Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Maoni ya kikosi kazi, kilichokuwa kikiongozwa na Profesa Mkandala, kimewasilisha rasmi maoni yake kwa Rais Samia, iliyoyakusanya kutoka kwenye makundi mbalimbali ya wananchi.
Hata hivyo nimeshangazwa Sana na kauli iliyotolewa na Rais Samia baada ya kuyapokea maoni hayo, kuwa maoni hayo ya kikosi kazi, siyo amri kwa Serikali.
Hiyo ina maana kuwa Serikali inaweza ikayatekeleza maoni hayo au isiyatekeleze!
Ifahamike kuwa maoni ya kuibadilisha Katiba yetu ni ya muda mrefu Sana, toka kwa wananchi walio wengi hapa nchini, kuwa Katiba tuliyo nayo ni ya mfumo wa chama kimoja, kwa hiyo haitufai kwa Sasa, wakati nchi ipo kwenye mfumo wa vyama vingi, kwa hiyo wananchi hao, wanataka iandikwe upya Katiba hiyo.
Kama tunaambiwa kuwa madaraka yanatokana na wananchi na wananchi hao hao ndiyo wanaosema kuwa mfumo wetu wa kisiasa na kiuchumi ni LAZIMA ubadilike na Ili ubadilike ni LAZIMA tubadili Katiba yetu, inakuwaje Rais wetu, atamke maneno ya jeuri kiasi hicho, eti maoni ya kikosi Kazi, siyo amri kwa Serikali?
Tunajua kuwa serikali hii ya CCM hawapendi kabisa kuibadilisha Katiba hii, kwa kuwa wao ndiyo wanufaika kwa kiasi kikubwa na Katiba hii ya Sasa tuliyonayo.
Hata hivyo ninachowaomba watawala wetu wa CCM, wajali maslahi mapana ya nchi, kama wananchi walio wengi, ndiyo wanaosema kuwa Katiba tuliyo nayo hivi Sasa, haitufai kwa sasa, kwa kuwa imepitwa na wakati, iweje yeye Rais atamke kuwa Serikali yake hailazimiki kuyafuata maoni hayo ya wananchi?
Niwasihi watawala wetu, ni vyema mkasikiliza maoni ya wananchi, kwa kuwa wananchi hao ndiyo waliowaweka madarakani na hampaswi kusema kuwa mna hiyari ya kuwasikiliza wananchi hao au laa!
Maneno yaliyotolewa na Rais Samia ya kusema kuwa Serikali yake inaweza kuyafanyia marekebisho maoni yaliyotolewa na wananchi au isiyatekeleze, ni maneno ya hatari Sana, ambayo yanaweza yakasababisha machafuko hapa nchini, hata kufikia umwagikaji wa damu hapa nchini.
Niwasihi Sana watawala wetu, wasingoje hadi nchi yetu ifikie umwagikaji damu, kama ambavyo imetokea kwa baadhi ya mataifa mengine, bali muyatekeleze kwa kuwa ndiyo maoni ya wananchi na muepuke kuitumbukiza nchi yetu kwenye machafuko makubwa.
Mungu ibariki Tanzania