Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Aiseee!!!!!! Wewe ni mtanzania kweli? Na umemaliza elimu kwa mitala ya Tanzania? Na hulijui bomba la Tazama?
Unashauri hilo bomba lipitishwe sehem nyingine sio?
Aisee! Good

Hahaaaaaa, anafikiri la maji kutoka Kigurunyembe
 
Kwanza alipataje hati; na pili alipataje kibali cha ujenzi? Mamlaka iliyotoa hivi vibali (serikali) inapaswa kuwajibika na kulipa gharama zote.
Kisheria ukinunua mali ya wizi hata kama umepewa risiti halali waweza fungwa.vivyo hivyo hilo ghorofa,hata kama lina hati iliotolewa na manispaa lakini kwa kuwa ni kosa kujenga juu ya bomba,basi ni haki yake kuvunjiwa
 
Aiseee!!!!!! Wewe ni mtanzania kweli? Na umemaliza elimu kwa mitala ya Tanzania? Na hulijui bomba la Tazama?
Unashauri hilo bomba lipitishwe sehem nyingine sio?
Aisee! Good

Kwani bomba la TAZAMA linatusaidia nini Watanzania? Hiyo ni mali ya Wazambia. Bora hata hilo ghorofa linasaidia kupendezesha mji wetu na kutufichia aibu ya umasikini na udumavu wa mji wa Morogoro...
 
Angalizo:kama unataka kununua kiwanja kilichopimwa au skwata,ukiondoa viwanja vinavyouzwa kwenye miradi ya kupima viwanja,unashauriwa uende kwa ofisa mipango miji wa manispaa husika,atakueleza kila kitu kuhusiana na eneo unalotaka kununua
 
Mh. Rais, kuna shule za sekondary zinawalimu wengi zaidi ya 80+ na hawana kazi walimu mpaka inafikia walimu wanashare darasa moja ili kuonekana anakipindi wakati kuna shule za kata zinawalimu wawili tu huko vijijini...ushauri wangu punguza watu waende vijijini asieyetaka aache kazi.hapa kazi tu hakuna brahbrah.
 
Me nawashangaa watanzania
kama kuvunjwa livunjwe tuu hakuna namna wakilichepusha huko ndi mnataka wakavunje za maskin
 
Thubutuuuuuu!hao ndio wenye Chama /vitu km hivo ndio vinaitwa maslahi ya Chama
 
Kiukweli hapo busara itumike.

Kama alivyoshauri mdau mmoja hapo juu, apigiwe gharama ya kuhamisha au kuchepusha bomba hilo kwenda upande mwingine. Hapo serikali itakuwa imeondokana na lawama pamoja na hasara kubwa endapo mmiliki ataenda mahakamani kudai fidia.

Busara kubwa itumike kama ilivyotumika kuepusha bomoabomoa ya jengo la Tanesco pale Ubungo.

BACK TANGANYIKA

Good idea,, wampigie tu calculation ya kuchepua hilo bomba la mafuta lipite upande mwingine, kama atamudu hizo gharama ni sawa wasimbomolee alipe in cash kazi ianze...
 
Majipu yatakayotumbuliwa ni wanyonge na watumishi basi majipu mazito Kama ya wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa ndoto

Endelea kuamini hivyo hivyo, umeambiwa serikali ipo, na serikali yenyewe ni ya Jihn Pombe Magufuli. Hata waliotumbumbuliwa hawaamini kilichotokea, maana nao walikuwa wanaishi kwa mazoea
 
12219483_936964903043135_2893456315640555997_n.jpg
lipo morogoro-msanvu

Jamani tusiendelee kupotosha,kilichojengwa juu ya bomba la TAZAMA ni jengo la generator na sehemu ya uzio na ndivyo vinavyotakiwa kuvunjwa.
 
Kwani Hilo bomba kaliziba au lina fanya kazi
Coz inaweza kuke ha kwenye maji meli zikapita chini
 
Hapa common sense itumike. Apigiwe hesabu za kupitisha bomba sehemu nyengine. Hilo jengo linatia sura ya mji na kuweka mazingira mazuri.

Aiseee!!!!!! Wewe ni mtanzania kweli? Na umemaliza elimu kwa mitala ya Tanzania? Na hulijui bomba la Tazama?
Unashauri hilo bomba lipitishwe sehem nyingine sio?
Aisee! Good

Jengo halijajengwa juu ya bomba bali liko ndani ya hifadhi ya bomba la Tazama
 
Tatizo Ni Rushwa, Ufisadi Na Uzembe Wa WATENDAJI Wa HALMSHAURI Na SERIKALI!! Iweje Jengo Kama Hilo Limejengwa Sehemu Isiyo STAHIKI Na Alipewa Vibali Vyote SAHIHI!!! Je WALIOHUSIKA Na Kadhia Hiyo Wamewajibishwa Vp!!!?? Na Yale Yale Ya Maghorofa Ya Dar Yanayoota Kama Uyoga, Yakijengwa Kwa Kuzidisha Idadi Ya Floor TOFAUTI Na Vibali Vyao!! Na MENGINE Yameporomoka Na Kuua Watu!!! Cha Kushangaza Wametoa Vibali KUJENGA Ghorofa Jirani Na Ocean Road Hospital Na Ikulu!! Eti Baada Ya Kukamilika Ndio Viongozi Wakuu Wa Nchi Wanashituka Na KUHOJI!!!!??? Yaani NCHI Vichekesho!!!
 
Kwani bomba la TAZAMA linatusaidia nini Watanzania? Hiyo ni mali ya Wazambia. Bora hata hilo ghorofa linasaidia kupendezesha mji wetu na kutufichia aibu ya umasikini na udumavu wa mji wa Morogoro...

You must be joking, if not, you are missing something very important especially upstairs
 
Hivi hilo bomba la mafuta la TAZAMA lilikuwa linashusha mafuta hapo Morogoro mjini au ndio njia ya kwenda Zambia? Kwa nini kama lilikuwa halishushi mjini walipitishie mjini bomba kama hilo linalokwenda nje ya nchi?
 
Jamani tusiendelee kupotosha,kilichojengwa juu ya bomba la TAZAMA ni jengo la generator na sehemu ya uzio na ndivyo vinavyotakiwa kuvunjwa.

Kaka watu wanaongea tu

Tatizo TBC waliitangaza vibaya kiwa jengo lote linabomolewa.

Lakini ukweli halibomolewi lote bali ni uzio na chumba cha generator ambavyo vimepita ndani ya eneo la hifadhi (na sio juu ya bomba kama wengi wanavyodhani) ya bomba la TAZAMA
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom