Mi naona wewe si mwanademokrasia. Maana ya demokrasia ni hiyo unayoiona. Watu wanahama kutoka huku kwenda kule muda watakao. Au kwako mkuu demokrasia ni Lema kutoka TLP na kujiunga na CDM tu lakini kina Waitara wakifanya the same ishakuwa kuua vyama vya siasa? Mi naona wewe ujitafakari upya. Hayo mambo ya hama hama unayoyaona Hiyo ndiyo Demokrasia.
Tanzania ni nchi ya Demokrasia ya Vyama vingi, kwa mujibu wa katiba yetu. Rais anafanya yafuatayo kukiuka Katiba hii:
1) Kuzuia vyama vya upinzani visifanye kazi zake. Vyama vya siasa, kwa mujibu hata wa sheria ya vyama vingi, vina majukumu ya kufanya mikutano, kufanya maandamano inapobidi, tena kuna utaratibu wa kufanya maandamano, ku-protest vitendo mbalimbali vya serikali, na mengineyo. Rais Magufuli kapiga marufuku hayo yote. Rais anadai kwamba kuviruhusu vyama vya upinzani vifanye kazi zake ni kumzuia yeye asilete "maendeleo". Nakumbuka Tume ya Haki za Binadamu (ya serikali), chini ya Jaji Amiri Manento, iliwahi kuikemea Polisi kwa kuwazuia CHADEMA kufanya mikutano yao, kwa kisingizio cha serikali kuongeza siku za watu kuhesabiwa katika sensa ya kitaifa, enzi zile yalipotokea mauaji ya Daudi, 2012. Jaji Manento alifafanua kwamba CHADEMA kama chama cha siasa chenye usajili wa kudumu kina haki na wajibu kuendelea na kazi zake. kufanya sensa haina maana kwamba watu na Taasisi wasifanye kazi. kisingizio cha kuwataka CHADEMA kusimamisha shughuli zao ilikuwa kwa sababu ya kuwadhibiti tu basi.
2) Chaguzi za marudio chini ya awamu ya Tano ni UDIKITETA MTUPU. Chaguzi zote zimekuwa na matumizi ya nguvu hasa dhidi ya mawakala, wagombea, viongozi wa vyama vya upinzani.
3) Kumekuwa na ushahidi wa viongozi wa serikali kuwahonga viongozi wa upinzani, uliokusanywa na mh. Nassari, na akaiwasilisha TAKUKURU. lakini baada ya Rais kumpa promosheni mtuhumiwa, TAKUKURU waligwaya kuendelea na upelelezi wao
Katika mazingira haya hii hama hama ya wapinzani kwenda CCM, ni wazi ni mbinu zinatumika