Wengine kukutana na Magufuli tunaona mkosi, hata ukitulipa hela tutakataa, kwa nini unasema kukutana na Magufuli kutakuwa bahati?
Na kipi ambacho unafikiri unaweza kumuambia ambacho hakijui sasa hivi? Mtu msomi kasoma mpaka Ph.D (hata kama ya kuandikiwa hawezi kukosa kujua the basics), mtu ana nyota zote za serikali zimemzunguka na kumsujudia akitaka kujua lolote anajua, mtu anadukua simu za watu anavyotaka, leo wewe utamwambia nini ambacho hajui?
Kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anajihusisha na uanaharakati wa elimu Tanzania. Msomi kasoma mpaka Harvard.Kisha anajua mambo ya mtaani kupita maelezo.Mjanja kimtaa mtaa na kisomi somi.
Akawa anafanya kazi na NGOs. Akawa mstari wa mbele kuikosoa serikali na kuishauri. Kikwete akamuona huyu anasema sana, ngoja nimuingize serikalini aone mambo yanavyoenda.
Kikwete akampa formal appointment na access zote kwa rais, nafikiri alikuwa mshauri wa rais wa mambo ya elimu. Basi jamaa akawa anakaa na Kikwete anampa makabrasha yake na mipango ya kufanya elimu iwe bora.
Kila jamaa akitoa makabrasha akimpa Kikwete, Kikwete anamjibu hili? Hili tunalijua, tena tunayo ma kabrasha ya studies zilifanyika kwa miaka mingi sana, ukitaka habari zaidi nitakupa mtu wizarani akuoneshe.
Jamaa akija na jipya anaambiwa hili? hili tulishaliundia tume na majibu yako yote haya yapo kwenye ripoti ya tume, naweza kukupa namba ya simu ya profesa aliyeandika ripoti.
Mwishowe jamaa akagutuka, kumbe hawa watu wa serikali tatizo lao si kwamba hawana habari, kwa kweli wao wanajua mambo kuliko mimi. Tatizo ni siasa na machinery ya operation ya serikali, tatizo si kwamba hawajui mambo, wanajua kuliko tunavyofikiri, wana wasomi wengi sana, wamefanya studies nyingi sana. Tatizo si kwamba hawajui mambo.
Jamaa alivyoona hivyo hakukaa sana, alijitafutia kazi sekta ya watu binafsi kimataifa akasepa.
Sasa wewe leo unataka kumshauri Magufuli kipi ambacho hajakijua na hawezi kukijua akiwa na nia?