Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Write your reply...Nchi wslipokea ikiwa nzuri leo zogo hadi kwenye daladala ninani hasa anateka watu na kupiga risasi?
 
Ndugu mhariri,
Napenda kutumia nafasi yako adhimu kumfikishia Rais wetu mpendwa Comrade John Pombe Magufuri ushauri wangu binafsi kuhusu wimbi hili zito tunalopitia la mheshiwa Tundu Lissu kuyanadi hayo anayoamini huko Ughaibuni, hakika hili sio jambo dogo hata kidogo ni bora busara itumike hasa kwa namna na mwenendo mzima wa kulishughulikia suala hili. Ninachokiamini mimi hizo ni hasira tu kwani kinachomsuma ni chuki alizonazo juu ya viongozi kwa namla suala laki la mashambulizi lilivyochukuliwa (kama kweli Bunge halikumpa msaada wowote wa kimatibabu) na hivyo basi ameamua kujilipua……..”liwalo na liwe”. Ni ukweli usiopingika hata ndugu wawili walio katika uhasama mara nyingi huungana wakati wa matatizo na kuziweka tofauti zao ili mradi tu watoke katika janga linalowasibu kwa wakati huo na tofauti zao huendelea baada ya hapo ijapokuwa uzoefu unaonyesha mara nyingi baada ya matatizo hayo ndugu hao husamiheana na kuendeleza mahusiano kwa mstakabari mpana wa baadaye…….
Ushauri
Napenda kumshauri mambo yafuatayo Rais wetu mpendwa:
  • Pindi arejeapo nchini mheashiwa Tundu Lissu, serikali isimchukuliwa hatua yeyote kwa haya ayafanyayo

  • Kama itampendeza Comrade Rais, basi amkaribishe Mheshimiwa Tundu Lissu Ikuru waweze kuteta kidogo ili kuona shida hasa iko wapi kwa maslahi mapana ya nchi hii.
Sababu za kutoa ushauri huu;
  • Sina uhakika kama kweli Mheshiwa Tundu Lissu amepata udhamini kutoka nje ili afanye hayo afanyayo isipokuwa ninaamini kwa kufanya hivyo ana uhakika atapata “support” kutoka nje za magharibi dhidi ya serikali na nchi yetu kwa ujumla.

  • Ni ukweli usiopingika kuwa nchi za magharibi hazitaki mafanikio ya nchi za kiafrika hata kidogo na hivyo wanatafuta mwanya vyovyote iwavyo ili mradi tu wapate kuingilia mambo ya ndani ya nchi husika na kufanikisha agenda zao……..nakusihi sana Comrade usiingie katika mtego huu kwani hatimaye huenda ikawa uharibifu……..kwani mifano hai wote tunaijua na kuisikia……..
Hitimisho
Tujifunze kutoka kwa majirani zetu Kenya…..Rais Uhuru Kenyatta alijua wazi kitendo cha hasimu wake Bwana Raila Odinga kujiapisha lilikuwa kosa la UHAINI lakini busara ilitumika kwa namna ya kuenenda na suala hilo ili mradi tu nchi haiingie katika msukosuko usio wa lazima…...
Benedict Kanaku
+255769082295
Kwenye ushauri wako paragraph ya kwanza. Hapo sikubaliani na wewe,kuwa amwite Lissu Ikulu! HAPANA.
Roho zetu ni vichaka vinene huwezi jua unayemshauri anaupokeaje ushauri wako.
Tumeona mwandishi wa habari kukatwakatwa kwenye ubalozi wa saudia huko uturuki. Technology umekuwa sana, anaweza akatoka huko akiwa mzima lakini asiwe salama. Watafute ukumbi hata kama wa harusi, waruhusu Lissu aende na ulinzi wake na kama kuna haja ya kutumia kipaza sauti basi aende na chake. Ama vingevyo watumie simu. Namshauri Lissu akirudi ajihadhari na press na waandishi wa habari. Vile vidude wanavyoweka mezani wasije pandikiza vyenye perfume.







Sent using Jamii Forums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom