Maoni ya Katiba Mpya: CHADEMA yaenda arijojo

GeniusBrain

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2010
Posts
4,315
Reaction score
309
Tumesoma kwenye magazeti ya leo (26.08.2013) kuhusiana na Babu Slaa kulalamika kwa kauli ya Mh. Kinana (katibu mkuu wa CCM) ya kwamba CCM imekusanya maoni ya zaidi ya wanachama wake milioni mbili na nusu kuhusiana na maoni ya mabadiliko ya katiba. Maoni haya ya CCM yamekusanywa kutoka wanachama wake ambao wanakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 6 nchi nzima (Hii ni sawa na 42% ya wanachama wake ndio wametoa maoni hayo).

Cha kustaajabisha ni kwa jinsi Slaa alivyo shindwa kuchambua tofauti ya njia waliyoitumia wao na CCM. CDM wametumia njia yakutumia mabaraza ya wazi ya mikutano ya hadhara, ila CCM wametumia njia za mfumo wa mikutano yao kwa wanachama wao tu. CDM katika mfumo huo, wameweza kufanya mikutano 48 tu ambayo inakadiriwa ni watu 1.2m ndio waliohudhuria mikutano hiyo tu tofauti na wenzao CCM ambao wamekusanya maoni ya zaidi ya WANACHAMA WAKE 2.5m.

Katika hili CDM wamekwenda arijojo kwa kutofikiria sawa sawa;

1. Walitakiwa mikutano hiyo waitishe kwa wanachama wao, na kwenye sehemu ambazo Tume haikufika sawasawa. Badala yake wamefuata njia za mikutano ya hadhara na kule kule sehemu ambazo Tume ilipita. Hii ina maana hakuna jipya walilokusanya zaidi ya yale tume ilikusanya.

2. Njia rahisi na isiyo na gharama ilikuwa ni ya kupitia kwa wanachama, kwani kwa mfumo ambao CCM imeutumia imekusanya maoni mengi naya watu wengi na gharama zake hazikuzidi Tshs 54m, ila CDM wamekusanya maoni ya wachache na gharama zake ni zaidi ya Tshs 1.45bilioni (ukichukua gharama za Chopa, perdiem etc).

Kwa hili twaweza sema CDM wamekwenda arijojo na hakusoma alama za nyakati za kujua ni njia ipi mwafaka ilitakiwa ya kukusanya maoni haya kwa ubora zaidi na kwa gharama nafuu.
 
mkuu naomba nikuelimishe chadema walichokifanya ni kukusanya maoni ya watanzania kwa kuzunguka nchi nzima na watu wakatoa maoni yao peupe kabisa nimebahatika kuhudhuria mikutano yao na nimeona ni kwa jinsi gani chadema wameweza kupata credibility kubwa kutoka kwa wananchi hii ni jambo zuri balaa kuliko kukaa chini tena ofisini na kusema haya ni maoni ya wanachama wa chama flani.PILi ulichozungumza hapa huenda ukawa hujui au umepitiwa kidogo kilichofanyika na chadema walichokifanya ni kusoma vile vipengele vya rasimu ya katiba na kuiomba jamii waseme wanaonaje kuhusu hivyo vipengele kuliko kutoa maoni mapya. Kiukweli hii imezidisha imani ya watanzania kwa chadema kuwa wao wanawakilisha wananchi kuliko kukaa ofisini na kupokea maoni yao kutoka kwa viongozi wao.
Tumesoma kwenye magazeti ya leo (26.08.2013) kuhusiana na Babu Slaa kulalamika kwa kauli ya Mh. Kinana (katibu mkuu wa CCM) ya kwamba CCM imekusanya maoni ya zaidi ya wanachama wake milioni mbili na nusu kuhusiana na maoni ya mabadiliko ya katiba. Maoni haya ya CCM yamekusanywa kutoka wanachama wake ambao wanakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 6 nchi nzima (Hii ni sawa na 42% ya wanachama wake ndio wametoa maoni hayo). Chakustaajabisha ni kwa jinsi Slaa alivyo shindwa kuchambua tofauti ya njia waliyoitumia wao na CCM. CDM wametumia njia yakutumia mabaraza ya wazi ya mikutano ya hadhara, ila CCM wametumia njia za mfumo wa mikutano yao kwa wanachama wao tu. CDM katika mfumo huo, wameweza kufanya mikutano 48 tu ambayo inakadiriwa ni watu 1.2m ndio waliohudhuria mikutano hiyo tu tofauti na wenzao CCM ambao wamekusanya maoni ya zaidi ya WANACHAMA WAKE 2.5m.

Katika hili CDM wamekwenda arijojo kwa kutofikiria sawa sawa;
1. Walitakiwa mikutano hiyo waitishe kwa wanachama wao, na kwenye sehemu ambazo Tume haikufika sawasawa. Badala yake wamefuata njia za mikutano ya hadhara na kule kule sehemu ambazo Tume ilipita. Hii ina maana hakuna jipya walilokusanya zaidi ya yale tume ilikusanya.
2. Njia rahisi na isiyo na gharama ilikuwa ni ya kupitia kwa wanachama, kwani kwa mfumo ambao CCM imeutumia imekusanya maoni mengi naya watu wengi na gharama zake hazikuzidi Tshs 54m, ila CDM wamekusanya maoni ya wachache na gharama zake ni zaidi ya Tshs 1.45bilioni (ukichukua gharama za Chopa, perdiem etc).
Kwa hili twaweza sema CDM wamekwenda arijojo na hakusoma alama za nyakati za kujua ni njia ipi mwafaka ilitakiwa ya kukusanya maoni haya kwa ubora zaidi na kwa gharama nafuu.
 
Wapi ccm walikusanya hayo maoni kwa wanachama wake? Wanachama wengi wa ccm wanalalamika kwamba hawajashirikishwa na chama chao! Ccm wamejifungia chumbani na kupika data! Hakuna jipya hapo!
 
Nyie lalamikeni tu, CHADEMA wametimiza wajibu wao.

Kamam unadhani hizi ni zama za watu 60 kuamua hatma ya watu mil. 47, basi wewe kweli ni GeniusBrain.

Nakumbuka katiba ya 77 iliandikwa na kina Msekwa wakatoka nje wakatangaza ndio hiyo.

Sasa kama Dodoma kwenye NEC ya MaCCM kuna watu mil. 2, utaeleweka lakini kama Dodoma kuna Milembe hutaeleweka.

Zingatia kiambatanisho chini.
 
mkuu naomba nikuelimishe chadema walichokifanya ni kukusanya maoni ya watanzania kwa kuzunguka nchi nzima na watu wakatoa maoni yao peupe kabisa nimebahatika kuhudhuria mikutano yao na nimeona ni kwa jinsi gani chadema wameweza kupata credibility kubwa kutoka kwa wananchi hii ni jambo zuri balaa kuliko kukaa chini tena ofisini na kusema haya ni maoni ya wanachama wa chama flani.PILi ulichozungumza hapa huenda ukawa hujui au umepitiwa kidogo kilichofanyika na chadema walichokifanya ni kusoma vile vipengele vya rasimu ya katiba na kuiomba jamii waseme wanaonaje kuhusu hivyo vipengele kuliko kutoa maoni mapya. Kiukweli hii imezidisha imani ya watanzania kwa chadema kuwa wao wanawakilisha wananchi kuliko kukaa ofisini na kupokea maoni yao kutoka kwa viongozi wao.

Sehemu walizopita CDM ni zile zile ambazo tume ili pita awali, kwa maana hiyo hakuna jipya. Afadhali wangepita sehemu mpya tungewaelewa, kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo tume haikupita. Suala la gharama liko wazi, hizi taarifa nina uhakika nazo zaidi ya asilimia 100
 
Hapo penye RED CHADEMA do waekwenda arijojo
 
Sehemu walizopita CDM ni zile zile ambazo tume ili pita awali, kwa maana hiyo hakuna jipya. Afadhali wangepita sehemu mpya tungewaelewa, kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo tume haikupita. Suala la gharama liko wazi, hizi taarifa nina uhakika nazo zaidi ya asilimia 100

Uko sahihi mkuu. Bila shaka viongozi wa CHADEMA hawakuelewa nini cha kufanya. Badala ya kuuliza wao walikurupuka tu wakaomba fedha kwa wafadhili wao ili waruke na chopa nchi nzima. Wakasahau kuwa tume ilishafanya kazi hiyo na kinachoendelea ni mabaraza ya katiba kujadili rasimu. Kama ungebahatika kuhudhuria mikutano yao yaani ungewahurumia. Hakukuwa na jipya hata moja
 
Mkuu wa m'a's'a'b'u'l'i naomba uchambuzi wa kina wa mkutano mmoja mmoja angalau kwa ushahidi wa picha

uelewa wako ni kusoma matukio kwa njia ya pichaeeeeee. Unafikiri picha ndo zinajadili katiba!
 
Nyie lalamikeni tu, CHADEMA wametimiza wajibu wao.

Kamam unadhani hizi ni zama za watu 60 kuamua hatma ya watu mil. 47, basi wewe kweli ni GeniusBrain.

Nakumbuka katiba ya 77 iliandikwa na kina Msekwa wakatoka nje wakatangaza ndio hiyo.

Sasa kama Dodoma kwenye NEC ya MaCCM kuna watu mil. 2, utaeleweka lakini kama Dodoma kuna Milembe hutaeleweka.

Zingatia kiambatanisho chini.
Yaani umati wote ni mtu mmoja tu ndiye aliyeshika rasimu ya katiba! Hii ni ajabu kweli. Kweli nimeamini wafuasi wengi wa chadema ni vihiyo
 
Wapi ccm walikusanya hayo maoni kwa wanachama wake? Wanachama wengi wa ccm wanalalamika kwamba hawajashirikishwa na chama chao! Ccm wamejifungia chumbani na kupika data! Hakuna jipya hapo!
Yaani kulalamika ulalamike wewe humu jf uwasingizie wanachama wa ccm! Ajabu kweli hii.
 
Uko sahihi mkuu. Bila shaka viongozi wa CHADEMA hawakuelewa nini cha kufanya. Badala ya kuuliza wao walikurupuka tu wakaomba fedha kwa wafadhili wao ili waruke na chopa nchi nzima. Wakasahau kuwa tume ilishafanya kazi hiyo na kinachoendelea ni mabaraza ya katiba kujadili rasimu. Kama ungebahatika kuhudhuria mikutano yao yaani ungewahurumia. Hakukuwa na jipya hata moja

Ndio maana mkuu tumetumia neno murua " ARIJOJO".
 
Tumesoma kwenye magazeti ya leo (26.08.2013) kuhusiana na Babu Slaa kulalamika kwa kauli ya Mh. Kinana (katibu mkuu wa CCM) ya kwamba CCM imekusanya maoni ya zaidi ya wanachama wake milioni mbili na nusu kuhusiana na maoni ya mabadiliko ya katiba. Maoni haya ya CCM yamekusanywa kutoka wanachama wake ambao wanakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 6 nchi nzima (Hii ni sawa na 42% ya wanachama wake ndio wametoa maoni hayo). Cha kustaajabisha ni kwa jinsi Slaa alivyo shindwa kuchambua tofauti ya njia waliyoitumia wao na CCM. CDM wametumia njia yakutumia mabaraza ya wazi ya mikutano ya hadhara, ila CCM wametumia njia za mfumo wa mikutano yao kwa wanachama wao tu. CDM katika mfumo huo, wameweza kufanya mikutano 48 tu ambayo inakadiriwa ni watu 1.2m ndio waliohudhuria mikutano hiyo tu tofauti na wenzao CCM ambao wamekusanya maoni ya zaidi ya WANACHAMA WAKE 2.5m.Katika hili CDM wamekwenda arijojo kwa kutofikiria sawa sawa;1. Walitakiwa mikutano hiyo waitishe kwa wanachama wao, na kwenye sehemu ambazo Tume haikufika sawasawa. Badala yake wamefuata njia za mikutano ya hadhara na kule kule sehemu ambazo Tume ilipita. Hii ina maana hakuna jipya walilokusanya zaidi ya yale tume ilikusanya.2. Njia rahisi na isiyo na gharama ilikuwa ni ya kupitia kwa wanachama, kwani kwa mfumo ambao CCM imeutumia imekusanya maoni mengi naya watu wengi na gharama zake hazikuzidi Tshs 54m, ila CDM wamekusanya maoni ya wachache na gharama zake ni zaidi ya Tshs 1.45bilioni (ukichukua gharama za Chopa, perdiem etc). Kwa hili twaweza sema CDM wamekwenda arijojo na hakusoma alama za nyakati za kujua ni njia ipi mwafaka ilitakiwa ya kukusanya maoni haya kwa ubora zaidi na kwa gharama nafuu.

Tatizo lenu nyinyiem mnadhani hii ni nchi yenu tu, hii ni nchi ya wote CDM wanapita kwa watanzania kuwaeleza ukweli, kumbukeni kuna watu hawana chama kama wajeda, polisi na mahakama. Nyinyiemu mmewafikiaje hao? Hao wenzenu akina Mansoor wameleta maoni mnawatishia kuwafukuza uanachama sasa unaongea nini wewe!
Puumbafuuuu!
 
CCM walipita njia gani?
Sehemu walizopita CDM ni zile zile ambazo tume ili pita awali, kwa maana hiyo hakuna jipya. Afadhali wangepita sehemu mpya tungewaelewa, kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo tume haikupita. Suala la gharama liko wazi, hizi taarifa nina uhakika nazo zaidi ya asilimia 100
 
mbona hata wana ccm wanalalamika kuwa hawajashiriki kutoa hayo maoni,hizo takwimu za kinana ni za kutunga ili kuwapumbaza watu.
 
Kilichofanyika kwa CCM si wanachama kutoa maoni yao bali wamepata shinikizo kukubali mawazo ya wakubwa wao wa juu maoni yao yapite hasa serikali mbili kuwa ziendelee. Vitini vya mawazo ya wakubwa vipo vingi tu humu mitaani tunaviona na kuvisoma.
 
Tumesoma kwenye magazeti ya leo (26.08.2013) kuhusiana na Babu Slaa kulalamika kwa kauli ya Mh. Kinana (katibu mkuu wa CCM) ya kwamba CCM imekusanya maoni ya zaidi ya wanachama wake milioni mbili na nusu kuhusiana na maoni ya mabadiliko ya katiba. Maoni haya ya CCM yamekusanywa kutoka wanachama wake ambao wanakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 6 nchi nzima (Hii ni sawa na 42% ya wanachama wake ndio wametoa maoni hayo).

Cha kustaajabisha ni kwa jinsi Slaa alivyo shindwa kuchambua tofauti ya njia waliyoitumia wao na CCM. CDM wametumia njia yakutumia mabaraza ya wazi ya mikutano ya hadhara, ila CCM wametumia njia za mfumo wa mikutano yao kwa wanachama wao tu. CDM katika mfumo huo, wameweza kufanya mikutano 48 tu ambayo inakadiriwa ni watu 1.2m ndio waliohudhuria mikutano hiyo tu tofauti na wenzao CCM ambao wamekusanya maoni ya zaidi ya WANACHAMA WAKE 2.5m.

Katika hili CDM wamekwenda arijojo kwa kutofikiria sawa sawa;

1. Walitakiwa mikutano hiyo waitishe kwa wanachama wao, na kwenye sehemu ambazo Tume haikufika sawasawa. Badala yake wamefuata njia za mikutano ya hadhara na kule kule sehemu ambazo Tume ilipita. Hii ina maana hakuna jipya walilokusanya zaidi ya yale tume ilikusanya.

2. Njia rahisi na isiyo na gharama ilikuwa ni ya kupitia kwa wanachama, kwani kwa mfumo ambao CCM imeutumia imekusanya maoni mengi naya watu wengi na gharama zake hazikuzidi Tshs 54m, ila CDM wamekusanya maoni ya wachache na gharama zake ni zaidi ya Tshs 1.45bilioni (ukichukua gharama za Chopa, perdiem etc).

Kwa hili twaweza sema CDM wamekwenda arijojo na hakusoma alama za nyakati za kujua ni njia ipi mwafaka ilitakiwa ya kukusanya maoni haya kwa ubora zaidi na kwa gharama nafuu.
Lazima utumie hesabu na uhalisia katika hili, wananchi tulio na vyama vya siasa na tusio na vyama vya siasa tunaishi pamoja!
CCM wakienda kutuma maoni ni lazima tufahamu sote, swali lini hao wanachama waliitwa kutoa maoni?
Kumbuka uchaguzi wa mwaka 2010 Raisi wako hata hizo kura milioni sita hakufikisha ambazo ni za wanachama tu sasa unataka kuniambia hata wanachama hawakumchagua na hakuna mwananchi hata mmoja tofauti na wanachama wa ccm alimchagua?
hizo takwimu ni za uongo kuanzia idadi ya wanachama hadi idadi ya maoni! labuda wanahesabu wanachama wa TAA+TANU+ASP+CCM=MAREHEMU+WALIO HAI(Toka mwaka 1929 hadi 2013)CCM haina wanachama mil 6 walio hai isingepiga hata kampeni 2010 kama ni kweli basi huyo si raisi wa mioyo ya watanzania ni kiongozi wa CCM .
Sikia wewe hatuko tiari kutumia maoni ya CCM kuleta katiba mpya tutatumia maoni ya wananchi bora hata CDM wametafuta maoni ya wananchi + wanachama.
sasa CCM wanakuja na maoni ya wanachama tu! sikia chadema wana akili sana huwezi kulinganisha mtu mmoja wa CDM na wakina Wasira mia mbili?
Unajua faida ya kuwasikiliza wananchi? CCM hata wanachama hai laki tisa sina uhakika!
KIFUPI HAPO CHINI NI MATOKEO YALIYOTANGAZWA 2010 sasa kama mko milioni sita na kura milioni sita za kiongozi wenu hazikufika huyo ni wa CCM au wa watanzania! Acheni habari za Nape na Kinana wao ni kazi yao kudanganya!

  1. Dovutwa Yahmi Nassoro/UPDP kura 13,176 = 0.15%
  2. Mgahywa Muttamwega Bhatt/TLP kura 17,482 = 0.20%
  3. Rungwe Hashim Spunga/NCCR-Mageuzi kura 26,388 = 0.31%
  4. Kuga Peter Mziray/APPT Maendeleo kura 96,933 = 1.12%
  5. Lipumba Ibrahim Haruna/CUF kura 695,667 = 8.06%
  6. Slaa Willibrod Peter/CHADEMA kura 2,271,941 = 26.34%
  7. Kikwete Jakaya Mrisho/CCM kura 5,276,827= 61.17%
 
mkuu mchakato wa sasa si kukusanya maoni ili katiba iweje bali ni kukusanya maoni ni jinsi gani wanataka kuboresha rasimu ya katiba.au kwa lugha nyingine wamepita zile sehemu tume imepita ili kuwauliza wale watu waliokwishatoa maoni ni hivyo wnataka maoni yao yawe au kuboresha zaidi.ni hivyo tu elewa
Sehemu walizopita CDM ni zile zile ambazo tume ili pita awali, kwa maana hiyo hakuna jipya. Afadhali wangepita sehemu mpya tungewaelewa, kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo tume haikupita. Suala la gharama liko wazi, hizi taarifa nina uhakika nazo zaidi ya asilimia 100
 
Sehemu walizopita CDM ni zile zile ambazo tume ili pita awali, kwa maana hiyo hakuna jipya. Afadhali wangepita sehemu mpya tungewaelewa, kwani kuna sehemu nyingi tu ambazo tume haikupita. Suala la gharama liko wazi, hizi taarifa nina uhakika nazo zaidi ya asilimia 100
Nakubaliana na wewe kuwa wamepita mlemle tume ilimo pita ila naona akili yako haijui nini kinaendelea yaani huelewi kitu kabisa! Ni hivi tume imechambua maoni walio toa watanzania, imeyachambua na imetoa rasimu watanzania wanatoa maoni sasa juu ya rasimu iliyotolewa mfano kama mabwege wenzenu wanavyosema kuwa kifungu cha rasimu ya katiba kinachosema tuwe na serikali tatu kiondolewe na tubaki na serikali mbili maana yake ametoa maoni juu ya rasimu ya katiba! sasa unataka wakenya au waganda ndio wakatoe hayo maoni?
yaani mnatia fora ya ujinga na upumbavuuu humu nyinyi ma-ccm, kuweni na akili hata hujui nini kinaendelea unachangia eti wanapita mlemle!
kwa hiyo hayo maoni ya wana CCM wamewatafuta wanchi gani? ambao hawakushiriki wakati tume inakusanya maoni?
Kila siku nasema Ma-CCM mia mbili ni sawa na mbunge mmoja wa CDM na tena watu wenyewe wawe mawaziri si majinga majinga kama wewe na wenzako wale wa ndioooooooooooooooooooooooooooo kwa kila kitu mle bungeni, namaanisha wale CCM ilio chuja na kuona hawa ndio afadhali na kuwapa uwaziri!
 
Hivi ni lini CCM imekusanya maoni ya sisi wanachama kwenye mashina sijawahi kusikia hata mkutano tu wa shina hapa kwetu Bunju na Tegeta na ndio mjini je huko vijijini hizo takwimu za kinana nizakupika tu.
 
Back
Top Bottom