Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
sisi wakulima wa mpunga tarafa ya pawaga tunalipishwa maji ya umwagiliaji shs elfu 10 kwa heka wakati hatuna huduma ya miondombinu ya mifereji zaidi ya kujitegemea sisi wenyewe. na mpango huo aliuleta lowasa akiwa waziri wa maji. na kuna michango ya kila aina na kila kijiji ambayo haisomwi vijiji vya tarafa hiyo ni mlowa nyuli luganga ilolo itununtu kimande kisanga mkombilenga mboliboli makuka mkumbwaji na hayo malipo ya maji yanaenda wapi?
 
Umelazimishwa kunijibu? au alimradi tu ufikishe idadi ya post za kulipwa?

Ukiwa puuzi, na maskini wa fikra na hali kama wewe utatumika na utafikiru wote wako kama wewe...

Mharakati ni msomi wa siasa na historia na mfanyabiashara wa Kati anayejielewa na mwenye mipango thabiti ya kukuza upeo wake na biashara zake.
Wewe kama unaonsha Wazee ulaya, kama uko Shule bado, kama unafikiria utamaliza Shule uje kuajiriwa, kama ni mission town kijiweni uliyefikiri lowassa akiingia na syndicate yake maisha yatafunguka shauri zako...watu tunasonga mbele na kazi.
 
Sometimes Faizafoxy huwa akiacha mapepe yake, hutoa hoja za maana.

Lakini once akiamua kutetea CCM, akili yake huiweka ndani ya kiroba!!
 
Wenye malori ya kubeba mizigo ya transit na tankers walipe ushuru/ada kila wanapopita mizani iwe point moja hasa wanapotoka dar hii itaipatia serikali pesa za kutosha kuikarabati reli na kunusuru barabara zetu
 
Salaam kwako rais wangu ni miaka mingi tumekuwa tukishuhudia viongozi wakirithishana matatizo lakini kwa bahati nzuri kipindi chote hicho watanzania walikua hawaja amka.

Lakini kwa awamu hii ya aliyekukabidhi kijiti watanzania wameamka sana na kibaya zaidi matatizo yamerundikana zaidi ushauri wangu kwako ni bora sasa kila mtu na abebe mzigo wake mwenyewe.

Ni vema sasa ukaweka mambo yote maovu adharani ili kuepuka kubeba zambi za wengine na watanzania watakuhoji kwa kile tu ulichokifanya mwenyewe la sivyo utajikuta uongozi wako ukionekana mbovu kwa sababu ya makandokando ya miaka kumi iliopita .

Tunajua wewe ni msafi tusingependa kusikia unachafuka kupitia wengine na kibaya zaidi ukichafuka kupitia hao jua huwezi safishika tena.

Nakutakia kazi njema na Mungu akuongoze.
 
mgogoro wa Zanzibar hauitaji kutafuta wasuluiishi, kinajoitajika hapo ni kuamua iliyo kweli na kweli ni kwamba,kura ziendelee kuesabiwa atakaeshinda akabidhiwe nchi. hapo ndipo tutaona ukweli wa Pombe
 
Nitapitia
Then nione kwa nini kwa mfano watu walikuwa wanauliza maswali juu ya bomba la gesi kama kila kitu kipo wazi.

Watu wanauliza kwa sababu hawajui, wanataka majibu.

Kama wewe ambae hukujua kitu hicho unachotaka kifanyike kipo kwa miaka mingi sana sasa.

Hakuna binaadam ajuae kila kitu na aulizae ataka kujuwa.

Kuuliza si ujinga.
 
Napendekeza Yafuatayo,
1. Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Umepitiliza Mpaka Unapotosha Wananchi, Wabanwe Watoe Taharifa Sahihi, Pia Atakayegundulika Kupotosha Apewe Adhabu Kali,
2. Alete Umoja Wa Kitaifa, Ikiwezekana Afute Taasis Zenye Harufu Ya Ukabila Au Vyama Vya Siasa Vyenye Haiba Hiyo
3. Asiteue Watu Kuwapa Nafasi Kama Fadhila Kwa Kuwa Walimsaidia Kampen, Bali Aangalie Uwezo Wao,
4. Aangalie Upya Mtaala Wa Elimu Yetu Maana Imeshuka Hadhi, Si Lazima Kuwa Na Vyuo Vikuu Vingi Bali Vichache Vyenye Tija
5. Atumie Mamlaka Alopewa Na Katika Ya Kuwaweka Kizuizini Watu Wanaoleta Vurugu Na Kuwapotosha Wengi, Hasa Wanasiasa,
6. Katika Mpya Inahitajika Wakati Huu Kuliko Wakati Wowote Ule,
7. Kuwafilisi Wote Waliohujumu Uchumi Pia Iwepo Toleo Jipya La Azimio La Arusha,
 

Safi kabisa!
 
Watu wanauliza kwa sababu hawajui, wanataka majibu.

Kama wewe ambae hukujua kitu hicho unachotaka kifanyike kipo kwa miaka mingi sana sasa.

Hakuna binaadam ajuae kila kitu na aulizae ataka kujuwa.

Kuuliza si ujinga.

Kweli

Kuna issue nyingine.

Utaratibu wa viongozi na watendaji wa serikali kuwa na magari kwa matumizi yao ya kazi.

Nchini Rwanda niliwahi kuambiwa kuwa ni raisi, spika na jaji mkuu peke yao wanakuwa na madereva wa kuwaendesha na wakitumia gari ambazo zimegharamiwa na serikali kwa 100%

Wengine wote hawapewi madereva, na japo sina uhakika kama ni wengine wote lakini viongozi na watendaji wengine wa serikali hawatumii magari yaliyogharamiwa na serikali kwa 100%
Kinachofanyika ni kwamba kwa wanaostahili serikali inachangia 50% na mtimiaji 50%. Hivyo serikali inatoa list ya magari na wauzaji wake wanaotambulika na mhusika anachagua analotaka. Then serikali inalipia 50% na mtumiaji analipia 50%. Hii inamaanisha kwamba mtu atatumia gari ya gharama anayojua kuwa anaweza kulipia 50% kuinunua.
Lakini pia suala la mafuta, serikali ina filling stations zake ambapo kila mtendaji wa serikali anayestahili anaruhusiwa kujaza mafuta kiasi fulani ambayo yamelipiwa na serikali. Akizidisha matumizi analazimika kulipia kwa fedha zake.

Najua Tz ni nchi kubwa kwa kuilinganisha na Rwanda. Hata hivyo naamini serikali ikichukua mfumo huu then pengine ni viongozi na watendaji wasiozidi 10 watakaostahili kupewa dereva.
Ni watendaji wachache sana watakaostahili kupewa magari yaliyolipiwa na serikali kwa 100% .

Kwenye nchi kadhaa zilizoendelea taasisi za serikali zina magari lakini hazina madereva. Mtendaji anayetaka kutumia gari kwa shughuli za kiofisi anatakiwa aendeshe mwenyewe.

Namini serikali ya Magufuli itakuwa na mpango wa kuangalia upya sekta ya magari ya serikali na gharama zake.
 

Mawaziri kutokuwa madereva mimi siafikiani na hilo. Waziri akiendeshwa anawezza kuwa productive hata ndani ya gari, akawasiliana na kufanya mambo mengi zaidi.

Binafsi nnaendessha lakini nimeweka dereva na wakati nipo hata barabarani nnaweza kuwasiliana na kufanya mengi ambayo yanafaida zaidi ya nikiwa nnaendesha mwenyewe. Siku hizi ofisi popote.
 
miongoni mwa sera ya ukawa ilikuwepo sera ya kujenga nyumba za mikopo kwa kuwajengea wananchi wenye nyumba mbovu mijini na vijijini na kisha kuwakopesha wenye nyumba hizo kwa bei nafuu zaidi maana kutakuwa hakuna gharama za kupima kiwanja.
 
kwa nini umetoa mawazo yangu kuhusu kumwambia Makufuli kuiga sera ya UKAWA kuhusu nyumba?
 
Mh. Magufuli, kama unataka kufanikiwa kujua madudu yaliko katika Taasisi na mashirika ya umma nchini,lenga kukutana na watumishi wa ngazi za chini na sio vibosile tu na utoe fursa kwa kila mtumishi kuandika kikaratasi cha matatizo yaliyoko katika Taasisi husika bila kuweka jina lake na kisha karatasi hizo zikafanyiwe kazi na tuhuma/matatizo yatakayokuwa yamejitokeza yachunguzwe na hatua zichukuliwe kwa watakaobainika kuwa wazembe na kusababisha mateso kwa wafanyakazi au ubadhirifu n.k.


Mh. Rais,Watumishi wa ngazi za chini ndio wanaoweza kukueleza ukweli na si vigogo au watumishi wandamizi katika Idara,Wizara na Taasisi mbalimbali za umma.

Tunaomba juhudi hizi zisiwe za muda tu bali zidume kwa miaka yote 5.

Pia ili kuwatendea haki wakurugenzi, hakikisha bajaeti wanazaomba na kutengewa wanazipata kwa wakati na zinazotosheleza mahitaji yao ili kama ni uzembe basi uwe ni uzembe wao wenyewe wa kushindwa kusimamia utekelezaji wa mipango waliojiwekea.
 
Huo ni ukweli na ushauri mzuri pia nashauri awe akipanga mwenyewe ni lini na kero gani anataka kwenda kuishughulikia, ili kuepuka wapambe kumharibia kwa kuwatonya walengwa mapema
 

Nakupa LIKE kwa maneno mkuu. Na huo ndiyo ukweli
 
Nakupa LIKE kwa maneno mkuu. Na huo ndiyo ukweli

Watu hawapindishwi vyeo,hela za matibabu mfanyakazi wa chini mpaka anyenyekee na madudu mengine mengi ili hali vibosile kila siku safari na vikao.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…