Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Rais wetu Dr. John Joseph Pombe Magufuli ni Rais sahihi kwa Tanzania yetu. Magufuli ana faa sn kuwa Rais wa Tz. Tz ilipokuwa imefiki, Rais kama JPM alihitajika sana. Watu karibia wauze nchi yote!!!! Kila sehemu wizi!! Kila sehemu pa mtu!!
Binafsi nampenda sn JPM ila afanyie maboresho mapungufu yafuatayo:
1. Udikteta. Yaani yy ndie anafahamu kila kitu nchini, wengine wote hatujui kitu. Na kwame naomba asiige Utawala wa Rwanda. Rwanda ni ndogo sn, kueneza hiyo style ya Utawala Tz itamchukua si chini ya miaka 10-15 na muda wake utakuwa umeisha. Hivyo raia hatuta ambulia kitu isipokuwa manung’uniko. Amekaribia kutupangia muda wa kulala mwisho saa 4 usiku.
2. Akubali kushaulika na kukosolewa. Hii ni sifa nzr kwa Mwanasiasa.
3. Akomeshe mauawaji. Mauwaji siyo hulka ya Watanzania. Watanzania wana hulka ya kupendana sana. Kama kuna genge la chama au chombo chochote linafanya ukatili huu alishughulikie, awakataze, na kulivunja kama KIBITI.
4. Democracy/Multipartism. Aruhusu uhuru wa Habari na kujieleza. Pia mfumo wa vyama vingi Tz siyo wa bahati mbaya bali ni wa makusudi na una manufaa yake. Siasa ni ajira. Unapo zuia siasa unakosesha watu kazi. Pia kupitia Demokrasia na mfumo wa vyama vingi Rais hukosolewa na kujifunza na kufanya vyema zaidi.
5. Nyumba alizo uza azirudishe. Uwezo anao iwapo atakuwa na dhamira na nia hiyo. Kwani nyumba zile nyingi zipo City Centers na Strategic Places mfano, karibu na Mahakama, Office za Mikoa, nk. Atenge Budget ya fidia. Naamini fidia yake ni ndogo sn ukilinganisha na hasara za kupangisha watumishi au kuishi hotelini. Hii itamuondolea doa na kupunguza Criticism za Wapinzani wake.
6. Aboreshe sera zake za uchumi. Hakuna Private kompany kwa miaka 2 itakayo ripoti ongezeko la mauzo au faida. Nyingi zimepenguza uzalishaji, Redundacy, na zingine kuuzwa (TBL, ACACIA), zingine kusimamisha uzalishaji (DANGOTE) na nyingi zimeshindwa hata kulipa mishahara (Wana madeni hadi miezi 6). Tutarajie MASS UNEMPLOYMENT akiendelea na sera zake hizi!!! Vyuo vikuu vingi vimekufa!! Na vingi vimeshindwa hata kulipa mishahara (un employment soon). Uchumi kiwe kipa umbele ya sera zako mwaka 2018. Angalia Rais wa Russia Putin anachofanya, ni ujasusi wa kiuchumi siyo wa MAUAWAJI!!
7. Hotuba: Nampenda sn JMP. Anaongea kitu toka rohoni. Ana nia njema kabisaa na Tz. Japo jazba humuzidi na kushindwa kujizuia na kujikuta ameongea lugha/maneno ya kutisha (Singida speech), kuogofya, au kutukana (Bukoba-tetemeko speech). Hii si sifa nzr kwa Rais kwa wananchi wake!! Kauli zake zimefanya watu wamchukie hata walio mpenda!! Kwa sasa yy ni Rais wa wote, uwe CHADEMA, ACT, CCM, CUF, TADEA, NLD, nk.
Kurugenzi ya Ikulu-Ndg Geryson Msigwa na Mkurugenzi wa TISS- Mlazimisheni Rais kusoma Hotuba. Apende asipende. Nchi si mali ya Rais. Ni mali ya Raia wake. Rais ni mtu tu, atapita ila amani na umoja wa Watanzania ni mhimu mno kuliko CCM nzima!! Nakuombea Mungu akusaidie ulimudu hili Rais wangu.
8. Tenganisha kofia ya CHAMA na U RAIS. Muda wako wa kutajataja CCM umeisha!! Huwa unasababisha vijana nyuma ya mikutano yako kukuzomea au kuguna. Hii haina mantiki kwako. CCM ni chama kubwa huna haja ya kuanza kampeni kwa sasa, utashinda tu hata 2020. Jikite katika utendaji uliotukuka. Uliosababisha upendwe na kila Mtanzania ukiwa Wizara ya Ujenzi. Toa msamaha kwa wafungwa wote na walio CELLO POLISI kwa Makosa ya kisiasa, uchochezi, kukosoa, na viongozi wote wa vyama pinzani na ww. Kujisahihisha ni jambo jema, hakuna aliye mkamilifu chini ya Jua. Naamini hata Mungu atakupunguzia dhambi zako.
Nadhani hata huyo Mange Kimambi, hakuchambi kwa mazuri ila kwa Mabaya yako!! Yaani Rais hujawahi hata siku 1 kukemea haya mauaji , utekaji na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea nchini? Rais gani ww?
9. KUWA NA JOPO LA USHAURI. Usitoe kauli yoyote bila kulishirikisha hili japo. Kamwe usikubali kushauriwa na hawa VILAZA wa DAR. Wengi wana utoto, mihemko na ufinyu wa Maono kama viongozi. Iwe ni timu ya (TISS, WACHUMI, JWTZ, WAHADHIRI, WATAFITI, WANASAYANSI, nk).
Ukifanaya hayo 2020 huitaji kampeni kuingia IKULU. Ila ukiendelea na siasa zako za sasa 2019/2020 hadi mnyakue masanduku ya kura vituoni ndio mshinde!!
WAVIVU, MAFISADI NA WEZI WOOOOOTE LALA NAO MBELEMBELE KWA MBELE.
MUNGU AZIDI KUKUONGOZA RAIS WANGU. NAKUPENDA SANA.