Kwanza napenda kutumia nafasi hii kuku pongeza kwa kazi unazo fanya kwani wewe ni mtumishi wetu na tuna haki ya kuku tuma na kukushauri tunapo ona mambo hayaendi sawa.
Kimsingi wewe ni kiongozi unaye toka miongoni mwetu sisi wana damu na ndo maana sio rahisi saana kufanya kila kitu kwa ukamilifu wote kama wafanyavyo malaika sababu wewe ni mwanadamu kama sisi. Lakini napenda kutanguliza angalizo nisi nukuliwe vibaya kwa hiki ninacho kiandika kwani pia hakiwezi kuwa ndio uhalisia wote wa namna mambo yalivyo kwani hata mm ni binadamu kama wewe ulivyo.
Muheshimiwa Raisi; kumekuwa na propaganda nyingi saana mtaani na malalamiko ya hapa na pale kuhusu hali ya uchumi mifukoni mwa watu kitu kilicho pelekea kuibuka kwa misemo mbalimbali kama vile vyuma vimekaza , kuisoma namba na kadhalika .sasa nikweli malalamiko hayo yana uhalisia kwamba mtaani hela haipo kihivyo?
Muheshiwa raisi mm kwa upande wangu naweza nikasema nikweli kabisa mtaani hela imekuwa ngumu vya kutosha, hii sio kwasababu sisi hatufanyi kazi au kwasababu sisi tulizoea kupiga au kwasababu sisi tulikuwa mafisadi la hasha ni kwasababu ambazo kwa namna moja au nyingine zimesabanishwa na ninyi watu tunao watuma kufanya kazi badala yetu.
Muheshiwa Raisi; ikumbukwe kwamba mara uchaguzi unapo isha sisi wana nchi wa huku kantawa maeneo ya sumbawanga huwa tunakuwa tume yakabidhi mamlka yetu yote ya kuamua na kutenda kwenu ninyi mlio bahatika kuaminika ili mtende badala yetu na sisi tunakuwa wasikilizaji tulo jaa matumaini kusubiri unafuu wa maisha na huduma kupitia mikakati mingi ambayo ninyi mnajiwekea kama viongozi.
Nashukuru kwa sababu naona kupitia luninga na kusikiliza redio ya kwamba kuna mambo mengi yanafanyika huko tanzania kama yale mabarabara ya juu tunasikia kunatreni huko ambazo zina tumia umeme tunasikia kuna madege makubwa yale ya ulaya kwakweli sisi tuna shukuru saana kwani hata hao wananchi wa huko tanzania Dar es salaam wanahaki pia ya kupatiwa hayo yote kwani nao niwatanzani kama sisi.
Hiku kwetu toka ulivyo kujaga kipindi kile ukiwa waziri wa ujenzi ukafanya mkutano pale karibu na kanisa la roma kwenye ile shule yao itwayo msakila, wakati ule muheshimiwa amekutuma kuja kusimamia barabara ya lami mlio tuambia kwamba ni msaada wa marekani, toka wakati huo sisi tupo vilevile baba, isipokuwa tunawashukuru saana kwani ule umeme mlotuwashia na muheshiwa jakaya bado una waka vizuri .
Baada ya utangulizi huo muheshiwa Raisi naomba nijikite kwenye hoja yangu ya msingi....
NI KWA NINI FEDHA HAIPO MTAANI?
Baba nikweli kabisa hela haipo mtaani lakini ukiwauliza watu wa fedha pale benki kuu lazima wata kwambia hamna kitu kama hicho bali wanao lalama ni wapigaji hawafanyi kazi. Huenda kitaalamu wako sawa kwani wao ndio wanajuwa kiuhalisai kunakiasi gani kwenye mzunguko.
Muheshimiwa Raisi; ni kwanini hakuna fedha mtaani ? Sio kweli kwamba fedha hakuna mtaani bali kinadharia zipo na kiuhaliaia hazipo hii imesababishwa jambo dogo tu ambalo hata kesho ukilipiga marufuku mambo yana rudi kama zamani.
Mmeamua kwa makusudi kama viongozi kuwa ruhusu hawa ninyi mnao waita wawekezaji kutoka huko barahindi na uchina wamekuja kuwekeza nchini mwetu kwa lengo zuri tu walipe kodi zitunufaishe kwenye jamii lakini imekuwa ndivyo sivyo, huku kwetu kila ki grocery kidogo cha bia kina mashine iitwayo slotting machine watu hutumbukiza fedha zao humo wakiamini wanaweza kula mamilioni ya fedha.
Huku pia kume kuwa na michezo mingi ya betting kitu ambacho kwa kweli kinatia mashaka makubwa .
Tumesikia na huko kwenu pia na nchi nzima haya mamashine yame jaa kila mahala watu wanatupia fedha humo watu wana beti kila uchao masaa ishirini na nne. Sasa nini ni matokeo ya hayo yote niliyo yaeleza ? Ni hivi madereva bodaboda, piki piki , wauza matunda , wauza mboga , wauza vitumbuwa , wachoma mahindi nk wote hawa huwa ikifika mida ya kufunga kazi au hata wakati wakazi hupendelea kwenda kucheza huko kutupia fedha kwenye hizo mashine na kubet wakiamini watapata fedha nyingi kwa mkupuo kitu ambacho hakiwezekani .
Mm ninacho kiona hapa yaani fedha yote ambayo ingepaswa kuwa kwenye mzunguko ana kaa nayo mtu mmoja tu kitu kinacho pelekea watu kudhani hakuna fedha mtaani na kuharibu mzunguko mzima wa fedha. Mkuu najuwa unaweza kukosa kuniamini lakini huo ndio ukweli wenyewe kwani sisi tupo huku mtaani na hiko ndicho tunacho kiona.
USHAURI
Muheshiwa raisi huenda watalamu wetu hawalioni hili au hawataki kujaribu kufikiri ni kwa namna gani wanasema kunafedha kiasi fulani kwenye mzunguko ilihali wana nchi wanalia ya kwamba fedha hakuna mtaani, pengine wamechoka au hawataki kuku saidia , kumbe fanya yafuatayo;
1), vunja mikataba yote ya hovyo ya hawa jamaa kutoka bara hindi na china waojifanya wanaendesha biashara ya bahati nasibu.
2). Piga marufuku michezo yote ya kubeti na coin machines ambayo imezagaa kila kona
3). Zuia matangazo yoote kwenye runinga yanyo jenga ari na imani kwa wana nchi ya kwamba ukicheza hizo biko tatu mzuka utapata fedha nyingi na kubadilisha maisha.
4). Waambie washauri wako wamaswala ya kiuchumi wawe wabunifu wa mambo hapo tutafika muheshimiwa.
Mwisho napenda kutanguliza shukra zangu nyingi kwako lakini nikutakie mapunziko mema ya mwisho wiki.
Ni mm chilemba wa mela pamputi.
Sent using
Jamii Forums mobile app