GeniusBrain
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 4,315
- 309
Tumesoma kwenye magazeti ya leo (26.08.2013) kuhusiana na Babu Slaa kulalamika kwa kauli ya Mh. Kinana (katibu mkuu wa CCM) ya kwamba CCM imekusanya maoni ya zaidi ya wanachama wake milioni mbili na nusu kuhusiana na maoni ya mabadiliko ya katiba. Maoni haya ya CCM yamekusanywa kutoka wanachama wake ambao wanakadiriwa kufikia zaidi ya milioni 6 nchi nzima (Hii ni sawa na 42% ya wanachama wake ndio wametoa maoni hayo).
Cha kustaajabisha ni kwa jinsi Slaa alivyo shindwa kuchambua tofauti ya njia waliyoitumia wao na CCM. CDM wametumia njia yakutumia mabaraza ya wazi ya mikutano ya hadhara, ila CCM wametumia njia za mfumo wa mikutano yao kwa wanachama wao tu. CDM katika mfumo huo, wameweza kufanya mikutano 48 tu ambayo inakadiriwa ni watu 1.2m ndio waliohudhuria mikutano hiyo tu tofauti na wenzao CCM ambao wamekusanya maoni ya zaidi ya WANACHAMA WAKE 2.5m.
Katika hili CDM wamekwenda arijojo kwa kutofikiria sawa sawa;
1. Walitakiwa mikutano hiyo waitishe kwa wanachama wao, na kwenye sehemu ambazo Tume haikufika sawasawa. Badala yake wamefuata njia za mikutano ya hadhara na kule kule sehemu ambazo Tume ilipita. Hii ina maana hakuna jipya walilokusanya zaidi ya yale tume ilikusanya.
2. Njia rahisi na isiyo na gharama ilikuwa ni ya kupitia kwa wanachama, kwani kwa mfumo ambao CCM imeutumia imekusanya maoni mengi naya watu wengi na gharama zake hazikuzidi Tshs 54m, ila CDM wamekusanya maoni ya wachache na gharama zake ni zaidi ya Tshs 1.45bilioni (ukichukua gharama za Chopa, perdiem etc).
Kwa hili twaweza sema CDM wamekwenda arijojo na hakusoma alama za nyakati za kujua ni njia ipi mwafaka ilitakiwa ya kukusanya maoni haya kwa ubora zaidi na kwa gharama nafuu.