Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Mwenge hauna tija kwa maendeleo ya Taifa letu.

Mwenge ni kichocheo cha ngono, ambayo matokeo yake ni mimba za utotoni na maambukizi ya magonjwa ya zinaa sehemu mwenge unapokesha.

Kwenye mikesha ya Mwenge ulevi wa bangi na pombe haramu huhalalishwa.

Kwenye mikesha ya Mwenge matukio ya ubakaji na ulawiti ni kitu cha kawaida kabisa.

Mwenge Una gharama nyingi kuliko thamani ya miradi inayozinduliwa.

Miradi yenyewe ni aibu hata kuielezea, eti mbio za Mwenge zimezindua choo.

Gharama za mbio za Mwenge zielekezwe Kwenye huduma nyingine za kijamii na miradi ya maendeleo.

Zindiko la kina Forojo Ganze halina nafasi tena kwa Taifa letu.
 
Nasema hivyo kwa kuwa mimi ni mpangaji ktk nyumba za ubia wa Nhc na wawekezaji, nalipia $ kila mwezi kwa ajili ya huduma zifuatazo, maji taka-dawasco; umeme wa komoni eriazi (common areas); walinzi wa kitanzania wasio hata na bunduki na wafanya usafi wa kitanzania wanaotumia maji ninayolipia kupiga deki huku wakitumia mifagio inayotengenezwa tanzania.
Wakati huo huo mimi mwenyewe nalisha luku yangu kwa fedha za kitanzania ktk nyumba hiyo hiyo. Mbaya ni kuwa Bili za nyumba yetu (ushaidi tunao) zote nilizozitaja hapo juu zinalipwa kwa pesa ya kitanzania yaani shilingi. Na mimi mpangaji ninalipa pango Nhc kwa fedha ya kitanzania pia. Tafadhali rais uliangalie sana swala la matumizi haya holela ya fedha yetu ya kigeni tuliyoichuma.
 
Mkuu Unasali kwa Gwajima au unakijiwe cha Gahawa hapo Kariakoo??
 
Yeye mwenyewe ni mwenge sasa atapigaje marufuku! ...kwani hukuona ile logo ya kampeini yenye nembo ya mwenge kwenye 'M'!?
 

Hiyo sasa ndoto..kuna bango l Magufuli ambalo halina mwenge?
 
Atafuta mambo mengine mengi lakini ubavu wa kufuta mwenge hana.
 
sio mwenge tuu, hata zile siku, sijui sikunya maji, siku ya maziwa , siku ya nyama, siku ya ,,,,, utaratibu ubadilike badala ya hizo bonanza za siku kugharamiwa na serikali waachiwe private sector wawe wanaandaa na kugharamia hizo siku na iwe fursa kwao kutangaza na biashara za bidhaa zao kama ni maziwa , maji nk. Pesa za serikali zitumike kwenye mambo tangible kama kutandaza mabomba ya maji safi na salama na kuongeza vyanzo vya maji safi badala ya kugharamia bonanza. MAGUFULI OYEEE

 
Nagufuli una kazi kubwa sana baba kila mtu anakulilia shida
 
Ila jamani kusema ukweli tuweke uchama pembeni. Mwenge hauna faida yoyote ya kuzunguka nao Tanzania nzima zaidi ya kumaliza fedha nyingi za umma bila sababu ya msingi. Hizi mbio za mwenge nazo zifutwa pesa nyingi tutaokoa ambazo zitakwenda kufanya mambo mengine katika jamii. Ila nadiriki kusema Magufuli hana jeuri hiyo ya kuufutilia mbali mwenge sababu maudhui yake yamekaa ki ccm hivyo ni ngumu kusaliti chama chake kwa maslahi ya Nchi.
 
Mwenge ni moja ya nembo ya taifa,, sasa unataka afute nembo ya taifa wananchi watamuelewaje??
 
Mwenge ni maagano ya nchi tena unaongeza umaskini nchini. Sasa wakiuondoa ccm watabaki kweli salama? kamwe hawawezi kuuondoa
 
Mwenge ni moja ya nembo ya taifa,, sasa unataka afute nembo ya taifa wananchi watamuelewaje??
Hajasema afute Nembo amesema zifutwe mbio za Mwenge, hata Ngao ni Nembo ya
Taifa lakini hakuna mbio za ngao, zimebaki tu maofisini hivyo ikiwezekana kila mkoa
na kila Wilaya kuwe na mwenge utakaokaa ofisi ya Mkuu wa Wilaya N.k
 
Kama uwaziri wao ulikoma ulipoapishwa,lakin Mashine za mhimbili ziliacha kufanya kazi zaidi ya miezi miwili.Ndani ya siku tango tangu uapishwe umekuta tatizo hilo maana take mawaziri Zhao hawafai.Ukiwapa kazi yoyote tutaelewa salsa kuwa tatizo la CCM ni mfumo.
 
zindiko la kina forojo ganze halina nafasi tena kwa taifa letu.

Nafikiri mwenge original umeibiwa, kupotea au kuuzwa maana nasikia ulikuwa
wa dhahabu halafu ulikuwa na uwezo wa kumulika wezi sasa huu wa leo ambao
umeshindwa kuwamulika wezi wa kura zanzibar na majimboni utakuwa feki tu
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…