni kukujulisha kuwa TRA (Tanzania Revenue Authority ) wameshindwa kufanya kazi ya eneo la kariakoo. Dar es salaam..

Kama ujuavyo kariakoo ni soko, Mataifa karibu yote tuliyo pakana nayo, kuna mzunguko mkubwa sana wa pesa, ajabu ni kuwa kuna uzembe ama makusudi inayofanywa na watendaji wako.

Mh, Rais ukwepaji wa kodi kariakoo umekithiri na unatuumiza sisi tunaolipa na kukatwa kodi zetu kihalali.. ukwepaji huu wa kodi tulisha utolea maelezo hapa lakini badala ya kupungua ndio unaongezeka.

Wafanyabiashara wanatoa risiti ambazo haziendani na mauzo wayafanyayo matharani mtu aweza kuuza bidhaa zenye thamani ya tsh milioni mbili lakini akatoa risiti yenye thamani ya tsh laki moja ama elfu hamsini tu.
Huu mchezo unafanywa na wafanyabiashara karibu wote w kariakoo.! Mnunuzi akijaribu kuikataa hiyo risiti anakuwa ametengeneza uadui na muuzaji. Akija wakati mwingine sio rahisi akauziwa bidhaa kwenye duka hilo.

Mh, Rais tutaendelea kupiga kelele hizi mpaka lini? Je wafanya biashara wa kariakoo ni wakubwa kuliko serikali yako?
Kama TRA hawawezi kufanya kazi yao vema kwanini waendelee kula kodi zetu kama mshahara?
Jambo hili likifumbiwa macho litaenea Nchi nzima..
ahsante kwa kunisikiliza natumai litafanyiwa kazi

Mzalendo halisi..
 
Ndugu wanabodi:
Kwa yanayoendelea nchini hususani hili janga la hamahama ya wapinzani halina afya kwa taifa, kwani inalenga kulipeleka taifa kwenye mfumo wa chama kimoja. Mfumo ambao husisitiza kudumisha fikra za mwenyekiti wa chama.

Mfumo wa zidumu fikra za mwenyekiti wa chama ni mfumo uliopitwa na wakati na haufai kwa maendeleo endelevu

Hivyo kama watanzania tunapenda maendeleo endelevuendelevu yapaswa tuipinge nia hiyo ovu ya kuua upinzani ili tubaki na chama kimoja kinachoshika hatamu.

Lakini bado tunatumaini kubwa la kuimarisha upinzani kwani bado tunayo silàha kubwa, silaha hiyo ni Mh, Tundu Lissu.

Huyu ni mpinzani asilia,historia yake inajitosheleza.Kipaji chake cha kuongea,kujenga hoja na taaluma yake inayoshabihiana na hulka yake ya kutetea haki za wanyonge vinamfanya kuwa nguzo kubwa ya upinzani kwa sasa.

Hivyo akirudi kutoka kwenye matibabu harafu shughuli za kisiasa zikaruhusiwa kwa mujibu wa katiba, ndani ya muda mfupi upinzani utaimarika mara dufu.
Nawasilisha.
Je hiyo itasaidia? Maana ww mpinzani unaweza kupata ushindi lakini usitangazwe kwa kuwa mwenye haki ya kutangazwa ni aliyeshindwa. Utafanyaje? Kumbuka hapo ww inakuwa huna hata rungu mkononi lakini mwenzio analindwa na watu wenye SMG zisizo na idadi.
 
kuna muda waeza ongea kitu kwa usahihi ila ukaonekana mnafki.
Ngoja waje
 
kuna muda waeza ongea kitu kwa usahihi ila ukaonekana mnafki.
Ngoja waje
Aliye turoga sijui ni nani? Nimebahatika kutembelea Nchi nyingi hawana huu upuuzi wa kutoa risiti pungufu.
Nimeenda kampala hawana huo ujinga sio Lilongwe, Lusaka, ama Harare.. kwanini wao waweze sisi iwe kituko?
 
Mkuu;
Naomba uweke hapa jina la duka ili malalamiko yako niyatume sehemu husika.
 
Mkuu;
Naomba uweke hapa jina la duka ili malalamiko yako niyatume sehemu husika.
Mkuu lingekuwa duka moja wala sikuwa na haja ya kulileta hapa barazani ama ingekuwa peke yangu nisingekuwa na haja ya kulipeleka kwa Mh Rais, huu ni ugonjwa ambao ama umekuwa sugu. Au unaenea kwa kasi katika eneo zima la kariakoo..tena yamkini unaenezwa makusudi.
 
Mkuu ni vigumu sana kupeleka malalamiko ya aina hii kwa muhusika mkuu bila kujua hasa ni duka/maduka gani.

Ingekuwa ni vizuri sana ukayataja hayo maduka ili malalamiko yawe ya uhakika zaidi lakini kikubwa zaidi wahusuka wakuu wajue sehemu ya kuanzia.
 
Hebu piga picha hiyo risiti uibandike kisha tuelezee uliuziwa nini cha thamani... kama huwezi acha ukuda... Tambua pia kuisumbua mamlaka ni kosa pia kisheria
 
Je hiyo itasaidia? Maana ww mpinzani unaweza kupata ushindi lakini usitangazwe kwa kuwa mwenye haki ya kutangazwa ni aliyeshindwa. Utafanyaje? Kumbuka hapo ww inakuwa huna hata rungu mkononi lakini mwenzio analindwa na watu wenye SMG zisizo na idadi.

..uchaguzi mkuu una WAANGALIZI WA KIMATAIFA.

..Siyo rahisi CCM kufanya UHUNI kama wanavyofanya sasa hivi ktk chaguzi za marudio.

..Pia ni kazi kubwa kuiba maeneo yote nchi nzima.

..Wapinzani wanatakiwa waelekeze nguvu kubwa zaidi kwenye kupata wabunge wengi zaidi.

..wapinzani wakiweza kufikisha asilimia 40+ ya wabunge CCM watakuwa hawana uwezo wa kupitisha miswada kimabavu bungeni.

..kila mswada, bajeti, itabidi ipitishwe kwa njia ya MARIDHIANO.
 
Aliye turoga sijui ni nani? Nimebahatika kutembelea Nchi nyingi hawana huu upuuzi wa kutoa risiti pungufu.
Nimeenda kampala hawana huo ujinga sio Lilongwe, Lusaka, ama Harare.. kwanini wao waweze sisi iwe kituko?
Kwenye hizo nchi nyingine vipi kuhusu matumizi sahihi ya hayo makusanyo? Mara nyingi Mwananchi yeyote akitambua kuwa kodi yake anayolipa inatumika vizuri kumletea maendeleo huwa hawana shida.... Lakini pale anapoona wazi kabisa fedha zinafujwa na serikali yake atatumia kila mbinu kukwepa kulipa au kulipia kidogo.....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom