Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Ni vitu gani vinamuangusha Magufuli katika uongozi wake ambavyo kama akiviweka sawa basi anaweza kuwa the best president in East and Central Africa??? Naona kuna malalamiko kadha wa kadha kutoka kwa wananchi wengine wanakubaliana na movement zake wengine wanaona kama anafanya vitu ambavyo si sawa.

kwa maoni yako Endapo ungepewa nafasi ya kumshauri Rais Magufuli ni kitu gani ungependa akifanyie reformation?

Tunashukuru kwa kutoa nafasi tumshauri, lakini ukweli ni kuwa hawezi kubadilika kupitia ushauri wetu. Kama ni kubadilika angebadilika miaka hii mitano ya mwanzo.

Kwa hili la kutokubadilika siwezi kumlaumu sana maana huo ni ubinadamu hasa kwa mtu mwenye hela au madaraka. Mtu kama yeye anaweza kubadilika akikosa madaraka au hela.

Angekuwa chini ya katiba ya US angebadilika kama alivyobadilishwa Trump, ila kwa katiba hii usitegemee abadilike, tuombe Mungu amalize muda wake bila kuacha madhara zaidi ya haya aliyoyafanya.
 
Kitu kikubwa alichoborongo ni uchaguzi,, ndiyo umeharibu kila kitu
 
Ni vitu gani vinamuangusha Magufuli katika uongozi wake ambavyo kama akiviweka sawa basi anaweza kuwa the best president in East and Central Africa??? Naona kuna malalamiko kadha wa kadha kutoka kwa wananchi wengine wanakubaliana na movement zake wengine wanaona kama anafanya vitu ambavyo si sawa.

kwa maoni yako Endapo ungepewa nafasi ya kumshauri Rais Magufuli ni kitu gani ungependa akifanyie reformation?

Huyu jamaa John Joseph Pombe Magufuli Alisha jitanabaisha kuwa YEYE HUWA HASHAURIKI NA UKIMSHAURI NDIYO UNAPOTEZA KABUSA.
Huyu ni Rais mwenye vimelea vya UDIKTETA!!!
 
  • Thanks
Reactions: VMD
.... Otherwise anaonekana kuwa na nia njema ya kutupeleka mbele lakin sustainability ya mbinu zake ni short lived akitoka madarakani,hardly mwezi mmoja.
Mkuu, unaamini hili uliloandika? JKN anafiti kiasi kikubwa kwenye maelezo yako haya. Hakuna mjadala kabisa kuhusu nia ya Mwalimu kwa taifa lake. Kwa hilo, binafsi, alijidhiki kabisa. Alijipa the minimum kumwezesha kufanya kazi na kuwawezesha wananchi wake kwa kadiri rasilimali za taifa zilivyoruhusu. Alianguka kwa kung'ang'ania mikakati mibovu na kutoruhusu mawazo mbadala.

Lakini bado najiuliza kama kweli kuna mfanano katika awamu hii. The apparent magnitude of excess and reckless is almost alarming.
 
Eleweni kuna Watawala na Viongozi
Hapo sasa Tanganyika tupo wapi kwa sasa iwapo Wabunge wana teuliwa na mtu mmoja kwa sasa
 
Aruhusu Uhuru wa watu kusema, kumkosoa ata anapokosea na kukosolew arekebshe taratbu

Aachie kanuni na taratbu zngne ziendelee sio Kila ktu asubiriwe yeye kuamuru wakt Kuna mamlak ambazo zpo zinatekelez kisheria.
 
Ni vitu gani vinamuangusha Magufuli katika uongozi wake ambavyo kama akiviweka sawa basi anaweza kuwa the best president in East and Central Africa??? Naona kuna malalamiko kadha wa kadha kutoka kwa wananchi wengine wanakubaliana na movement zake wengine wanaona kama anafanya vitu ambavyo si sawa.

kwa maoni yako Endapo ungepewa nafasi ya kumshauri Rais Magufuli ni kitu gani ungependa akifanyie reformation?
Moja, aache Uongo

Mbili, arudie andiko lake la PhD, hatutaki vyeti fake sisi
 
Akitaka kweli akumbukwe basi atubadilishie katiba hii, aruhusu ile ya Warioba ndio iwe katiba yetu. Pamoja tutengeneza system ambayo hata mtoto mdogo akituongoza hatuwezi yumba. Wapinzani sio maadui wa taifa hili, pia akumbuke duniani tunapita tu ipo siku atakufa je anataka kukumbukwa na watu wa chama chake tu au na TAIFA ZIMA?
 
Asitishe dhamira yake ya kunuia kutaka kuwapunguzia mishahara waliokuwa wafanyakazi wa iliyokuwa TMAA. Kama anapata hisia kuwa wapo "over paid" ni vyema akawapangia majukumu mapya yenye kuendeana na mishahara hiyo ambayo wamekuwa wakiipata kwa miaka mitano iliyopita chini ya utawala wake.

Najaribu tu kufikiria, miongoni mwao wameshachukua mikopo kutoka katika mabenki na taasisi nyingine za kifedha, na walifanya hivyo kwa kuzingatia "debt ratio" ya mishahara yao ya zamani. Je! Endapo makato ya mikopo hiyo yanapobakia kuwa ni yaleyale huku mishahara yao ikipunguzwa, hapo si itakuwa ni sawa na kuwadhoofisha na kuwasambalatisha kabisa kiuchumi?

Sent from my Nokia 2.1 using JamiiForums mobile app
 
Ni vitu gani vinamuangusha Magufuli katika uongozi wake ambavyo kama akiviweka sawa basi anaweza kuwa the best president in East and Central Africa??? Naona kuna malalamiko kadha wa kadha kutoka kwa wananchi wengine wanakubaliana na movement zake wengine wanaona kama anafanya vitu ambavyo si sawa.

kwa maoni yako Endapo ungepewa nafasi ya kumshauri Rais Magufuli ni kitu gani ungependa akifanyie reformation?

Roho ya korosho, kujiona anajua kumbe ni baba jesca
 
Hili zee litufanye chochote linachotaka kutufanya sisi wala hatujali! Tayari limeshabakiza miaka minne!
 
Hahaha sio uongozi, sema utawala wake.
Uongozi sio kazi rahisi.

Halafu huko east na central Africa afanye nini wakati ni mtawala wa Tanzania pekee?!
Swala la mazingira.

Miji inakuwa kila mwaka bila mipango miji.

Nashauri watu wa mipango miji wapewe nguvu zaidi ya kisheria ya kuzuia ujenzi usiokuwa na vibali vya mipango miji.

Yawepo pia maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya miti tu.

Miji iliyozungukwa na milima basi watu wakatazwe kuweka makazi maeneo ya miinuko badala yake yatengwe kwa ajili ya upandaji wa miti.

Miji mizuri imetokana na uthubutu wa serekali kuelekeza ujenzi ulioruhusiwa.

Maeneo ya wazi ni sehemu ya miji murua.

Viwanja vya michezo ni uwekezaji kwenye afya za wananchi pia huondoa muda mchafu wa kushinda bar huku uchumi wa familia na afya ukiwa hatarini.
 
Mimi ningemuomba atafakari vile ana iendesha serikali mim naona kama hayupo sawa japo anabadilika ila bado anahitaji kubadilika zaidi.

Taifa linaongozwa kwa misingi ya utawala bora na umuhimu kufuwata sheria. Kufuta sherehe za kitaifa na mambo yanafanana kama hayo sio ubunifu ila nidalili mbaya kwa mtawala asie heshimu katiba je ufanye mambo yote haya ukose point ya utawala bora?

Pili ukali wako unafanya watu wako wawaumize wananchi na madhara yake hutoyaona sasa ila utayaona utakapo toka kwenye kiti utashuhudia utitiri wa kesi za watu kuvunjiwa haki zao how could ye feel Mr President?
 
Mbili, arudie andiko lake la PhD, hatutaki vyeti fake sisi
Tuhuma hizi kwa rais wa nchi sio nzuri. Kwa vile zimerudiwa mara nyingi hapa jukwaani, ingefaa mamlaka zinazohusika, eg university aliyosoma au maprof waliomsimamia, zijitokeze na kutoa ukweli wa jambo hili. Uongo usipokanushwa, wengi wataamini ni ukweli. Pia nafikiri ni haki ya wananchi ambao ndio waajiri wake kujua taarifa zake zote. Wakati wa kampe huko America, Obama alilazimika kutafuta nakala ya cheti chake cha kuzaliwa kuthibitisha uraia wake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom