Kitty Galore
JF-Expert Member
- May 24, 2011
- 345
- 100
Wananchi tunaona na tunaridhishwa na utendaji wako uliotukuka. Ni muda sasa tumekuwa tukilalamika katika maswala mbalimbali, lakini sasa tuna imani yale yote yaliyokuwa sio utayarekebisha.
Ikumbukwe kidole kimoja hakivunji chawa.
Tunashauri, uunde kitengo cha kupokea maoni na malalamiko ya wananchi ili nia yako njema itekelezeke. Sisi ndio wahanga na ndio tunaokutana na uozo mwingi ndani ya serikali yako, tupo tayari kukupa ushirikiano kwa 100% bila kificho, ila kwa sasa hatumuamini mtu kwa sababu hatukupewa hiyo nafasi kwa uwazi, tulitoa ushirikiano sehemu mbalimbali lakini mwisho wake wengine walipoteza uhai.
Nakuhakikishia muheshimiwa rais, kitengo hiki kitatumbua majipu, vipele hadi chunusi
Asante sana