Watu wanauliza kwa sababu hawajui, wanataka majibu.
Kama wewe ambae hukujua kitu hicho unachotaka kifanyike kipo kwa miaka mingi sana sasa.
Hakuna binaadam ajuae kila kitu na aulizae ataka kujuwa.
Kuuliza si ujinga.
Kweli
Kuna issue nyingine.
Utaratibu wa viongozi na watendaji wa serikali kuwa na magari kwa matumizi yao ya kazi.
Nchini Rwanda niliwahi kuambiwa kuwa ni raisi, spika na jaji mkuu peke yao wanakuwa na madereva wa kuwaendesha na wakitumia gari ambazo zimegharamiwa na serikali kwa 100%
Wengine wote hawapewi madereva, na japo sina uhakika kama ni wengine wote lakini viongozi na watendaji wengine wa serikali hawatumii magari yaliyogharamiwa na serikali kwa 100%
Kinachofanyika ni kwamba kwa wanaostahili serikali inachangia 50% na mtimiaji 50%. Hivyo serikali inatoa list ya magari na wauzaji wake wanaotambulika na mhusika anachagua analotaka. Then serikali inalipia 50% na mtumiaji analipia 50%. Hii inamaanisha kwamba mtu atatumia gari ya gharama anayojua kuwa anaweza kulipia 50% kuinunua.
Lakini pia suala la mafuta, serikali ina filling stations zake ambapo kila mtendaji wa serikali anayestahili anaruhusiwa kujaza mafuta kiasi fulani ambayo yamelipiwa na serikali. Akizidisha matumizi analazimika kulipia kwa fedha zake.
Najua Tz ni nchi kubwa kwa kuilinganisha na Rwanda. Hata hivyo naamini serikali ikichukua mfumo huu then pengine ni viongozi na watendaji wasiozidi 10 watakaostahili kupewa dereva.
Ni watendaji wachache sana watakaostahili kupewa magari yaliyolipiwa na serikali kwa 100% .
Kwenye nchi kadhaa zilizoendelea taasisi za serikali zina magari lakini hazina madereva. Mtendaji anayetaka kutumia gari kwa shughuli za kiofisi anatakiwa aendeshe mwenyewe.
Namini serikali ya Magufuli itakuwa na mpango wa kuangalia upya sekta ya magari ya serikali na gharama zake.