Ya kwangu naelekeza kwa idara ya uhamiaji. Naamini Serikali itakuwa imegharimia fedha za kutosha kuwa na mfumo uliopo wa maombi ya pasi za kusafiria.
Mtu anapotoa maombi anaweka namba zake za simu, na ukiangalia ule mfumo unatoa mwanya wa kufiluatilia hatua ya maombi ya pasi ilipofikia, lakini cha kusikitisha hicho kisehemu hakifanyi kazi.
Ukiamia upande mwingine, pamoja na mwanachi kutoa namba ya simu, inamlazimu kwenda kurundikana ofisi za uhamiaji kuulizia kama pasi yake ipo tayari.
Mapendekezo
Watu wa mifumo wa idara waweze sehemu ya ufuatiliaji wa hati ufanyike online. Ili baafa ya mwananchi kuwa amekwisha kamilisha maombi yake na kufanya malipo aweze kuona hatua iliyopo mpaka siku inapokuwa imekamilika
Simu za waananchi zinazowekwa kwenye maombi zitumike kuwajulisha siku ya kwenda kuchukua pasi na watengewe muda badala ya watu kwenda kukusanyika kwenye ofisi za uhamiaji. Manufaa ya hili pendekezo
a) Itapunguza misongomano isiyo ya lazima ktk ofisi za uhamiaji
b) Maofisa uhamiaji watakuwa na muda wa kutosheleza bila kuwa na mwingiliano kutimiza majukumi mengine
c) Wananchi watakuwa na muda mfupi wa kukaa ofisi za uhamiaji kwa ajili ya kuhudumiwa na hivyo muda mwingine watautumia katika shughuli zao za uzalishaji iwe ni ktk biashara, maofisini, hospitalini, viwandani, ktk kutoa ushauri nk.
Wanaomsaidia Rais ktk eneo hili walitupiye macho ili kuboresha kwa manufaa ya taifa.