Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Kitufe cha like kimeenda wapi siku hizi?

Anyways, kweli tupu. Tumefikishwa hapa tulipo na watu wanaofanya kazi kwa mazoea. Mimi ninashauri atafute mwanasheria mzuri sana adraft standard contracts za Mawaziri wote, ili atakayelala apewe mwezi mmoja wa kuondoka ofisini kama ilivyo kwenye mashirika binafsi yaliyo makini. Pia baraza la mawaziri lipungue kwa nusu kabisa..makatibu wakuu wanatosha kusimamia shughuli za wizara kukiwa na mawaziri wachapakazi wanaosimamia wizara 2 kila mmoja.

Ni kweli kwamba hapa kwenye uteuzi ndio kwenye make or break..alishaharibu pale kwa AG asiendelee na kuharibu. Vinginevyo hamu yake ya kufanya mabadiliko itaishia kwenye kumbadilishia mapigo ya moyo wake.
 
Kwa mtazamo wangu kwenye hio list Mwakyembe, Prof Muhongo na Mwigulu ni watu bora zaidi.
Prof Muhongo ni mtendaji mzuri, chini ya uwaziri wake amesaidia sana kupunguza gharama za ufungaji nguzo za umeme na upatikanaji wake.
Na mkakati wa usambazaji umeme ulikuwa unaenda kwa kasi nzuri.
Ni ajali za kisiasa tu ndo zimemuharibia credibility yake.
 
Mnamfichia aibu siyo? Juzi anaapishwa niliona aibu alishindwa kusalimia hata wageni kwa Kiinglish! Wengine wanajitoa akili eti tunatukuza lugha za Wageni wakati mwanao anasoma English Medium, Wadanganye hao siyo Mimi.

Kwenye kampeini alisifiwa sana kwamba anajua vilugha vyoote kumbe mweupe Kimataifa.
 

Siasa za Tanzania wakati mwingine huangalia ku-balance kikanda ndio maana unakuta kuna viongozi wabovu lakini lazima wawepo sababu ndio pekee wapo kwenye baadhi ya maeneo.Shukuru Kawambwa,Anna Tibaijuka,Andrew Chenge,William Ngeleja,Saada Mkuya,George Mkuchika,Maghembe,Hawa Ghasia,Sofia Simba,Makame Mbarawa,Nkamia,Marry Nagu,Magreth Sita, hawa hawastahili kabisa kurudi

Naamini kuna ambao walifanya vizuri ambao watarudi kama Jestina Mhagama,Kasim Majaliwa,Mwakyembe
Sura mpya kama Hassan Zungu,Kangi Lugola,Faustine Ndungulile,Adadi Rajabu ningependa ziongezwe
 

Shost mbona umeweka unaoona wewe hawafai weka na wanaofaa basi unaoona wewe tuwapime pia!
 

Naungana na wewe mkuu kwa hoja yako
 
Tatizo lenu mnamuona Dr Magufuli ni kilaaaza wala haelewi na kuwajua watu, he has been in the government for over 20 years as the cabinet minister. Na watu wote wa caliber yake ambao anawajua ni wachapakazi na sio mafisadi woote anawajua. Huwezi mshauri kuhusu hili. Ulivyoanza na Prof Muhongo tuu nikajua unaandika utumbo au umetumwa na wafanya biashara ambao hawapendi mtu anayewazibia ulaji. Kaa kimya kamanda huelewi nchi yetu inavyokwenda.
 
Tanzania sasa tumempata Rais mpya wa awamu ya 5, ambaye watanzania wengi tunamatumaini atatekeleza ahadi zake kwa asimilia zaidi ya 90, katika ahadi zake aliahidi kufufua viwanda , katika kufufua viwanda asisahau zao la mkonge ,zao hili kwa sasa limekuwa na soko kubwa sana ukilinganisha na kipindi cha nyuma mkonge kwa sasa grade ya SS kwa tani 1 ni takribani US dollar 2500- 3000 katika soko la dunia na local market ni makadirio ya Tsh 2,500,000 kwa tani , na SSUG ni takribani US dollar 1900-2200 kwa tani

Hivyo basi katika mashamba ya mkonge ajira nyingi zinaweza zalishwa na vijana wengi kuajiriwa wasomi na wasio wasomi na kulipwa vizuri , mashamba mengi yamebinafsishwa kwa wawekezaji ambao wanapunja maslahi ya wafanyakazi hasa unskilled labor kwa kuwapa ujira wa 4950 kwa siku ambayo ni ndogo kulinganisha na kinachozalishwa pia chama cha wafanyakazi mashambani TPAWU wakupe ushirikiano kurekebisha mishahara ya mashambani itakayokidhi maisha ya sasa

Mashamba mengi yamekufa na machache yanauhai , hivyo juhudi zifanyike kurudisha zao la mkonge katika ubora na kupunguza tatizo la ajira kwani mahitaji kwa mkonge duniani ni makubwa sana kulipo hapo awali

Nawasilisha, nikiwa nimefanya research ya kutosha kuhusu zao la mkonge Tanzania
 
Talking about "Word processor", that makes sense to me. Hakuna zaidi ya kile ambacho ume feed.



Yule mwingine pamoja na kuwa aligombea uongozi, degree ya Uchumi na kuongoza wizara ya fedha alikiri bado HAJUI NI KWANINI SISI NI MASKINI!

Wanasema "Ndege wa aina moja huruka pamoja"
 
Huyo makamba ndio hata unaibu usimpatie, hajitambui..!!
 
Shost mbona umeweka unaoona wewe hawafai weka na wanaofaa basi unaoona wewe tuwapime pia!

mkuu nimesema bora akateuwa vijana wenye elimu isiyo na shaka, ambao hawajawahi kuwa mawaziri, sio viongozi wa chama, na km hawapo ktk wabunge wote 200 wa ccm basi ana mamlaka ya kuteuwa wabunge 10 ambao anaweza fanya nao kazi
 
nyie akina Riz si ndio hamuishi kulalamika kuhusu wagala sasa leo mnaaza kuwapigia kampeni wapewe nafasi

flip flopping
 
Asandeee.

Hizi ni fursa ambazo serikali imekuwa haizioni. Pia badala ya kuzalisha crude fibres, watanzania wawezeshwe kuwekeza katika kutengeneza downstream products ambazo naamini zina soko pia hapa nchini. Mfano mdogo ni magunia. Hizi salfet zinaharibu mazingira na ni kero sana. Badala yake yakitumika magunia mazingira yetu yatakuwa salama huku tukiendelea kunufaika na "made in Tanzania"

Naunga mkono hoja
 

Yule mwingine alimwambia bibi yangu wa mwanarumango akasome ilani ktk mtandao
 
Tatizo falsafa yake (ACT-WAZALENDO) na ya Magufuli (CCM) ni tofauti mfano ACT wanataka Katiba mpya ni ile inayotokana na matakwa ya wananchi (rasimu ya Warioba) CCM wanataka katiba mpya rasimu ya CCM (ya Sitta na Samia Suluhu) nk
 
Yaani hapa nacheka mwenyewe tu!
 
Ni ushauri mzuri mno,hongera.Frankly hata mimi singependa kuwaona watu hao katika any position of power tena. Wametu-let down sana.Akimuweka yeyote kati ya hao tutajua kwamba hana nia ya kweli ya kuwasaidia watanzania,na infact yeyote ambaye alikuwa kwenye awamu ya nne.Haikuwa serikali makini kabisa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…