Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Hujajibu nikichouliza na ulichojibu sijauliza.

Kwa msingi huu nakubali hamuendi popote.

Mtabaki kwenye umasikini, maradhi na ujinga.
Nikujibu ili iweje? Nipoteze muda wangu kujibu mtu mwenye mawazo ovu? Hata sasa nimeheshimu hisia zangu kuandika haya...Hustahili majibu yangu wewe!
 
Mkuu utaua.

Umenikumbusha kulikuwa na vita moja kati ya wanajeshi wa Kikristo na Kiislamu nchini Lebanon.

Basi kuna vijiji fulani vilikuwa vinafuata upepo wa vita. Wakija wanajeshi wa Kikristo wakiwauliza wanavijiji nyie ni dini gani? Wanasema wao Wakristo.

Wakija wanajeshi Waislamu wakiwauliza nyie dini gani? Wanasema Waislamu.

Mradi mwenye nguvu mwambie anavyotaka kusikia ili wewe unusurike, bila kujali ukweli.

Sasa unaposema anaweza kuja rais akamponda Magufuli na watu wakamshangilia umenikumbusha hao wanavijiji wa Lebanon ambao walikuwa bendera kufuata upepo.
 
Nikujibu ili iweje? Nipoteze muda wangu kujibu mtu mwenye mawazo ovu? Hata sasa nimeheshimu hisia zangu kuandika haya...Hustahili majibu yangu wewe!
Sasa mbona unaendelea kujibizana na mtu mwenye "mawazo ovu"?

Huoni kwamba habari ya kupoteza muda ni kisingizio tu, kwa sababu kama huna muda wa kupoteza usingejibizana nami kabisa?
 
Nimezungumzia suala la kupendwa au suala la watu kuonekana kufurahia na kuombea rais akutwe na umauti?! Hata JK watu walikuwa hawampendi lakini hatukuwahi kushuhudia haya!! Hizi kauli za kwamba sijui "mtenda haki", sijui nini na nini ni kujaribu kufanya ujanja wa mbuni, kuficha kichwa chini wakati kiwili kiwili kinaonekana!!!

Tumeshuhudia majumba yakibomolewa hovyo hovyo kule Kilwa Rd... ndo utendaji haki wa wapi huo?!

Tumeshuhudia watu wakipotea, akina Saanane, Azory Gwanda, na wengine kuokotwa kwenye viriba, n.k... mnataka kusema huko ndo kutenda haki?!

Kwanini msifikrie hiyo ndiyo sababu iliyowafanya watu wapige shangwe badala ya hizi kauli mbiu za kutenda haki?! Kawatendea haki nani dhidi ya akina nani, ili tujiridhishe hao "dhidi ya..." ndiyo waliokuwa wanafurahia?!
 
Wengi wapi? Raia mmoja wa israel ni sawa na raia elfu nchi nyingine , hivyo jibu unalo hapo.
Hao raia 1000 wa nchi nyingine ni wale wenye fikra kama za kwako! Na kama hujaona hao wengi, sorry, sina namna ya kukusaidia!!
 
Maisha au ulimwengu ni mzunguko, na watu hatufanani , hivyo zamu ya dhaifu imeshapita na , sasa ni zamu nyingine zamu ya kunyoosha hivyo watu watulie tu.
 
Hao raia 1000 wa nchi nyingine ni wale wenye fikra kama za kwako! Na kama hujaona hao wengi, sorry, sina namna ya kukusaidia!!
Sijaomba kusaidiwa na wewe sorry ya nini sasa? Na ulichosaidia hapo sikioni , hahaha usijihami hao 1000 ndio nyie , asante kwa kujitambua.
 
Sijaomba kusaidiwa na wewe sorry ya nini sasa? Na ulichosaidia hapo sikioni , hahaha usijihami hao 1000 ndio nyie , asante kwa kujitambua.
Ni nani aliyetukuza watu wa taifa lingine kama sio wewe?! Sasa unakwepa vp kutoka kwenye hilo kundi lenu la watu 1000 mnaojiona si lolote si chochote mbele ya Mwisrael mmoja?!

Btw, utasemaje nilichosaidia hukioni wakati nimekuambia wazi kwamba siwezi kukusaidia?! Ikiwa sentensi fupi kama hiyo umeshindwa kuelewa, hakika siwezi kushangaa unapojaribu kuweka rehani utu wako na wenzako mbele ya Mu-Israel 1!
 
Maisha au ulimwengu ni mzunguko, na watu hatufanani , hivyo zamu ya dhaifu imeshapita na , sasa ni zamu nyingine zamu ya kunyoosha hivyo watu watulie tu.
Hakuna kunyoosha bila viwango na nidhamu.

Ukitaka kunyoosha hivyo utaunguza. Maana hata pasi ina moto wake kwa nguo tofauti, sasa ukitaka kunyoosha nguo kwa kupandisha moto mpaka juu, wakati nguo ya nylon, utajikuta unaunguza nguo.

Hoja ya kunyoosha naielewa na nimeitaja hapo juu, kwamba kulikuwa na haja ya kunyoosha mambo fulani yaliachiwa sana.

Lakini, kunyoosha kuna lazimisha kutukana wananchi? Rais ni lazima awe na kauli mbovu ili anyooshe?

Hiyo anayenyoosha mwenyewe una hakika ananyoosha kweli au anacheza mchezo wa maigizo ya kunyoosha?

Mbona tunaambiwa kauzia nyumba za serikali mpaka kimada wake na ndugu yaje kinyume cha utaratibu?

Mbona anafanya manunuzi makubwa nje ya bajeti na bila kufuata utaratibu wa tenda wala ukaguzi wa mahesabu?

Akiwa anawapiga hela kubwa hapo, na kuwapa maigizo ya kunyoosha, mtajuaje?
 
Na awamu ya dhaifu nayo uifafanue ehe kilitokea nini ?
 
Hakuna ulichonisaidia na sijakuomba kufanya hivyo , ukweli utabaki kuwa kweli na umeelewa kiroho safi , hayo maneno mengine ndio ya wale 1000.
 
Hakuna ulichonisaidia na sijakuomba kufanya hivyo , ukweli utabaki kuwa kweli na umeelewa kiroho safi , hayo maneno mengine ndio ya wale 1000.
Wapi nimekuambia nimekusaidia?! Ni kweli nimeelewa kuhusu wale 1000 manake mashabiki wengi wa Magufuli uelewa wenu ni finyu, ndo maana mnakidhi 1000 nyie kuwa sawa na Mwisraeli mmoja!!
 
Na awamu ya dhaifu nayo uifafanue ehe kilitokea nini ?
Chochote kikichotokea ni irrelevant kwenye point zangu ambazo hujazijibu.

1. Hakuna kunyoosha nchi bila viwango na nidhamu.

2. Magufuli si mtu wa kunyoosha nchi, anafanya maigizo ya kunyoosha nchi, kwa sababu, na yeye ni fisadi.

Huko kwa Kikwete kama kulikuwa na udhaifu, udhaifu huo hauondoi point zangu mbili za hapo juu.
 
Wapi nimekuambia nimekusaidia?! Ni kweli nimeelewa kuhusu wale 1000 manake mashabiki wengi wa Magufuli uelewa wenu ni finyu, ndo maana mnakidhi 1000 nyie kuwa sawa na Mwisraeli mmoja!!
Uzuri ni kuwa umeelewa kuwa ufinyu wa akili ni kubwabwaja na kuuliza mambo ya kuombeana ubaya, hivyo hao 1000 mmijitambua vizuri.
 
Ukweli uko wazi , mambo yananyooshwa safi kabisa , na nidhamu ilioporomoka inajengwa na kizazi kijacho kitakula matunda yake , sasa hivi tunakula matunda ya zaifu.
 
Wezi wakubwa nyie.. magorofa mnayo jenga mwanza na bashite mnadhani hatujui
Ukweli uko wazi , mambo yananyooshwa safi kabisa , na nidhamu ilioporomoka inajengwa na kizazi kijacho kitakula matunda yake , sasa hivi tunakula matunda ya zaifu.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…