wana jamvi
nikili wazi Mimi ni Moja ya watu wanaofurahishwa sana na utendaji Wa jpm, na kuna wakati naona hapewi sifa anazostahili.
lakin jumamos ya tarehe 5/10/2019 imefungua upya uelewe wangu, yaan nilisikitika sana kusikia jpm akisema wazi wazi kuwa Haoni mtu Wa kuendeleza mazuri anayoyafanya isipokua yeye tu, akimaanisha huenda itabid aendelee kuwa raisi mpaka akimaliza miradi yake.
swali langu kubwa Kwa raisi wangu jpm ni hili
kwa Kua hatujui Siku Wala saa ya kuondoka hapa dunian ,ikitokea Israel amekuchukua week ijayo unamaanisha Tanzania itakufa ?
kwa kuwa una umri unaoelekea70 na umri Wa mwanadamu kuishi akiwa na Akili timamu si zaid ya 85 ,unamaanisha baada ya miaka kama 20 ijayo Utakua imepoteza utashi,hivyo Tanzania tutapoteana ?
nakuomba sana Raisi wangu Fanya jambo hili Moja ,tutakukumbuka
1.weka mfumo Wa kiutendaji ambao tukitazama maendeleo ya nchi tusifie mfumo na sio mtu , mtu hufa hata ndani ya dakika 1 ijayo lakin mfumo haufi kirahis.
kwa Sasa mazuri yamefanyika juu ya mabega yako Na si juu ya mfumo.
wewe ni mwanadamu ,ni udongo tu ,ni maiti ya kesho ,mazuri unayoyafanya yatapotea siku Moja maana hayajajengwa juu ya mfumo.
wezesha mahakama,bunge na serikali kuu zifanye kazi kimfumo.
utapata wapokezi wako wema na wenye uelewa huenda mkubwa kuliko wako huko mbelen,
ni Mimi kijana ninayeandika haya nikiwa na huzun sana maana sijui cku Wala saa utakapotutoka