Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Nawasalimu wanajamvi.

Serikali inapaswa kuingilia kati suala la tozo iliyoanzishwa na Tume ya vyuo vikuu nchini, kiasi cha Tsh 20,000/= kwa kila mwanafunzi nchini. TCU imeanzisha tozo hili kwa wanafunzi Wa vyuo vikuu kinyume na regulation ya 14 (1) (d) ya "Universities (General) Regulations, G.N.No.226" ya mwaka 2013 ambayo inakitaka chuo kilipie "prescribed annual commission fee" kwa kila mwanafunzi aliyedahiliwa kwenye chuo husika. Jambo hili limepelekea wanafunzi kutoendelea kujisajili katika vyuo vikuu vingi nchini kwasababu tozo la TCU Tsh 20,000/= kwa kila mwanafunzi limeanzishwa bila kufuata utaratibu Wa kisheria. Pia sheria ambayo TCU wameitumia, wameitafsiri vibaya kwa kuwataka wanafunzi walipe tozo hilo na isiwe chuo kama utaratibu ulivyokuwa kipindi cha nyuma.


Pia wanasheria tuwasaidie wanafunzi wanaoonewa nchini kwa kulazimishwa kulipa tozo hilo. Tusome "Regulation" ambayo TCU wameitumia katika Public Notice yao kupitia website yao www.tcu.go.tz ili tuwasaidie wanafunzi na hata baadhi ya uongozi wa vyuo kupata tafsiri sahihi ya nani anapaswa kulipia hiyo pesa. Pia Mhe. Rais JPM, suala hili linagusa tabaka ambalo ulikuwa unalilia sana liweze kutimiza ndoto zao za kielimu lakini usajili umeshasimama katika vyuo vingi nchini kwasababu wanafunzi wamekataa kulipa tozo hilo; ni wakati sasa, baada ya kulijua hili, pamoja na viongozi wengine MULITOLEE MAAMUZI, VIJANA TULIOWATUMA WAKASOME WANATESEKA MNO NA HILI SUALA. Kwani kwa namna nyingine lilipaswa kufahamiawa na bodi ya mikopo ili kiasi kitoke board halafu wanafunzi walipie, unfortunately haipo hivyo.


Serikali iingilie kati jambo hili ili lisije likasababisha mgogoro kati ya wanafunzi na uongozi Wa vyuo kuwa mkubwa nchini.
 
Nawasalimu wanajamvi.

Serikali inapaswa kuingilia kati suala la tozo iliyoanzishwa na Tume ya vyuo vikuu nchini, kiasi cha Tsh 20,000/= kwa kila mwanafunzi nchini. TCU imeanzisha tozo hili kwa wanafunzi Wa vyuo vikuu kinyume na regulation ya 14 (1) (d) ya "Universities (General) Regulations, G.N.No.226" ya mwaka 2013 ambayo inakitaka chuo kilipie "prescribed annual commission fee" kwa kila mwanafunzi aliyedahiliwa kwenye chuo husika. Jambo hili limepelekea wanafunzi kutoendelea kujisajili katika vyuo vikuu vingi nchini kwasababu tozo la TCU Tsh 20,000/= kwa kila mwanafunzi limeanzishwa bila kufuata utaratibu Wa kisheria. Pia sheria ambayo TCU wameitumia, wameitafsiri vibaya kwa kuwataka wanafunzi walipe tozo hilo na isiwe chuo kama utaratibu ulivyokuwa kipindi cha nyuma.


Pia wanasheria tuwasaidie wanafunzi wanaoonewa nchini kwa kulazimishwa kulipa tozo hilo. Tusome "Regulation" ambayo TCU wameitumia katika Public Notice yao kupitia website yao Home - Tanzania Commission for Universities ili tuwasaidie wanafunzi na hata baadhi ya uongozi wa vyuo kupata tafsiri sahihi ya nani anapaswa kulipia hiyo pesa. Pia Mhe. Rais JPM, suala hili linagusa tabaka ambalo ulikuwa unalilia sana liweze kutimiza ndoto zao za kielimu lakini usajili umeshasimama katika vyuo vingi nchini kwasababu wanafunzi wamekataa kulipa tozo hilo; ni wakati sasa, baada ya kulijua hili, pamoja na viongozi wengine MULITOLEE MAAMUZI, VIJANA TULIOWATUMA WAKASOME WANATESEKA MNO NA HILI SUALA. Kwani kwa namna nyingine lilipaswa kufahamiawa na bodi ya mikopo ili kiasi kitoke board halafu wanafunzi walipie, unfortunately haipo hivyo.


Serikali iingilie kati jambo hili ili lisije likasababisha mgogoro kati ya wanafunzi na uongozi Wa vyuo kuwa mkubwa nchini.
 
Mh. Rais ahakikishe yafuatayo
1. Wananchi wanakuwa na uwezo wa kupata milo 3 kwa siku
2. Wananchi wanapata maji safi na salama kwa gharama nafuu na kwa wakati. Akisikiliza vipindi vy mama lowasa atapata kujua kwa undani ataweza kuwasaidia sana akina mama.
2. Huduma ya afya bora na kwa gharama nafuu
3.Elimu bora kulingana na uhitaji wa taifa. Ilani ya CDM itamsaidia sana hapa
4. Ardhi. Wananchi wamilkishwe ardhi. Pia ajitahidi kuondoa migogoro ya ardhi na kushughulikia fidia za wananchi ambao wana zaidi ya miaka 10 hawajalipwa.
5. Ajira ya kuajiriwa na kujiajiri. Tatizo ni mitaji hivyo tunaomba uangalie
6.Nchi kutumia tafiti katika maendeleo
 
1.Kuwe na tarehe maalumu ya kupata mshahara nchi nzima isiwe mara tarehe 19, 23, 27, 25 hii itasaidia kupanga bajeti kwa wakati.

2.Stahiki mbalimbali za watumishi zilipwe kwa wakati.

3.Tenga siku maalumu ya kutoa maelekezo kwa watumishi nchi nzima.
 
Kwanza watulipe madai yetu ,maana wao wanalipa walimu tu kana kwamba hakuna watumishi wengine ,this is very sad !!
 
Cha ajabu sasa ,madiwani na wabunge haki zao zinalipwa haraka ,wakurugenzi makatibu na maafisa waandamizi chao mfukoni
 
Watumishi wengine ni shiiiidah ,wakurugenzi waliowaweka mawilayani nao hawajali haki za watumishi kabisa ,ni wabinafsi
 
Aamue mkurugenzi asiyelipa haki za watumishi piga chini ,haingii akilini likizo,transfer ilipe hazina ded unafanya nini
 
Kwanza watulipe madai yetu ,maana wao wanalipa walimu tu kana kwamba hakuna watumishi wengine ,this is very sad !!
mshaanza kulalamika mara hii? hamkujua hii ni ile ile, wale wale, zile zile,yale yale!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Katiba yetu inampa Rais wa nchi mamlaka ya kuteua wabunge 10 na hata kuwateua kushika nafasi ya uwaziri na unaibu waziri. Pia katiba hiyo hiyo haimzuii Rais wa nchi kufanya uteuzi nje ya Chama chake na ndiyo sababu Rais aliyepita aliwahi kumteua James Mbatia kuwa mbunge.

Hivyo,kwa mantiki hiyo hapo juu ninamshauri Rais Magufuli amteue Prof Ibrahim H. Lipumba kuwa mbunge na kisha amteue kuwa waziri wa uchumi katika serikali yake ya awamu ya tano. Binafsi ninaamini prof Lipumba atasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua na kuimarisha uchumi wa taifa letu kutokana na uwezo wake mkubwa katika masuala ya kiuchumi alionao kitaifa na kimataifa.

Ninauhakika Rais utaufanyia kazi ushauri huu kwani una tija kwa taifa letu. Pia ninaamini Rais wetu ataweza kumteua prof. Lipumba kuwa waziri wa uchumi kwani alituahidi katika kampeni zake kuwa atashirikiana na wapinzani katika kuongoza nchi na kufikia mabadiliko ya kweli ya kiuchumi. Mungu ibariki Tanzania! Mungu mbariki Rais Magufuli!
 
John Pombe Magufuli fanya hivi uifurahishe nafsi yangu!

1.kwanza nianze kwa kukwambia kua wananchi wengi both wa Ccm na Ukawa wana imani sana na wewe hasa utendaji wako hivyo usiwaangushe.

2.Usije ukathubutu kutoa vyeo vya ahsante,undugu,kujuana wala upendeleo kabisa!! Kwa miaka mingi viongozi wetu wamekuwa wakijisahau na kujikuta wakitoa vyeo au nafasi kwa kubebana sana!
Nakuomba usilipe fadhira kamwe,hata kama mtu alikuwa mstari wa mbele wakati wa kampeni yako hilo lilikuwa jukumu lake wala usimpe nafasi ya ahsante.

2.Usisikilize zaidi maoni na mawazo ya wapambe njaa,ni ngumu sana kukweleza hali halisi kwa kuogopa kukuudhi na kuharibu kazi zao! Tafuta namna ya kupata habari za uhakika kutoka kwa wananchi kwa njia unazoweza wewe.

3.Tuchagulie waziri mkuu asiye na tuhuma wala kashfa yoyote na awe mchapakazi sana hata kama atakuzid uchapakazi usione wivu kwa sababu tunajenga nchi moja,pia jihadhari asiwe mtu wa makundi wala siasa majitaka.

4.Chukua hatua palepale tatizo linapotokea achana na maisha ya kuunda tume huku ikitumia kodi za wananchi,tuna vijana wa usalama wa taifa,watume linapotokea tatzo naamini watakuletea majibu ya kweli na uhakika na chukua hatua hapohapo na kuwawajibisha wahusika.

5.Kuwa raisi wa watanzania wote bila kubagua itikadi za vyama vyao! Usipeleke maendeleo makubwa kwenu pekee kama baadhi ya viongozi waliopita na wala usipeleke maendeleo kwa sisi wanaccm ukwasahau wenzetu!

6.Simamia uwajibikaji wa watumishi ili kuongeza ufanisi makazini.

7.Pitia mikataba yote ya rasimilami zetu na angalia ile inayoweza kuvunjwa na kuwekwa upya kwa misingi ya sheria ivunjwe na wale wawekezaji wanaokwepa au kupewa misamaha ya kodi ondoa hiyo misamaha ili kuongeza kipato cha nchi.

8.Angalia namna itakayoweza kuongeza nafasi za ajira hasa kwa vijana sijui utafufua viwanda au la! Ila tungependa kuona ajira zikiongezeka na hapa naomba mheshimiwa wale wazee waliofikia umri wa kustaf basi wapumzike na kuachia nafasi vijana na sio wakistaf wanateuliwa tena katika nyadhifa zingine mpya! Hapana!! Hili linakwaza wengi liangalie.

9.Simamia ukusanyaji wa mapato ya serikali kwa ukamilifu na matumizi yake pia.

10.Pambana na ufisadi kwa nguvu zako zote kama ulivyotuahidi mheshimiwa!


Ahsante!

Gadyson Baita.
Kijana na kada wa chama cha mapinduzi.
Mchambuzi wa siasa
0676733796
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…