Duniani kote, hakuna mkweli na mtenda haki akapendwa. Angalau Injili na Quran vinasema hivyo.
Yesu hakusulubiwa kwa vile alitenda uovu, mifano ipo mingi. Kama Mungu ni ukweli basi wengi wetu hatumpendi Mungu kwa yakini, tunazipenda nafsi zetu ambazo zimejaa uovu, dhuluma na unafiki.
Anayeitaka haki ni lazima ajikane, sisi hatujajikana, bado hatujaweza kuuza tulicho nacho tumfuate.
Hata leo hii tunaulizwa, kati ya Baraba na Yesu nani asulubiwe, bila aibu tunasema Yesu.
Njia ya uzima haijanyoika, imejaa dhiki, mahangaiko na dhihaka. Raid Magufuli ni mtu wa haki, hana cha kujitafakari, atende kama alivyopanga kutenda, dunia haijawahi kubadilika, inapenda dhuluma kuliko haki.
Kila mmoja wetu anaifahamu nafsi take, kama ni ya dhulma au ya haki. Kwa lolote ulifikialo jiulize Mimi ni wa dhulma au wa haki halafu chukua hatua stahiki