Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli

Status
Not open for further replies.
Wewe ni Bashite mwingine, alafu nyie watoto wa Lumumba FC mnafikiri ni rahisi kiasi hicho nchi kuongozwa na mtu ambae hata kuandika huwezi?
 
Mh Magufuli kwanza kabisa nakupa pole kwa shughuli unazozifanya kila siku. Pili ningependa sana kukupongeza kwa kazi ya kusafisha josho liliojaa kupe. Najua kabisa hao kupe walijazwa na chama chako kilichokuweka madarakani, lakini usiwe na wasiwasi watanzania watakusamehe tu kama utawasaidia kulisafisha hilo josho.

Nyerere alitumia kauli hii wakati wa kutuletea Azimio la Arusha, tumenyonywa kiasi cha kutosha na tumedhulumiwa kiasi cha kutosha sasa tunataka kuondoa unyonyaji na kujenga ujamaa. Na sisi kizazi baada ya Nyerere tunasema walio madarakani na rafiki zao walitunyonya kiasi cha kutosha na sasa tunataka kuondokana na huo unyonyaji. Hivyo tunatiwa hamasa pale tunakuona mheshimiwa rais ukitolea maamuzi mazito ya kamati unazoziunda tofauti na huko nyuma ambapo tulijua "business as usual".

Ulipoteua hii kamati wengi walikubeza wakiamini kuwa itakua business as usual, lakini mimi binafsi nilikupatia nafasi ya 50% kama ungekuja na maamuzi mazuri na 50% niliachia business as usual. Leo tumeona wenyewe hata wale waliokuponda leo wamekupongeza japo sina imani kama pongezi zimetoka mioyoni mwao Mungu pekee analijua hilo. Lakini kwetu hizo pongezi ziwe za kinafiki ama la ni vizuri kuona kama pande mbili za wanasiasa kwa mara ya kwanza zimekuunga mkono.

Baada ya sifa hizo hapo juu, nina maombi makubwa mawili kwako Mheshimiwa Rais:

1: Usafishaji wa bwawa: Hili Bwawa bado lina mamba wengi sana, ikibidi hao wanaosafishwa basi wanatakiwa walipe kwa yale makosa waliyoyafanya ili wengine watakaowafuata wasiguswe na huo uchafu. Hili bwawa lina mamba walifugwa na wakazaana kwa kupitia chama chako ukipendacho cha CCM kwa miaka mingi tangu Muanzilishi wenu aachie ngazi. na mamba wengine wakahamia kwa majirani zenu wa upinzani. Najua itakua kazi kubwa lakini usikate tamaa sababu watanzania kidogo kidogo wameanza kulielewa lengo lako. waliokutangulia waliunda kamati ambazo ziliongeza shibe kwa wateule hazikuwa na maana yoyote(Warioba,Richmond,Escrow,EPA) lakini leo umetuonyesha kua ulipanga kutufikisha katika nchi ya ahadi.

2: Bwawa likiwa safi linahitaji sheria za maana na siyo zilizopitwa na wakati. Hivyo Ombi langu kubwa kwako ni kuhakikisha unatuletea katiba mpya kabla hujamaliza muda wako. Ninajua kabisa mwaka 2020 watanzania watakurudisha Magogoni maana katiba yetu inakupatia nafasi kubwa sana ya kurudi magogoni. Ukirudi magogoni mwaka 2020 basi kazi yako kubwa iwe tu ya kutuletea Katiba mpya yenye maslahi mapana kwa watanzania wote hata sisi tusiokua na vyama ama wale wapinzani. Kwakuwepo katiba mpya yenye maslahi ya wengi na yenye kufuata haki za binadamu katika ulimwengu wa karne ya 21 tutategemea kuwapata viongozi wasafi wasiokuwa na makandokando wawe kutoka upinzani ama chama chako.

Nyerere alituachia katiba isiyokamili lakini tutamkumbuka sana kwa kutuachia katiba iliyoweka ukomo wa urais na kiukweli wewe mwenyewe utaniunga mkono kama asingefanya hivyo labda kuna wengine wangefia magogoni kama Mugabe na kukunyima nafasi hiyo ulinayo sasa.

Ili uwekwe katika kumbukumbu na wazee wetu waliopigania uhuru wetu kama kina Chief Mkwawa wa wabena, Mangi Meri wa uchaga, Nyerere,Sykes, mzee Dosi, na wengine wengi basi utupatie KATIBA MPYA inayoendana na dunia ya sasa na siyo hii ya chama kimoja.

Kwa ndugu zangu Watanzania ombi langu ni kwamba rais wetu ana nia nzuri na nchi hii tunatakiwa tumpatie muda nina imani naye japo mara nyingi hua nakwazika ninapoona anavurunda haki za raiImani yangu kubwa ni kwamba Tanzania njema inakuja na sisi hapa JF tusiache kumchana pale anapokosea na kumpongeza pale anapofanya vizuri.

Mungu Ibariki Tanzania
Mungu Ibariki Africa
 
Kwanza napongeza kazi nzuri sana unayofanya.
Sikubalian na wewe katika mambo fulani lakini katika kutetea maslahi ya nchi hapa niko tayari kufa.
Mkuu,kuna watu wachache ambao wanataka kuturudisha nyuma,Wana woga ambao mkoloni alitupandikiza,kuwa mtu mweupe ni wa kumwogopa,sasa ni wakati wetu kusimama wima.
Nimesoma Nje ya nchi dharau tunazozipata waafrica kwa ujumla hakuna tena.Huu ni wakati kusimama wima na kutumia rasilimali zetu kujiendesha wenyewe.
Napenda kukushauri kuwa itakuwa jambo jema mikataba ya madini,utalii,gesi ikawa wazi na kurudiwa tena upya.
Na kuweka sheria kali juu ya wahujumy uchumi wa nchi hii ikiwa na adhabu kifo.
pili,kubadili katiba hata maraisi washtakiwe. Suala la madini ni utitiri wa viongoI wengi ambao wanastahili kuwa chini ya ulinzi muda huu.
Tatu,elimisha na kubadili mfumo wa elimu ambao tulionao ni mbovu,unaotufanya kuwa wavivu wa kufikiria na watumwa.Hii inatokana na kile mkoloni alitaka nini kwtu na alifanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Ukifanya hayo utakuwa umeiweka nchi pahala salama for the next generation.

mwisho,ushauri wangu kwa watanzania wote.Inatupasa kusimama kwa pamoja juu ya maslahi mapana ya nchi yetu. Umaskini tunajitakia sisi wenyewe.
 
Mheshimiwa Rais wangu, kiukweli mi naona pale unapo toa tamko fulani kuhusu serikali, viongozi wako wanafata kile ulicho sisitizia. Mfano, uliosema stand huko igunga itumike, tayari imeanza kutumika. Uliposema, watumishi hewa watolewe, kila kiongozi alitekeleza agizo hilo. Vile vile, bila kusahau la serikali kuhamia dodoma, baadhi ya wizara walikaa vikao ili wahamie dodoma hata kabla ya hiyo miaka minne uliyo sema. Sasa Mheshimiwa, naomba pia utamke kuhusu watumishi wanao tumia vyeti feki na digriii za kununua makazini, pia wamechangia kufikisha nchi ilipo kuwa imefikia.
Angewatoa na wanasiasa waliopata kura za kununua
 
Ndugu wanajukwaa. Ninayo heshima kwenu kuanzisha uzi huu maalum kwa ajili ya kumshauri Rais na wasaidizi wake kuhusu namna bora ya kufanya ili kulinda rasilimali za taifa ziweze kulinufaisha taifa. KWA KUANZIA TUTAZAME HILI LA MCHANGA WA MADINI NA MATOKEO YA TAARIFA YA KAMATI ILIYOUNDWA NA RAIS. NAAMINI RAIS ANA LENGO ZURI SANA KUHAKIKISHA RASILIMALI ZETU ZINALINUFAISHA TAIFA. HUENDA KILA MTU ANA JAMBO LA KUTAKA KUSEMA LAKINI HANA NAMNA BORA YA KUSIKIKA AU HANA MAHALI PA KUSEMEA KAMA NILIVYO MIMI . TUITUMIE JF KUMFIKIA RAIS. WALE WAKOSOAJI NI VYEMA WAUONE MOYO WA RAIS JINSI ALIVYO NA INTEGRITY YA HALI YA JUU NA LENGO LAKE NI UTAIFA KWANZA. TANZANIA KWANZA. MODS WA JF WASIUNGANISHE UZI HUU TAFADHALI
 
Kwanza nampongeza,pili vyovyote vile iwavyo,mikataba ivunjwe kwa kigezo cha wizi wa mali km walikuwa wanachukua zaid na kuandika wamechukua kidgo,pili migodini kote wapelekwe usalama wa taifs na jeshi,wakafanya kazi,tatu, atulize kichwa katika hili akae na wanasheria wa govt waone wap pa kupitia
 
Nina 100% akiingia kwenye gesi kuna madudu ya ajabu huko ,hapo ndipo watu wa "ntwara" watapojua jamaa zao waliuawa bure na ilikua ni white elephant venture
Halafu Magufuli anamuachaje Chenge kwenye hii mikataba ya madini ikiwa amekalia ile office tangia 1995-2010 ?
 
Hapo Mkuu tupo pamoja na Jpm kabla hata hajagombea uraisi alilaaani hii kitendo ya kubeba hadi mchanga
Hio clip ipo alikua akisema nikiwa rais haitatokea hawa watu wakabeba hadi mchanga
Huku kitwanga akimambia kachkue fom sasa ugombee urais
Hio vdeo clip nayo
Sasa kwa hilo tu hili swala lipo wazi kabxaa kua hawa watu ni wezi wa dhahir kabxxaaa kama hoja ni mikataba sawa lakini mikataba inaelezea uchimbaji wa madini ya dhahabu
Sasa nahio madini mengine inakuaje?
Mimi nimchimbaji mdogo nafahaam wazi kua dhahab inaambatana na madini mengi
Kifupi namsapot mh MAGUFULI NA YEYE PIA NI MCHIMBAJI HUYO RAIS WETU ANAYAJUA MACHUNGU HAYO
KAMA KINA TUNDULISU NA ZITO WANADAI MIKATABA ITAWAKAMATA
BASI IWAKATE WALIOFUNGA NAO HIO MIKATABA
LAKINI SIO MH.MAGUFULI
WATZ LAZMA TUAMKE JAMAA TUACHE SIASA WALA USHABIKI KUPIGANIA HAKI YETU NA RASIMALI ZETU
MAGUUUUU PIGA KAZIIII
HAPA KAZI TU
 
Ndugu wanajukwaa. Ninayo heshima kwenu kuanzisha uzi huu maalum kwa ajili ya kumshauri Rais na wasaidizi wake kuhusu namna bora ya kufanya ili kulinda rasilimali za taifa ziweze kulinufaisha taifa. KWA KUANZIA TUTAZAME HILI LA MCHANGA WA MADINI NA MATOKEO YA TAARIFA YA KAMATI ILIYOUNDWA NA RAIS. NAAMINI RAIS ANA LENGO ZURI SANA KUHAKIKISHA RASILIMALI ZETU ZINALINUFAISHA TAIFA. HUENDA KILA MTU ANA JAMBO LA KUTAKA KUSEMA LAKINI HANA NAMNA BORA YA KUSIKIKA AU HANA MAHALI PA KUSEMEA KAMA NILIVYO MIMI . TUITUMIE JF KUMFIKIA RAIS. WALE WAKOSOAJI NI VYEMA WAUONE MOYO WA RAIS JINSI ALIVYO NA INTEGRITY YA HALI YA JUU NA LENGO LAKE NI UTAIFA KWANZA. TANZANIA KWANZA. MODS WA JF WASIUNGANISHE UZI HUU TAFADHALI
Wakosoaji wa Raisi ktk hili ni wezi na maharamia WALIOHONGWA NA MAKAMPUNI HAYA KWA PESA NYINGI. Watu kama akina ZTO. Ni watu wanaoimba na kuanzisha vyama vya uzalendo kumbe kinyume chake ni kutumia vyama hivyo kupiga dili.Aibu sana kwa wasomi wa nchi hii.Uzalendo hakuna.
 
Wakosoaji wa Raisi ktk hili ni wezi na maharamia WALIOHONGWA NA MAKAMPUNI HAYA KWA PESA NYINGI. Watu kama akina ZTO. Ni watu wanaoimba na kuanzisha vyama vya uzalendo kumbe kinyume chake ni kutumia vyama hivyo kupiga dili.Aibu sana kwa wasomi wa nchi hii.Uzalendo hakuna.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom