Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
hapa ipo kazi!
haya majengo yanayouzwa ni chanzo kizuri sana cha mapato!
ARDHI HAPA WANAHUSIKA!
UNAKUTA NYUMBA IMEUZWA MILION 300,KATIKA MAUZIANO WANAANDIKA 90 MILION HIYO NDIYO INAYOLIPIWA!
 
Mmekalia kodi tu, madini waliyogawiwa wazungu hamuyaoni?! Gesi iliyombioni kugawiwa wachina hamuioni?! Utarii?! Nk?! Tunataka kodi ishuke imezidi!! Rasilimali za nchi zifanye kazi!! Tutaendelea kuikwepa tu hata wafanyeje! Mpaka pale itakaposhuka.! Hatuwezi kuwa tunanyonywa huku wengine wakijineemesha.! Rejea mshahara wa rais.!
 
1.jipu la machoni.hili ni la ufumbiaji makusudi wa haki za mtu na hupofusha watoa haki.mahospitalin,polisi,mahakamani.
2.jipu la masikioni,hili ni kwa wote wanaogeuza matokeo ya kura kwa kuiba au kulazimisha ushindi.hili ni kama masikio ya mbuzi mpaka lichemshwe.
3.jipu la kwenye koo,ni rushwa iliokomaa kubwakubwa ya kimataita kama epa,escrow,radar
4.jipu la sehemu za siri.linauma Sana limejificha ni mashirika ya jamii yamulikwe,.mf cwt,nssf,ppf,n.k wastaafu hawalipwi kwa wakati,majengo mazuri wamejenga manufaa kwa mwanachama hakuna.
5.jipu la kwapani ni NGO,hutembea na ofisi kwapani,fedha zikiletwa walengwa hawapati hii ni pamoja na kujinufaisha kwa kuwa na majumba,na magari mazuri,hili nalo lilishaiva kitambo.
Mengine ungezeeni hapo na hatua zichukuliwe yatumbuliwe bila ganzi.
 
Ni miaka mingi tumeomba weeeee! Wapi!
Tunaomba kituo cha mafuta mbele ya soko kuu la mjini Morogoro kibomolewe. Kilijengwa kwa ushujaa wa pesa, enzi zile za kila mwenye uwezo kuvunja sheria. Ujenzi huu uliziba barabara ya mtaa ikitokea night klabu ya kahumba.

Naleta taarifa hii kwa kuamini kabisa kwamba bomoa bomoa hii itahama jangwani na itafika morogoro itusaidie kusafisaha mitaa na sehemu za wazi zilizovamiwa.
 
Dar es Salaam, Tanzania. Rais John Magufuli amemwagiza Waziri wa
Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kikanda na Mambo ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki, Balozi Dk Augustine Mahiga kuanza kushughulikia
mgogoro wa Burundi na ametaka kazi hiyo afanye kwa kushirikiana na
waziri wengine kutoka Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Huu utakuwa mtihani wake wa kwanza kwa Balozi Mahiga ambaye
aliapishwa hivi karibuni kwenye wadhifa huo baada ya kuteuliwa na
Rais kuwa mbunge. Balozi Mahiga aliliambia gazeti moja akisema
kuwa, ameagizwa kushughulikia kiini cha mzozo huo na tayari wakati
wowote alitarajiwa kuwasili Bujumbura kuanza mazungumzo.
Hata hivyo, alitarajiwa kuwasili kwanza mjini Arusha kwa ajili ya
majadiliano na Katibu Mkuu wa EAC, Dk Richard Sezibera na baadaye
kuweka mikakati ya pamoja ya namna ya kushughulikia mzozo huo.
Tanzania ndiye mwenyekiti wa EAC.
Wakati hali ya wasiwasi ikiendelea kujitokeza Burundi, ripoti zinasema
kuwa zaidi ya raia 1O0,000 wamewasili nchini kwa ajili ya kuomba
hifadhi tangu mzozo huo ulipoanza Aprili mwaka huu.
Wakati Tanzania ikianzisha juhudi mpya kuhusiana na mzozo huo,
kuna ripoti kuwa Umoja wa Afrika (AU) umeanza kujadili uwezekano
wa kutumwa jeshi la Afrika Mashariki nchini humo kwa lengo la
kuzima ghasia na machafuko yanayotishia kuitumbukiza nchi hiyo
kwenye vita vya ndani.
Baraza la Usalama na Amani la Umoja wa Afrika limesema hali ya
Burundi ni mbaya na kwamba hatua za dharura zinahitaji kuchukuliwa
ili kuepusha nchi hiyo kutumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa
wenyewe.
Kamishna Mkuu wa baraza hilo, Ismail Chergui ameandika kwenye
ukurasa wake wa Twitter akisema kuwa mauaji nchini Burundi ni
lazima yakomeshwe. Baraza hilo la AU limefanya kikao cha dharura
kujadili kadhia ya Burundi na pendekezo la kutumiwa kikosi maalumu
kinachojulikana kama ‘East Africa Standby Force’ kwa ajili ya kudhibiti
hali ya mambo katika nchi hiyo limetolewa. Kikosi hicho kiliundwa
mwaka 2003 na kinajumuisha nchi za Kenya, Burundi, Comoros,
Djibouti, Ethiopia, Rwanda, Ushelisheli, Somalia, Sudan na Uganda.
Huku hayo yakijiri, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja
wa Mataifa amewalaumu viongozi wa Burundi kwa kuchochea ghasia
na machafuko nchini humo na kulitaka Baraza la Usalama la umoja
huo kuwawekea vikwazo vya usafiri viongozi kama njia moja ya
kuwashinikiza wakomeshe ghasia hizo.


CHANZO: Gazeti La Mwananchi


NOTE:
SAWA! ILA ZANZIBAR MBONA UMEWAPA KISOGO? AU YAMEKUSHINDA MH.???
 
dunia hii maajabu kweli hayataisha,unasuluhisha mahirani nyumbani kwako hakuna amani
 
dunia hii maajabu kweli hayataisha,unasuluhisha mahirani nyumbani kwako hakuna amani
Zanzibar hakuna mgogoro, kwani uchaguzi umeshafanyika? Subirini uchaguzi muone kama swala la Zanzibar litamsumbua JPM huyu ndie rais atakayewanyoosha wote waliokuwa wanafaidi pesa za walipa kodi bila kunawa mikono.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom